Sunday, July 15, 2007

Maendeleo Bongoland II

Tunapiga hatua katika shooting ya sinema, Bongoland II. Juzi tulipiga scene ya Car Chase Manzese, na watu kukimbia kwenye vichochoro vya huko. Authentic hasa. Wacha nikanyage maji machafu ya bafuni, si mnajua Manzese hakuna sewage system!

Sinema ina mapenzi, lakini kwa sasa sisemi ni kati ya nani na nani. Mtaona wenyewe.

Bwana Kibira amekutana na problem ya actors wa Bongo kutaka kuigiza kama zile sinema za Nigeria. Kuna mikasa mpaka unaweza kuanguka chini kwa vicheko. Hivyo actors wengine wa awali wamebadilishwa. Lakini anajitahidi sana kuwapa training ya style anayotaka kwanza, wakishindwa ndo kwa heri. Mama Mjatta na Mzee Olotu ni A+ actors.

Watu wamekuwa freshi kweli kila sehemu tukienda ku-acti. Na picha zimepigwa kibao.

Juzi cameraman wetu Sam Fischer, alianguka na kuteguka mguu. Alikuwa analia kwa maumizu, ikabidi apelekwe hospitli. Lakini mzungu wa ajabu huyo hajaomba evacuation, anabaki na kuendelea kushuti na magongo yake.

Kichekesho. Tuko na mabinti wa chuo kikuu cha UCLA, sasa hivi wamebakia wawili tu., tulianza na kumi. Wanataka kula maisha tu. Bwana Kibira alienda Slipway kwenye shughuli fulani. Huko si ndo kakutana na moja wa hao mabinti akishuka kwenye boti akitokea sijui kisiwa gani. Kibira kamwuliza kwa nini hakwenda kwenye seti. Yule binti alikuwa hana la kusema. Pia tuna interns wa Bongo wanaotoka kampuni ya Sofia Records.

8 comments:

Anonymous said...

Kwa kifupi Ndugu zetu hawako serious na kazi wanapenda starehe na kuwasimamnga wanao earn kwa jasho. Kuna mtu amesema mtoa semina please kabla hamjarudi chondechonde mfanye hivyo kwa maendeleo na manufaa ya bongowood.Tufafanulie vizuri wanatakje kuwa kama wanigeria? wameniudhi sana!!! ila Poleni

Anonymous said...

We jijengee maadui tu kwa kuwasema wana wa wenzio. ni bora utupu habari njema kuliko kutupea udaku

Unknown said...

Kinachotakiwa kuwa na moyo ndio tunaanza picha za kmataifa. Polepole si unatujua wabongo
watazoea tu kumbuka kila kitu kina Mwanzo na maendeleo by kennytz. Angalia blog www.kennedytzblogspot.com

Anonymous said...

Nasikitika kwa namna unavyoonyesha hakuna Jema na maendeleo nyumbani. hilo la waigizaji siliingilii maana sidhani nasifa hizo. unaposema manzese hakuna sewage system unamaanisha nini? unataka kusema tuko nyuma kiasi hicho? sitaki kukubali hilo hata kidogo kwani wengi hapa ndio nyumbani na hilo si ukweli. sikufundisha namna ya kuandika blog yako ila naomba semi nyingine usiangalia kwani zinaweza kuwa onyesha watu picha tofauti kabisa na hali halisi

(son of a peasant)

Chemi Che-Mponda said...

Anonymous wa 5:08PM, nyumba nyingi Manzse zimejengwa kiholela. Hivyo unakuta maji ya bafuni kwa mtu yanapita tu njiani inabidi uyaruke.

Anonymous said...

Hapa ni Kibira naandika comment hii ninikwa Maputo Mozambique. Kwanza si kweli kuwa wanafunzi wa UCLA walipunguka....wote tulioanza nao wote walimaliza program vizuri kabisa. Wanafunzi wote walifanya kazi nzuri kabisa ya kujifunza film production kufuatana na matakwa yao.

Kuhusu huyu mwanafunzi niliyekutana naye...si kweli kuwa alikuwa anatakiwa kuwa kwenye seti. In fact sisi (kibira Films) tulikuwa hatuna uwezo wa kuwa control.

Tafadhali kama unataka kuandika habari kuhusu production ya Bongoland lazima kwanza labda tujadiliane...hata kama ulikuwa kwenye seti ya movie production!!!

Chemi Che-Mponda said...

Hi Josiah,

Asante kwa maoni yako. Salamu zako nilipata kutoka kwa Dada Thecla.

Asante kwa kutoa ufafanuzi juu ya UCLA interns.

Anonymous said...

Hey,mimi nafurahi kuona kuwa kuna msuguano wa kimawazo kuhusu nyumbani,kwanza manzese ya leo sio hiyo jamma anijua,manzse hata saa nane na tax unaingia nyumbani.Kuhusu movies za kibongo,mimi naamini kabisa kuwa fani hii inahitaji msukumo wa kimawazo yaani "ELIMU"ya sanaa hii,haitoshi kujionyesha katika runinga tu,kitu ambacho kinawafanya wajione wamefika ni kutokana na kutokujua maana ya sanaa "kikamilifu",wasanii wetu wengi hujifunza sanaa pale anapofanya mazoezi ya kurekodi,na katika kurekodi haonyeshi tofauti na mtu asiye ijua sanaa,ndio maana hata haki zote za sanaa wengi hawazijui,Elimu ya sanaa kwa vitendo ndio mwanga.Ila manzese kimtindo shwari,dio nyumbani kwetu bwana.