Saturday, August 04, 2007

Kumbe James Brown ana watoto wengine!

The Godfather of Soul (1933-2006)

Kumbe James Brown ana watoto wengine zaidi ya hao sita aliyowatambua. Asante DNA hao watoto wamethibitisha baba yao ni nani.

James Brown alifariki siku ya Krismasi mwaka jana. Katika wosia wake alitambua watoto wake sita. Huyo ambaye alizaa na mzungu, Tomi Rae bado hajapimwa DNA, lakini James Brown alidai kuwa siyo mwanae maana kipindi hicho alikuwa na matatizo na nguvu za kiume.

Watu 12 walijitokeza wakidai kuwa ni watoto wa marehemu James Brown. Wote walifanya testi ya DNA. Kati ya hao wawili waligundilika kuwa ni kweli ni watoto wake.

Moja wa watoto hao, ni Bi LaRhonda Petitt, ambaye sasa ana miaka 45. Majibu ya DNA yanasema kuwa 99.99 percent probability kuwa yeye ni mtoto wa Brown. Petitt anashukuru kuwa baba yake amaethibitishwa ila anasema kuwa ana masikitiko sana kuwa hakutambulika mapema na maisha yake yalikuwa magumu kutokana na ukosefu wa pesa. Anasema kuwa kila James Brown akionekana kwenye TV basi mama yake angesema, "Yule ni baba yako!"

Hao watoto huenda wakawa na haki ya kudai urithi kutoka estate ya James Brown.

Na hivi karibuni, asante DNA mtoto wa Spice Girl, Melanie Brown amegundulika kuwa ni mtoto wa mcheza sinema Eddie Murphy kama alivyodai.

Sasa huko Bongo wakianza kupima DNA mbona itakuwa ngoma kwa hao wanaume wenye mchezo wa kukataa watoto wao!

Kwa habari zaidi soma :

http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2007/08/04/AR2007080402520.html

6 comments:

Anonymous said...

itakuwa pia balaa maana wengine tunajua baba zetu tulio nao sio wetu kweli ila mama zetu ni "wataalamu" wa kuchanganya wanaume na kuwabambika watoto wanaume wenye uwezo kichumi au msimamo ktk maisha!

KakaTrio said...

Picha za Tanzania ndio umeishiwa hivyo? Manake tanzania ulilalamikia Internet, upo usa sasa na picha ulizopost umezipost kwa uchoyo sana, si ni bora usinge ahidi kitu tu?

Anonymous said...

maricha mwangangu, hapo umenikuna ile mbaya. hawa wanaojifanya na ijiblog vyao na kujidai wana hiki, kile au bongo hatuna mtandao wa kasi, wana taabu.
hata mimi nilimuuliza siku moja juu ya picha eti hazijatoka kwa sababu hajasafisha!looooo. siku hizi kuna digital kamera kibao huhitaji kusafisha wala nini.
au yale ya mjengwa ulipomuuliza virunga ni Rwanda au Congo hajajibu mpaka leo. chukua tano babake maricha wa kiboroloni

Unknown said...

duh hao mambo yakija bongo ni balaa, maana matatizo yataibuka hasa baada ya kifo cha mtu, mwenye uwezo. Nina marafiki ambao baba zao walikuwa na uwezo wakati wa uhai wao, walipo fariki, hata kabla ya mazishi, watot wa pembeni waliibuka, tena wale ambao walikuwa, "hawatambuliki" au amabao walikuwa hawaja jitokeza au kutabuliwa hao mwanzo. DNA itasaidia saana kaitka hali kama hii ingawa hali inaonyesha matokeo yatakuwa accurate

Chemi Che-Mponda said...

stephen,

Hebu fikiria kama kusingekuwa na DNA ina maana hao 12 waliojitokeza wangetambulika kama watoto wa James Brown.

Na maskini huyo dada, kumbe ndo wa kwanza kuzaliwa kwa James Brown lakini hakumtambua maishani mwake. Alisema hakumsaidia mama yake pesa hata kidogo. Lakini na huyo mama yake alikuwa na huruma maana angeweza kudai child support.

Anonymous said...

chemi huo mtambo hupo dar kwa sasa.wewe tu kama unahitaji basi unapimwa! Nyie vipi mambo ya nyumbani not1 richabo