Tuesday, August 07, 2007

Maisha


Kuna watu ambao wanaamini kuwa ukifa ndo basi tena, hakuna cha mbinguni wala motoni unageuka vumbi tu. Na kuna watu ambao wanaamini kuwa ukifa unazaliwa tena upya na kurudi duniani kama mtu mwingine.

Ukweli hakuna mtu aliyekufa halafu akarudi duniani kutuambia kifo kilikuaje.

4 comments:

luihamu said...

Da Chemi,
Nabii Peter Toshi aliwahi kusema
EVERY ONE WANTS TO GO TO HEAVEN BUT NON WANTS TO DIE ONLY BLACK JESUS.

GLORY BE TO HIS MAJEST HAILE SELASSI I,KING OF KINGS,LORD OF LORDS,LION OF JUDAH.

Anonymous said...

Chemi, mbona wewe haueleweki kwenye blog yako, mambo haya ya dini hasa ukristo unahitaji mwanga wa theolojia pamoja na falsafa. Sasa wewe hivi vitu ulivisoma lini? Jaribu kuwa makini kwa kila unalolipost kwenye blog yako vinginevyo utakosa wasomaji. Kila art ina maana yake, hivyo usibandike vitu tu pasipo kujua maana yake. Asante.

Unknown said...

Mbona kwenye bibila kuna hadithi za lazaro, na Yesu mwenyewe, alivyofufuka. Hadithi zote zinatoa picha ya kifo na nini kitachotokea baada ya kifo, vile vile katika kitabu cha ufuno, yohana anatupa maono ya mambo yakutarajia baada ya kifo.

Kwa watu wasio amini ukiristo kifo ni mwisho wa maisha , and that is it. Mimi binafsi naamini kifo ni one of life's greatest mysteries. Na hua na pata uchungu hasa ninapopata habari za kijana mwenzangu amefariki, au mtu ambaye yuko chini ya umri wangu. Inauma kila ninapopata taarifa za watu wanavyo kufa ovyo hasa nyumbani. Mawazo haya hunifanya nimshukuru Mungu wa uhai niliyonao, kwani naona ni kupitia neema ya Mungu tu, mimi kuwa hai wakati watu wa rika langu wakifa hovyo.

Mawazo ya kwamba waliokufa wamepumzika hunipa faraja, kwani dunia hii ni dunia ya matatizo, changamoto na stress za kila aina na namna. Lakini nafikiri ingekuwa vyema kila mtu angepumzika pale anapo fikia uzeeni, lakini sote tuwafahamu, we do not live in a perfect world.

Anonymous said...

Eti nini...kwamba ukifa ndo basi...sio kweli...Kinachokufa ni ile body ambayo ndiyo ilitumika kama identity yako hapa duniani kwa wakati huu ukiwa duniani...ila roho huwa haifi....Utazaliwa tena ila ID itabadilika kutokana na wale waliokutana kimwili kutengeneza body yako. sasa roho itakayopuliziwa ni ile ile...cha ajabu ni nini...mimi binafsi ni mwanamke mTZ ila miaka takribani milioni moja iliyopia nilikuwa ni mwarabu tena mwanamme....na enzi hizo tulikuwa tunatumia punda kama chombo cha usafiri. Sikumbuki chochote kuhusu familia yangu ila pale nilipokuwa naishi kwa sasa pamepitishwa reli...matokeo yake mimi na treni ni vitu viwili tofauti.....soma Re-incarnation utapata ideas.....sasa hii body ambayo binadamu anapatiwa kwa kipindi awapo duniani, ina guideline zake ili iweze kuhifadhi ile roho...mojawapo ni AFYA...afya ikilemaa roho inajiondokea zake. Na usiku ukiwa kwenye deep sleep unakuwa kwenye state ya spirits kitu ambacho kitakuwezesha kuwaona marehemu ambao kwa wakati huo mtakuwa kwenye state moja....Lakini kwanini niwape hii lecture bure.....hapendwi mtu lazima kieleweke.....