Leo nimesoma kwenye ippmedia.com habari za kifo cha kijana wa Form II, Mussa. Huyo kijana simjui lakini kifo chake kimenigusa. Kimenigusa kwa vile nina ndugu yangu ambaye naye alijiua miaka ya 80 baada ya kuugua kwa muda, lakini alikuwa na Kifua kikuu (TB). Watu walimtania kuwa anao lakini nashangaa hakuwahi kupimwa kujua kama anayo kweli. Na naamini angefuata utaratibu wa matibabu angepona ugonjwa wake japo ingechukua muda mrefu. Wakati huo alikuwa anasoma Form Four, na habari za mdudu zilikuwa ndo kwanza tunaanza kuzikisikia.
Lakini nauliza huyo marehemu Mussa, aliamua kuji-diagnose mwenyewe ndo kaamua basi maisha haina maana na kujiua? Hivi hata kama alikuwa anao hakuwahi kusikia habari za dawa za kurefusha maisha?
Ama kweli inasikitisha na kweli Bongo wanahitaji kampeni kali zaidi ya kuelimisha watu kuwa kuwa na virusi vya UKIMWI haimainishi utakufa mara moja.
*****************************************************************************
From ippmedia.com
Denti ajiua kwa hofu?alihisi anao
2007-08-13
Na Emmanuel Lengwa, Jijini
Mwanafunzi wa shule ya sekondari wa kidato cha pili, ameamua kukatisha uhai wake ghafla kwa kujintia kitanzi kutokana na hofu ya kuhisi ana virusi vya ukimwi. Imeelezwa kuwa mwanafunzi huyo alifikia hatua hiyo baada ya kuugua kwa muda mrefu magonjwa yanayodaiwa kutokana na zinaa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Suleiman Kova amemtaja mwanafunzi huyo kuwa ni Mussa Mwalembe aliyekuwa akisoma kidato cha pili katika shule ya sekondari Ngana. Kamanda Kova amesema kuwa mwanafunzi huyo mkazi wa kijiji cha Makwale wilayani Kyela, alikutwa akiningiinia kwenye mti huku amejining?iniza kwa kamba ya nailoni.
Amesema marehemu alipopekuliwa alikutwa na barua, akielezea kuwa amekata tamaa baada ya kuugua kwa muda mrefu, ugonjwa uliotokana na zinaa. Hata hivyo Kamanda Kova hakuutaja ugonjwa huo uliokuwa ukimsumbua denti huyo lakini amesema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio zima.
Monday, August 13, 2007
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment