Saturday, August 11, 2007
Watoto wa Kileleni Road UDSM
Hapo juu ni picha niliyopiga 1993 huko Kileleni Rd. University of Dar es Salaam. Kutoka kushoto, ni mwanangu Elechi, Pandi (David) Qorro, Selemeni (?) alikuwa anakaa namba 23, Bino, na huyo binti nadhani alikuwa mdogo wake Pandi.
Elechi amemaliza High School hapa Cambridge mwezi wa sita. Anajiandaa kwenda College.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
14 comments:
Jamani chemi naona sasa umeishiwa na topic, haya lahafu? hadithi inaendeleaje? wamekuwa wakubwa au? wanafanya nini, hivi hizi potraits za za 14yrs ago unazifukulia wapi na wewe wakati mwingime mh!!!!
kmbe da chemi una mtoto?umeolewa au?sikujua!bora umetuambia maana sikuwahi kuona ukiongelea kuhusu familia yako ie mume au m(wa)toto.
Nami ningependa kujua hao watoto wako wapi sasa.
Dada Chemi,
Nadhani nawe unafurahia sana raha ya kulea na kuwaona watoto wakikua kutoka wenye nepi/diaper hadi wenye masuti. Nimeliwazwa sana na picha zako mbili, ile ya kitoto cha kuchezea madongo na ile njemba lenye high school diploma.
Da chemi una maana gani, kwani si umesema huyo wa kwanza ni mwanao, sasa wako wapi tena una maana gani, tufafanulie??
Elechi!! Jina kama la mnigeria vile.Huyo baba yake kama ni mnigeria hajakutosa na kupotelea mitini na kukuacha ulee mwanao peke yako kweli?
Mimi nilizaa na mnigeria alikopotelea sikujui hadi leo! Kama wako bado yupo hongera!
Hongera sana Chemi.
Hii ni blog yako. Uko huru kuweka mada au picha unazoziona zinafaa bila kujali matakwa ya wasomaji.
Mimi nimekuelewa kupitia blog ya issamichuzi na pia kupitia blog yako. Bahati nzuri pia nimekuelewa historia yako kupitia blog hii yako - tangu kuzaliwa US, kurejea TZ, masomo, jkt, ndoa, kazi, hadi kurejea tena 1998(?) huko Marekani.
Umepitia kipindi cha raha na machungu kimaisha; na ninafurahi kuona mwanao amefikia hapo alipo.
Namtakia huyo kijana kila la heri na Mungu aibariki familia yako.
Dada Chemi,
Pole kwa kazi. Mimi naomba niambie tu mdogo wako Jessica na Malaika na wale wasichana wengine wawili waliokuwa wanakaa mlimani Dar na group yao sikumbuki ilikuwa inaitwaje, lakini walikuwa na vituko sana hasa kwenye mavazi, niliwapenda kwa kweli, wamejificha wapi??
Nilikuwa nasoma darasa moja na Jessica form 3 na 4 Shaaban Robert, 1987-88 baada ya hapo sifahamu jessica amepotelea wapi. Lakini najua Dada mtu utakuwa unajua. Naomba nifahamishe yuko wapi na anaendeleaje.
Mungu akubariki
nakuonea wivu da Chemi, Hongera sana kwa kulea. hongera dada. Mungu azidi kukuzidishia furaha, amani na upendo. kila mtu atakula kwa jasho lake, unafanya kazi kwa bidii dada na mshukuru Mungu aliyekupa kipaji hiki
Anonymous wa 3:47PM, asante kwa maswali kuhusu wadogo zangu. Wote ni wazima pamoja na hao akina dada wengine wa Black Sisters. Ndo jina la hiyo kundi. Actually moja wa hao Black Sisters aliwahi kuwania taji la Miss Tanzania miaka ya tisini.
Holla at chemiche3@yahoo.com nitakupa habari zaidi.
Anonymous wa 3:19am mume wangu wa kwanza, Prof. Henry Kadete alifariki 1995. Ndiye baba yake Elechi. Alisoma First degree Nigeria.
Anonymous wa 2:28AM kuhusu jina, Elechi, tuliamua kumpa hiyo jina kwa vile majina ya kinyumbani aliyopewa walikuwa nayo watoto wengi kweli katika ukoo wao. Marehemu alikuwa Mnyamwezi. Huko kijijini ukiita jina wanaitika watu watano!
pole da Chemi kumbe ulifiwa na mumeo?nimesikitika sana dear.Mungu akuzidishie nguvu katika maisha yako na malezi ya kijana wako.
Chemi mwanamke mwenzetu tupe uzoefu wako kuhusu mirathi baada ya kufiwa na Huyo Profesa Mumeo.Watanzania wanawake wakifiwa na waume eneo la mirathi ni balaa!
Mimi nilipata shida sana mume wangu wa kichaga alipokufa.
Sina hamu ya kuolewa na dume la kichaga hata liwe na mabilioni ya dola sitaki nilidhulumiwa kila kitu. Wakaniacha mweupe.
Pole sana Dada Chemi, kumbe Mumeo alifariki.
Ila umenitia moyo, kwani unaendelea vizuri na shughuli zako na malezi ya mtoto wako. Mungu akuzidishie.
Jamani!! Dada Chemi umenikumbusha mbali sana!! Mimi nilikaa kileleni...Hongera sana kwa Elechi. Na kaka yake je yuko wapi?
Pandi yupo CBE anafanya Diploma ya Business Admin. Tausi mdogo wake Pandi anasoma Marian Girls bagamoyo yupo form three!! Nimewatumia dada zake Pandi
Post a Comment