Tuesday, August 14, 2007

Mjue Msanii Mkongwe wa Bongo - Bi Hindu



Bi Chuma Suleiman aka. Bi Hindu, ni msanii maarufu huko Tanzania. Bi Hindu ameigiza katika film na michezo kwenye TV Bongo nyingi sana. Pia ameigiza katika michezo mingi ya redio. Kwa siku hukosi kumwona kwenye television huko Bongo.
Bi Hindu anapenda sana mambo ya usanii na aliniambia alianza miaka mingi sana iliyopita hata kabla ya Uhuru wa Tanganyika. Bi Hindu alisomewa lines zake za kuongea na kuzishika mara moja.
Nilibahatika kukutana naye kwenye siku ya kwanza ya film shoot ya Bongoland II huko Magomeni Dar es Salaam. Katika sinema ya Bongoland II Bi Hindu anaigiza kama mama mwenye nyumba (landlord) wa Juma, wakati anakaa kwenye nyumba ya uswahilini.

2 comments:

eNa said...

Kama hii senema bi hindu yupo tena kama mama mwenye nyumba itakuwa imenoga! maana bi hindu maneno yake tu ni kama ngumi ya tyson na mzimia sana. sijui kam katika hali ya kweli anayazungumza maneno yale. alisomewa kwani kusoma hawezi?

Kibunango said...

Hapana shaka Bi Hindu, ataweza tena kuonyesha umahiri wake katika fani..