Showing posts with label UCLA. Show all posts
Showing posts with label UCLA. Show all posts

Thursday, August 09, 2007

Bongoland II ndani ya Bongo

Mimi na Josiah Kibira. Bwana Kibira ametunga sinema ya Bongoland II, ameuongoza na amecoordinate production. Pia ni Producer. Bongoland II ni sinema yake ya tatu, sinema zake zingine ni Bongoland I na Tusamehe.
Cameraman Sam Fischer na Soundman Alex Alvarez, wakijadili jinsi watavyopiga scene huko Mikocheni B. Josiah Kibira akitoka kucheki kuwa set up ya scene iko tayari.
Huyo ni Patrick kutoka Sofia Records akicheki scene kwenye camera.
Mimi na Peter Omari. Katika Bongoland II nimeigiza kama dada yake Zaina.

Thecla Mjatta na Peter Omari wakifanya scene katika Bongoland 2.
Director Josiah Kibira, akijadili jinsi ya kupiga scene.
Ndani ya hiyo nyumba kulikuwa na makochi imported, utadhani za IKEA.
Crew na interns kutoka UCLA wakijadili jinsi ya kupiga scene huko Mikocheni B.
Dada Thecla Mjatta yuko tayri kufanya scene yake.


Sunday, July 15, 2007

Maendeleo Bongoland II

Tunapiga hatua katika shooting ya sinema, Bongoland II. Juzi tulipiga scene ya Car Chase Manzese, na watu kukimbia kwenye vichochoro vya huko. Authentic hasa. Wacha nikanyage maji machafu ya bafuni, si mnajua Manzese hakuna sewage system!

Sinema ina mapenzi, lakini kwa sasa sisemi ni kati ya nani na nani. Mtaona wenyewe.

Bwana Kibira amekutana na problem ya actors wa Bongo kutaka kuigiza kama zile sinema za Nigeria. Kuna mikasa mpaka unaweza kuanguka chini kwa vicheko. Hivyo actors wengine wa awali wamebadilishwa. Lakini anajitahidi sana kuwapa training ya style anayotaka kwanza, wakishindwa ndo kwa heri. Mama Mjatta na Mzee Olotu ni A+ actors.

Watu wamekuwa freshi kweli kila sehemu tukienda ku-acti. Na picha zimepigwa kibao.

Juzi cameraman wetu Sam Fischer, alianguka na kuteguka mguu. Alikuwa analia kwa maumizu, ikabidi apelekwe hospitli. Lakini mzungu wa ajabu huyo hajaomba evacuation, anabaki na kuendelea kushuti na magongo yake.

Kichekesho. Tuko na mabinti wa chuo kikuu cha UCLA, sasa hivi wamebakia wawili tu., tulianza na kumi. Wanataka kula maisha tu. Bwana Kibira alienda Slipway kwenye shughuli fulani. Huko si ndo kakutana na moja wa hao mabinti akishuka kwenye boti akitokea sijui kisiwa gani. Kibira kamwuliza kwa nini hakwenda kwenye seti. Yule binti alikuwa hana la kusema. Pia tuna interns wa Bongo wanaotoka kampuni ya Sofia Records.