Wednesday, August 01, 2007

Poleni mlioko Minneapolis, Minnesota - Daraja laanguka





DOH! Kwa kweli ni makubwa! Sijui kama watasema ni terrorism au vipi.

Daraja kubwa limeanguka huko Minneapolis, Minnesota, tena saa ambazo ilikuwa imejaa magari na watu waliokuwa wantoka kazini. Hiyo daraja inavuka mto Mississippi. Taarifa za awali zinasema kuwa watu kadhaa wamekufa na wengi wamejeruhiwa. Pia kuna wazamaji (Divers) ambao wanacheki mtoni, kuona kma kuna watu kwenye aji. Wanasema magari zaidi ya hamsini yalianguka ndani ya maji.

Pia wanaomba watu watoe damu kwa ajiliya kusaidia waliojeruhiwa.

Mungu awape nguvu waliofiwa, walioumia ma watu wa Minnesota kwa ujumla. Poleni sana.


Kwa habari zaidi someni:

2 comments:

Chemi Che-Mponda said...

Kwa kweli naona kuanguka kwa hiyo daraja bado ni kitendawili. Huenda tutajua siku za karibuni ilikuaje mpaka ilianguka. Sasa watu wengi wanaogopa kuvuka kwenye madaraja.

Anonymous said...

sasa ndugu yangu chemi una kitu gani kipya katika blog yako.
yaani huna la kuvumbua mwenyewe bali kuingia kwenye net za watu na kuiba picha na habari eti watu wasome. kama huwezi kujituma kutafuta chako, funga hii blog hutakufa. itakayokufa ni hii blog yako!
mara mkenya ameuawa na picha kama vile umepiga wewe, kumbe umechota toka yahoo au msn.
leo daraja limeanguka, picha kibao kama vile ulikuwepo huko ms. jamani huu ulimbukeni mwengine.
wengine walipokuwa wanachukua picha za michuzi na kutumia kwenye blog zao, ulikuja juu kama vile wewe ni mke wa michuzi. kumbe mwenzio ana papa la kihaya lililohamia uganda.