Wednesday, August 22, 2007

Mjue Mwimbaji Maarufu wa Bongo Carolla Kinasha




Huyu ni Dada Carolla Kinasha. Ni mwanamuziki mkongwe wa Bongo. Aliwahi kualikwa kuimba na bendi ya Dr. Remmy na wanamuziki wengine maaraufu.

Carolla namfahamu miaka mingi. Nilisoma naye Zanaki Girls Secondary School. Alikuwa anapenda sana kuimba wakati huo. Alikuwa anajua nyimbo zote za Boney M na ABBA, tena alikuwa anaziimba vizuri mpaka walimu walichukia na kusema kuimba kizungu ni kasumba!

Namsifu sana maana alifuata mapenzi yake ya kuimba japo alisomea sheria. Ana bendi kali sana huko Bongo.

Kwa habari za Dada Carolla nendeni kwenye tovuti yake:
http://www.carolakinasha.com/index.html

7 comments:

KakaTrio said...

Wow hao ndio wanamuziki haswaaaa, ana digirii yake na anaimba ama kweli mziki uko damuni

Anonymous said...

Skeeter Davis, Jim Reeves, na hizo ulizozitaja zili-permeate Mlima wa Kilimjaro!

Unknown said...

Her music is excellent. I love how she blends traditonal Tanzanian music with modern sounds.

Aliko said...

my neighbour my sis ..the credited musician Karola kinasha
hivi dk remy alivyoimba KAROLA NI WEWE? SWALI HILI TUMEJIULIZA SANA SANAA BAGAMOYO
"yule unakula nae eehe adui wako karola wee karola wee"

Anonymous said...

Mie sijawahi kumsikia huyu dada-lakini nimesikiliza track zake-sasa hivi, muziki wake ni mzuri. Sauti yake ni nzito na imetulia, inataka kufanana na yule mwanamuziki wa Congo-Abeti Masikini. Kazi nzuri sana. Nitaaangalai kama naweza kununua CD yako online. Hongera.

Anonymous said...

Hiyo Track 6 kali sana!

Anonymous said...

kama aliimba na Remmy basi ndio yeye alimwimba na mimi nimejiuliza sana sasa nimepata jibu