Monday, August 27, 2007

Mume wa Marehemu Amina Chifupa Anaumwa


Kuna habari kuwa mume wa marehemu Amina Chifupa, Bwana Mohamedi Mpakanjia yuko hoi hospitalini na ugonjwa wake unafanana na ugonjwa uliyokuwa unamsumbua marehemu mke wake. Pia wikiendi kulilkuwa na uzushi kuwa Bwana Mpakanjia amefariki dunia lakini si kweli.

Huko Bongo gazeti la Sani umeandika kuwa Mpakanjia na Kepiteni John Komba, walienda nyumbani kwa mke wa Mpakanjia wa kwanza kuomba msamaha kwa mabaya aliyomtendea.

Kwa kweli kitu ambacho sikufurahi ni ile tendo la bwana Mpakanjia kwenda kwa Spika wa Bunge kutangaza talaka aliyompa mke wake, marehemu Amina Chifupa. Lakini uwongo mbaya hao walikuwa ni chakula kikuu cha mapapparazzi. Bado mapaparazzi watasaka habari zao hata kama jamaa kaugua malaria au mafua.

Tumwombee Bwana Mpakanjia apone na aweze kuendelea na shughuli zake, na kulea watoto wake.

Kwa habari zaidi someni:




**************************************************************************

Kutoka Ippmedia.com

Hali ya afya ya Mpakanjia si shwari

2007-08-25 19:21:22 Na Mwandishi wetu, Jijini

Kuna taarifa kuwa mfanyabiashara maarufu wa Jijini Dar es Salaam, Mohamed Mpakanjia amekumbwa na kile kile kilichomuua mkewe, marehemu Amina Chifupa. Baadhi ya watu walio karibu na familia hiyo wamelidokeza gazeti hili kwamba dalili alizokuwa nazo marehemu Amina siku za mwanzo za ugonjwa wake, tayari zimeanza kuonekana kwa mumewe.

Baadhi ya watu wamedai kuwa kutokana na hali yake kutoridhisha, sasa Mpakanjia kalazwa katika Hospitali Kuu ya Jeshi iliyopo Lugalo Jijini.

Amesema namna ya ugonjwa unaomsumbua Mpakanjia ulivyo ni fumbo linalowashangaza hata wao, hasa kutokana na ukweli kuwa dalili za ugonjwa wenyewe ni kama zile alizowahi kuwa nazo mkewe, marehemu Amina Chifupa.

``Hali yake si nzuri. Hivi sasa, hata anachokizungumza hakieleweki? amedhoofu mno na hata kusimama mwenyewe hawezi. Kwakweli anasikitisha sana,`` akasema ndugu huyo.

Dalili kama hizo pia zililipotiwa kujitokeza kwa aliyekuwa mkewe, marehemu Amina Chifupa, ambaye alifariki dunia Juni 26 mwaka huu katika hospitali hiyo hiyo ya Lugalo. Kabla ya kifo chake, marehemu Amina aliripotiwa kuzungumza mambo yasiyoeleweka na mwili wake kudhoofu kiasi cha kushindwa kuinuka.

Baadhi ya ndugu wa mfanyabiashara huyo wamedai Bw. Mpakanjia alilazwa hospitalini hapo mwanzoni mwa wiki hii. Akizungumzia kile kinachomsibu Mpakanjia, ndugu mmoja wa mfanyabiashara huyo amesema mgonjwa wao hivi sasa ana hali mbaya na kwamba hata kula kwa mikono yake hawezi. Amesema amewekewa mirija kwa ajili ya kumsaidia huku madakitari wakijitahidi kumhudumia.

9 comments:

Anonymous said...

Kwenye gazeti la SANI la jumamosi kuna picha ya John Komba na Mpakanjia, John Komba anamsindikiza Mpakanjia Kigamboni kwenda kuomba msamaha kwa mkwe wake wa kiarabu. Hapo kuna utata ina maana ni kweli Mpakanjia alimuoa binti wa kiarabu wa huyo mzee.

Anonymous said...

Kuna mwanamuziki mmoja aliimba "POPO WALA WENZIO, POPO NAWE UTALIWA!" Hebu nikumbusheni jina lake.

Anonymous said...

Kithuku umeniua mbavu sina za kucheka, this is so funny!!!

Anonymous said...

Hayo Magazeti ya Sani, mnayapata wapi, huku Ugahibuni?

Anonymous said...

Huyo mwanamuziki anaitwa KITHUKU.

Anonymous said...

Sio Wana - Njenje (Kilimanjaro stars) kweli? Katika album ya kwanza nadhani wimbo ulikuwa na mandhari ya kinyamwezi ila sikumbuki jina la wimbo.

Anonymous said...

Hayo magazeti yanatoka TZ bwana na si ughaibuni. We Kithuku huo wimbo mbona sijaelewa unamaanisha nini?

Anonymous said...

jamani tusitiane utata.Gonjwa alimpa mkewe sasa limemrudia.Bora aende mbele kwa mbele,kumtaliki mkewe kinyama alidhani atapona?Kila mtu atayawamba mauti.God bless.

Anonymous said...

Mpakanjia apona!


Mtoa habari wetu ambaye pia ni rafiki wa karibu wa Mpakanjia, Mheshimiwa John Komba (Mbunge wa Mbinga Mashariki-CCM) alilithibitishia gazeti hili hivi karibuni kwa njia ya simu kuwa, afya ya swahiba wake ameimarika.

“Ninachoweza kukuambia ni kwamba Mpakanjia anaendelea vizuri, hana tatizo na madaktari wamethibitisha hivyo, atakuwepo hospitali kwa uchunguzi zaidi, nadhani ataruhusiwa hivi karibuni,” alisema Komba.

Aliongeza kuwa, tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua mfanyabiashara huyo ni msongo wa mawazo, jambo lililomfanya adhoofu afya na kuhitaji uangalizi wa wataalam kazi ambayo imefanywa kwa umakini.

Akielezea uvumi uliozagazwa mtaani siku chache zilizopita kuwa Mpakanjia amefariki Komba alisema, “sielewi nia ya mtu aliyesambaza taarifa hizo, labda niseme ni mwendawazimu ndiye aliyefanya hivyo maana kama ni binadamu asingeshangilia kifo cha mtu”.

Aidha alisema, habari za mtu kufariki lazima zihakikishwe kabla ya kutawanywa, vinginevyo zinaweza kumfanya msambazaji aonekane hana akili mbele ya jamii inayomzunguka kama ilivyotokea.

Habari za kudhoofu afya ya mfanyabiashara huyo zimekuja siku chache tangu Mheshimiwa Amina Chifupa aliyekuwa mkewe kipenzi kufariki dunia, ambapo baadhi ya watu wamedai kuwa Mpakanjia anasumbuliwa na msongo wa mawazo ya kifo cha mwandani wake.