Monday, August 06, 2007

Makaburi ya Kinondoni


Makaburi ya Kinondoni yamejaa lakini naona watu bado wanazikwa huko. Je, wanazikwa juu ya wengine? Au wanatupa mifupa ya watu nje kusudi mwingine apewe nafasi? (Nilishuhudia tukio kama hiyo Tabora). Na pia nilisikia eti kuna watu ambao wamenunua viwanja vya kuzika huko kwa ajili ya familia zao. Makubwa maana Kinondoni si makaburi ya umma (public)! Na kuna watu walisema siku hizi Kinondoni wanazikwa watu wazito na wenye uwezo tu, maskini haingii. Duh! Jamani wote si wamekufa, kuna mtu anondoka na hela yake dunia hii?
Nakumbuka miaka ya 80 walifungua Kinondoni Cemetery part II na penyewe sasa pamejaa!
Lakini pamoja na makaburi ya Kinondoni kujaa naona watu bado wanataka ndugu zao wazikwe huko. Mwisho itakuwa kama yale makuburi ya Kinshasa ambako kuzikwa huko mpaka kutoa donge nono!
Na baada ya kuulizia ziaidi niliambiwa hata makaburi ya Sinza, Magomeni na Temeke yamejaa lakini watu bado wanazika tu! Wanasema hata wakichimba na kukuta mifupa wanaendelea kuchimba. Itabidi halmashauri ya jiji watenge sehemu zingine kwa ajili ya kuzika.
Sasa tukikosa sehemu za kuzika itabidi maiti zichomwe moto kama wanavyofanya wahindi (cremation).

5 comments:

Anonymous said...

Eneo lingine litengwe?Sio ishu.Watu wachomwe moto tunapoteza ardhi kubwa sana ambayo ingetuletea manedeleo na fweza za kigeni,imagine Kinondoni cementry pale majengo mangapi yangeinuka,kwanza pangepigwa Apartment Complex kama tatu(3)parking za kumwaga na jiji lingekusanya Franka za kumwaga,Hayo sio delopme?

Chemi Che-Mponda said...

Sasa ndo wahamishe hayo makuburi wapeleke wapi? Umewahi kuona ile sinema ya Poltergeist? Kumbe jamaa walisema kuwa wamehamisha makaburi, kumbe hawakuhamisha badala yake walijenga juu ya makaburi. Balaa ilitokea wale wafu walitokea kudai haki yao.

Makaburi ya Kinondoni yabaki pale pale, maana wakijenga pale watu watapata nuksi. na eno lingine litengwe hata upande wa pili wa barabara, waondoe nyumba zile za kikoloni!

Anonymous said...

yeah ni kweli bi chemi pabakie vile vile pa watu kupigia kipara.baada ya kukosa ma ghetto

Anonymous said...

Kwenye yala makaburi watu wanafanya mchezo wa sex, sasa bora yaamishwe, kifanyike kitu cha maana, kama hao wafu kufufuka na kudai haki zao wangefufu sasa kwa huo mchezo.
Napi ingesaidia watu wengine kufikiria sehemu nyingine za kuzikia maana kuna wengine wanajua kinondoni ndio sehemu nzuri kuzika, kazi kweli kweli wakati mtu waweza zikwa popote pale.

Anonymous said...

upumbavu tuu, tanzania haina uhaba wa ardhi kiasi cha kufikiria suluhisho za kuhamisha makaburi au kuchoma moto waliokufa. Pelekeni maiti kwembe au kisarawe, kuna ardhi kibao kule ya kuzikia.

Cha muhimu labda ni kwamba serikali iondoe utaratibu wa kujengea makaburi kwa sababu kaburi likishajengewa basi mtu mwingine hawezi kuzikwa hapo tena. Na hakuna mfu yoyote anayestahili kupewa pande la ardhi peke yake.