Tuesday, August 02, 2011

Marudio - Miaka Baada ya tukio kaniomba Msamaha!

(Pichani Ukaguzi wa Gwaride Mlale JKT Songea - Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

Naona, kuna 'Anonymous' fulani kagusia hii swala ya yalionipata nikiwa jeshini JKT. Watu wengi wamenitumia e-mail kuulizia details. Nimeamua kuibandika tena. Ni posti ya kutoka April 2006. Lakini mjue enzi za JKT, wasichana wengi walinyanyaswa kijinsia, mimi nilikuwa na bahati maana nafahamu wasichana waliokuwa gang raped. Dada fulani, alimkubali afande, alivyomaliza kaita wenzake kwa kusema, "Njooni, Mboga hii hapa!" Yule dada hakuweza kutembea vizuri kama wmezi baada ya hapo!

*****************************************************************************

Nilipokuwa Jeshi ya Kujenga Taifa (JKT) karibu nibakwe na afande Fulani (jina nahifadhi). Lazima niseme kuwa katika kipindi hicho wanaume wengi waliona makambi ya JKT kama ‘buffet’ ya wasichana. Si maafande wa jeshi tu, bali hata viongozi wa serikali walikuwa wanapitia makambi ya JKT kula tani yao!

Mimi nilikuwa Masange JKT, Tabora. Wakati huo huyo jamaa alikuwa ni Kepiteni wa JKT. Nadhani alidhania kwa vile yeye ni kepiteni basi alikuwa na haki ya kutembea na yeyote aliyemtaka. Kwangu aligonga ukuta! Bila shaka alikuwa hajawahi ‘kunyimwa’ mpaka siku hiyo alipokutana na mimi.

Miaka baada ya tukio nikiwa nafanya kazi Daily News mara nyingi nilikuwa napishana naye Posta Mpya. Basi ananisemesha, na mimi namnunia halafu napita zangu kimya bila kumjibu kwa hasira. Siku moja kanisimamisha kaniambia, "Chemi, naomba msamaha, nisemahe tafadhali, kweli nilikukosea!” Aliongeza kuwa miaka mingi imepita hivyo sina sababu ya kuwa na hasira naye! Na mimi nilimjibu, “Mshenzi sana wewe!” nikaenda zangu.

Ikapita kama mwaka mwiingine. Jamaa anaendelea kunisalimia kila nikimpita njiani na mimi kwa uchungu bado nikashindwa kusema kitu. Basi nikafikiria alichoniambia Posta Mpya. Lakini niliona kama jambo hilo linamsumbua. Na nikasema kama Bwana Yesu aliweza kusamehe watu kwa madhambi yao kwa nini mimi nisimsamehe. Basi baada ya hapo ikiwa nikimwona na akinisalimia naitika na naendelea zangu na nikaona kidogo hata yeye alikuwa na raha.

Lakini bado najiuliza kama kitendo chake kilimsumbua miaka na miaka kama ilivyonisumbua mimi.Unauliza ilikuaje mpaka nikajikuta kwenye situation ya kubakwa. Au mnasema nilitaka mwenyewe. Ngoja niwaelezee ilivyokuwa.

Nilikuwa mhudumu Officer’s Mess, mpishi na msafishaji. Huyo jamaa alikuwa ni mgeni kutoka Makao Makuu ya JKT Dar es Salaam. Kwa kweli sikutaka kufanya kazi pale Mess lakini tulichaguliwa special na Matron, mimi kwa vile niijua kupika vyakula mbalimbali hasa za kizungu. Lakini uzuri wa hiyo kazi ni kuwa uanambulia mabaki ya vyakula (leftovers), na mara nyingine kulikuwa hakuna.

Basi huyo Afande alikaa kambini wiki kadhaa. Katika kumhudumia tukawa tunaongea na mimi nikawa namheshimu kama kaka vile. Wala sikusikia mapenzi yoyote kwake. Basi jioni fulani, kanialika chumbani kwake kunywa soda na biskuti na kwa Maongezi zaidi. Sasa kama ulienda jeshi unajua njaa kali unayokuwa nayo. Nikaenda, kanikaribisha vizuri, nilipewa soda na tukawa tunaongea. Basi nikaona mwenzangu anabadilika ghafla! Mara ananikumbatia kwa nguvu, na kunibusu na mengine. Nikajaribu kuaga lakini jamaa hakuniachia. Baada ya ku-plead naye aniachie, kaniachia. Kaomba msamaha na kaniomba niendelee kukaa nimalize hizo soda alizoninulia.

Kama mjinga nikamwamini, nikakaa nakunywa hizo soda. Tukaendelea na Maongezi, kukaa kidogo huyo kanirukia, najaribu kusimama huyo, kanivuta na kuniangusha kitandani! Mimi saa hizo nikawa naogopa kabisa nia yake!Kaniambia eti, “ukipiga makelele najua nitasema nini! Nyamaza! Huna sababu ya kunikatalia!” LOH! Kanizaba kibao! Nikamwuliza kwa nini anaifanyia hivyo, na mimi nilikuwa namwona kama kaka yangu!Hapo sasa ikaniingia. Nabakwa! Loh!

Nilimpiga mangumi na mateke lakini jamaa alikuwa na nguvu huyo kachana chupi yangu! Baada ya hapo, jamaa kashika miguu yangu huko anafoka kwa sauti kama vile anatoa amri “panua miguu! PANUA MIGUU!” Huko katoa ume wake uliyosimama kwenye suruali! Basi kuona sipanui jamaa kaongeza makofi na kafanikiwa kupanua miguu yangu! Kuona kafanikiwa kupanua huyo kajaribu kupenya. Ilipogusa kwangu nilipiga kelele cha kufa! Nikasema, “Nakuufaaaa!”

Heh! Ghafla jamaa kaniachia kaniambia niende. Alisema, “Nimeigusa na ume wangu, unatosha!” Nenda zako! Na ukimwambia mtu najua nitasema nini!”Loh nilikimbia bwenini na giza lile la Masange huko nalia. Wenzangu wananiuliza vipi, nikashindwa niseme nini! Kwanza niliona haya! Fikiria, niliona haya (shame)!Kesho yake nikaenda dispensary na kujiandikisha mgonjwa. Sikwenda kazini Officer's Mess bali nililala bwenini.

Siku iliyofuatia huyo Afande mshenzi kapita bwenini kwetu kaulizia hali yangu, na mimi huko natetemeka kwa woga nikashindwa niseme nini. Alininunulia Orange squash na biskuti na kuzileta bwenini. Sitasahau alivyonitazama! Ilikuwa kama vile anapanga jinsi gani atanipata. Baada ya hapo alimwopoa msichana mwingine na huyo alimkubali kabisa. Akawa analala kabisa huko Officer’s Mess. Hakuna anayemsumbua wakijua ni bibi wa Afisa. Basi, siku za yule jamaa kukaa kambini zikaisha, na yule binti alienda naye Tabora mjini kwa siku kadhaa. Halafu jamaa karudi zake DSM. Yule binti karudi zake kambini! Kumbe alienda bila pass. Alidhania kwa vile yuko na mkubwa hana haja ya pass. Na yule Afande ndo kaondoka kimoja! Maafande waliobakia wacha wamtese huyo binti alivyorudi kambini! Walimtesa kwa Extra drill na mengine mpaka ikabidi Military Police waombe wakuu wamsamehe la sivyo atakufa. Raha yake iliishia kwa suluba! Sijui yule binti alidhania jamaa atamwoa! Kwa nini alimkubali yule mshenzi.

Anyway, kila mtu na vyake. Alivyotoka kwenye suluba tulimwuguza! Siku haizkupita na mimi nilitolewa kazi Officer’s Mess na kupelekwa kwenye kikosi cha Ujenzi na lazima nisema hapo nilifurahi sana. Basi miaka ilipita. Mimi nilikuwa mwandishi wa habari Daily News, tena nilijenga jina. Sasa nikawa napishana na yule jamaa huko kapandishwa cheo na yuko JWTZ. Jamaa anajaribu kunisalimia na mimi napita zangu kimya, namnunia kabisa.

Nilimwona mshenzi, mnyama, na kila kitu kibaya ndo ilikuwa yeye! Angefanikiwa kuingiza na kunimwagia uchafu wake ningejiona mchafu mpaka leo! Miaka kama 20 imepita sasa na bado nina uchungu naye.Jamani nyie wanaume nawaambia kubaka kinaathari zake kwa wanawake. Unataka raha ya dakika na unamwachia mwenzio na uchungu wa maisha! Wengine mpaka wanakuwa wagonjwa wa akili.

Kwa nini nimeamua kuzungumzia kubakwa kwangu hapa, ni kwa sababu naona wasichana wengi wanabakwa, halafu wanaamua kunyamaza kimya. Kisa wakienda polisi na hospitali wanahofia kuambiwa ni Malaya au walitaka wenyewe! Hata mwamanke mwenzako anaweza kukufokea kuwa ulitaka mwenyewe. Tanzania, wanaume walikuwa na usemi wao kuhusu wanawake na ngono. Walisema eti ukimwomba mwanamke halafu akijibu ndiyo, manake ndiyo atafanya. Akisema labda, manake atafanya, akisema hapana, manake hapana. Lakini jamani tendo si inakuwa tamu kama wote mmekubali? Na kama angefanikiwa kuingiza si angeniumiza sana!

Wengine wanasema ningemshitaki. Je, ningemshitaki ingekuaje? Kwanza jeshini mimi ningepewa Extra Drill mpaka niumie au kufungwa jela ya jeshi iliyojaa maji na mbu kusudi niteswe. Kumbuka ilikuwa Tanzania na yule alikuwa ni Kepiteni wakati huo na mimi nilikuwa Private. Hakuna ambaye angekuwa tayari kunisikia zaidi ya wenzangu maPrivate, na yeye alijua hivyo. SHENZI TAIPU!

30 comments:

mama Jeremiah said...

pole Chemi, manyanyaso kwa wanawake yapo sana tuu. Nashukuru kwa kuirudia hii story kwa faida ya wanawake wote. Ninaamini kabisa umetusaidia sana tuu, na kuzidi kutupa moyo wa kutokuwa waoga, na kujiamini.

Baraka Mfunguo said...

Pole sana. Inaumiza. Wakati mwingine mtu unafanya kitu pasipo kujua kwamba umemkwaza yule ambaye umemfanyia. Haya masuala ya kubakwa kulazimishwa kufanya ngono yapo maeneo mengi na wahanga wapo wengi. Inatokana na mazingira. Wanaume hasa watoto wadogo wanabakwa na kuharibiwa , watu wazima wanabakwa na athari zake ni mbaya sana.

Kuna bwana mmoja aliwahi kubaka msichana akiwa Tanga (JKT) jeshini mpaka leo hana mtoto na anahangaika kupata mtoto. Na kila akikumbuka kile kitendo alichokifanya anajutia anajaribu kumtafuta aliyemfanyia hajui mahali atakapompata. Kweli athari zake ni mbaya sana. Nadhani wapo vijana/wazee ambao wenye michezo ya kubaka hata wafanyakazi wa ndani bila ridhaa ni lazima tuheshimu utu wa mtu wengine walishawahi hata kuwa maofisa wakubwa wa polisi. Imenigusa sana.

Anonymous said...

Dah Chemi nna hakika jamaa alikutomba au alikojoa kabla yakuuingiza ndani (nyege zilimzidi), sababu mwanaume anapokuwa katika hali hiyo hawezi kukuachia wakati ushapanuwa miguu kabla hajakojoa. Ni bao tu ndo litampunguza speed. Bado kunakitu umeficha katika kutuelezea mkasa huu.

Pole sana dada yangu kwa maswahiba hayo, kwakweli ni unyama na ushenzi mkubwa.

Lakini ujufunze kwamba dunia hii hakuna kisicho na gharama " you can't get something for nothing" Soda na biskuiti ulitakiwa uzilipie!

Jacqueline Mushi said...

Pole Da Chemi kwa yaliyokusibu. Kama ulivyosema, haya yalikuwa ni mambo ya kawaida JKT.

Mimi nilikuwa Makutupora JKT na pale kulikuwa na mikikimikiki mingi sana. Pale ndipo wakuu walikuwa wanakuja kupumzikia na kufaidi vibinti vibichi. Hata wabunge walikuwa wanakuja kula vinono pale tena kweupee hata bila kujificha.

Mkuu wa JKT wakati ule (somebody called Makame), Salim Ahmed Salim na wakuu wengineo walikuwa hawakosekani kwenye majumba ya wageni yaliyojengwa milimani. Basi wakiweko wasichana wale wazuri kabisa kutoka kila Kombania ndo wanapelekwa huko kuwahudumia. Walikuweko akina Clara Mamuya, Elizabeth Yongolo, Caroline Chikokoto, Prisca Mtei na wengineo. Wasichana wadogo wazuri kama nini na walikuwa mboga ya wakubwa - akina Makame na akina Salim Ahmed Salim, wabunge na wengineo.

Cha kusikitisha ni kwamba wasichana hawa walikuwa wanafurahia na kututambia sisi "wabaya" ambao tulikuwa hatupati "bahati" hii ya kwenda kuwastarehesha wakubwa. Usiku tukiwa tumelala kwenye mahanga huko ungewasikia wanasimuliana mkubwa yupi ni mkali kitandani, yupi mwenye nanihii kubwa, yupi mwenye kibamia n.k.

Nimefurahi sana kusikia binti mwenye msimamo makini kama wewe. Matatizo mengi na kudharauliwa kwetu wanawake mara nyingi tunajiletea sisi wenyewe tu.

Nimeguswa na kisa chako lakini JKT lilikuwa ni kituo cha unyanyasaji wa mabinti na kupeana UKIMWI.

Mpaka leo nikisikia jina la Salim Ahmed Salim likitajwa huwa nasikia KICHEFUCHEFU.

Wewe ni mwanamke jasiri na Please usiogope kuiweka comment yangu. Imefufua hisia zangu upya!

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni kwa support! Sikutegemea! Wengi wanadhani na jambo la aibu ambayo tuanstahili kuficha. Halafu jamani tusiogope kuongelea hii suala! Nikitaja listi ya viongozi waliopita pale kambini kula vituuz utashangaa. Wengi wamekwisha kufa!

Na wewe mdau wa 4:13AM, amini unachotaka kuamini ila nakuambia jamaa hakufanikiwa kwangu! Sikumpanulia miguu, ingawa alikuwa ananiamrisha nifanye hivyo! No Way! Kinachonisikitisha ni kuwa sidhani kama aliwahi kukutana na mwanamke aliyemnyima kabla yangu!

Lugeye said...

Hongera kwa kwa kuonyesha ujasiri,na kusaidia jamii,mimi naitwa LUGEYE ADOLPH MWANASELE,nilikuwa op miaka 40,ni hivi karibuni tu,mwaka 2002-2008,mimi pia ni mhanga wa tatizo kama lako ila mimi sikutaka kubakwa kama wewe ila nilifukuzwa jeshini pale katika kambi ya STONE QUARRY KUNDUCHI JKT kwa sababu kama ulizozitaja wewe kuwa Afande kutumia cheo chake kunyanyasa watu hasa sie ambao hatutoki familia za maafande,yule afande alikuwa anaitwa afande BAZICHA alikuwa na nyota 2 tu,akishirikiana na kibaraka wake afande MAHELA yeye alikuwa ni staff sajenti,kitu alichoamua kunifanyia mazingira ya kukatishiwa mkataba wangu ni baada ya mimi kua nakataa sera zake za unyonyaji hasa pale alipokuwa anataka sisi service man tukamfulie nguo zake mpaka mashuka yake,na wakati huo utaratibu haupo jeshini inatakiwa anitume kazi za kijeshi hapo kambinilakini sao kwenda nyumbani kwake kumfulia nguo,sasa mimi nilipokuwa nawaeleza vijana wenzangu kuwa mnaonewa yeye akaamua kuweka chuki na mimi akaniundia zengwe kwa CO wakaamua kunisitshia mkataba wangu mm peke yangu,na wakati tulikuwa tumebakisha miezi 2 tu tuajiriwe kweli wenzangu waliajiriwa kasoro mimi tu,ila namshukuru Mungu baada ya kurudi nyumbani nikapata mfadhili wa kunilipia ada ya chuo kwa sasa nasomea ACCOUNTANCY CBE, kitu ambacho napenda kuwashauri Serikali yangu sikivu ni kwamba kuanzia mwaka kesho nimesikia wanafunzi wanaomaliza form six wanaenda jeshini kwa mujibu wa sheria,serikali iwe makini sana na hao watoto wa watu dhidiya maafande wenye tamaa ya ngono,na tukizingatia 75%ya maafande ni waathirika wa HIV,naogopa badala ya kupata tulichokitarajia vijana wakakamavu tukajikuta tunatengeneza Taifa la waathirika wa ukimwi na kama tunavyojua watoto wa siku hizi wanaaanza hayo mambo ya ngono mapema!tuwe makini sana hata ukiangalia zamani waliokuwa wanamaliza form six walikua kidogo ni vijana wakubwa wameshakomaa kiakili lakini watoto wa siku hizi wanamaliza form six bado vitoto kabisa naomba serikali iandae mazingira mazuri kwa hao vijana wanaotegemewa kuingia jeshini mwaka kesho.

Rik Kilasi said...

Duuuh kisa kinatia hasira hiki, pole sana Da Chemi na pia nikupe hongera kwa ustahimilivu wa kushinda huo unyama maana haikua kazi ndogo ati.Pia kama alivyosema mdau mwingine kama kuna mpango wa kurudisha ile system ya wahitimu kidato cha 6 kuingia JKT basi vema serikali itambue uwepo wa unyama huu na kuweka njia za kudhibiti.Hali ya sasa si nzuri kama kutakua na kutakana kimapenzi kinguvu na haya magonjwa yaliyo zagaa taifa litakua pabaya.Ukiachia mbali jeshini nina imani matumizi ya vyeo kuwataka mabinti yapo sehemu nyingi za kazi sasa ile ya Tanzania bila ukimwi naona itakua ngumu sana.

Mtazamo wangu Wanawake wakielimishwa vizuri juu ya haki zao,kutoa taarifa ya unyanyasaji bila kujali nani kafanya au cheo (japo hii ngumu sana kwa Tz yetu) na kujengewa mazingira ya ujasiri kwa maana yakupewa msaada wanapokumbana na dhahma kama hizi basi Tanzania bila ukimwi itawezekana vinginevyo tunapoteza muda na hio kauli mbiu Tanzania bila Ukimwi

Anonymous said...

Pole sana Da Chemi kwa mkasa wako! Nayajua matukio ya jeshini yalivyo na hasa kama u service.
Kuna afande pale Makutupola alikuwa anaitwa Zacharia nadhani, aliwahi kumnyanyasa sana dadaangu lakini tulipoelezwa na kumfahamu huyo afande tukamwekea mtego na kwa vile alikuwa anapenda pombe akaingia kiulaini..
unajua kilichotokea? Kwa hasira nilizokuwa nazo kwa yule afande mie na rafiki zangu watatu tukamfira!! Nilikuwa sijawahi kuwaza hata siku moja kama nitakuja kufanya hicho kitu! tena kwa mwanaume mwenzangu!

Basi jamaa alitushtukia lakini alikuwa nguvu hana na akashindwa cha kufanya halafu tukamwekea kijibarua mfukoni mwake kuwa aache kunyanyasa watoto wa kike kambini akirudia tutazisambaza picha zake (tulijifanya tumempiga picha pia) Haikupita muda nikasikia yule afande kahama ile kambi

Anonymous said...

Mfungulie mashtaka Umoja wa mataifa wa haki za Binadamu.
Alafu mi najiuliza kwa nini kuna mijitu michache ina roho mbaya sanaaaaa kule Tz,tuifanyaje?Wizi ,kunyanyasa wanyonge n.k

Anonymous said...

Kuna kaka amenichekesha hapo juu!! Duh! kweli kuna watu wana hasira mbaya hadi wakamfira afande wa watu! Sasa huyo afande akijiona humu si atajisikia vibaya sana

Anonymous said...

Hivi ni kwa nini wanajeshi wanakuwa na nyege kuliko watu wengine? Yaani vitombi sana hawatosheki hata wakiwa na wake wazuri kiasi! Pole sana Da Chemi

Anonymous said...

Hebu checki huyo Afande anayetembea nyuma ya huyo mama anavyomtazama kwa macho ya kumtamani! Hata haya hana! Kweli wanajeshi ni sex maniacs! UKIMWI umepita huko JKT na JWTZ pia!

Anonymous said...

unayosema ni ukweli mtupu hata me nimepitia jkt ni op jiajiri 833kj Arusha na sasa nimeajiriwa jeshini ebwana sio siri dada zetu wametombwa sn hasa wale wanaopendekezwa kufanya usafi ofisazi mess ndio balaa maana huwa ndio wazuri wanaangalia wenye mvuto kwa hili sio siri na mambo mengi huwa yanatokea ya kuzalilishana ila kwa huku jeshini yote haya ni sawa hakika nimeapa hakuna dada yangu yoyote atakaeenda jeshini nimeyaona mwenyewe na pia nawaonea huruma sn hao form six wanaokuja wakusanye nguvu maana wanawasubiri kwa hamu wakufunzi kuna msemo wetu huo jeshini huwa binti hatemi dawa na hivi wadogo wadogo we acha tu

Anonymous said...

Dada Chem,Pole sana!! yaani nimesoma kisa chako huku nikicheka lakini moyoni nikisikitika jinsi ulivyokuwa unatendewa.

Mimi ni mwanaume na mimi nilikuwa Jeshini Masange tena naamini tulikuwa hapo wakati mmoja huo.Kuna wakati dada wawili fulani hivi walikuwa wanatoroshwa na afande mmoja anawapeleka kijiji cha Mbola kunywa pombe.Nadhani unaweza kukumbuka kijiji cha Mbola kipo kama km 15 magharibi ya Masange JKT unakatiza kale kamsitu ndo unafika hapo.Yaani wale wadada walimaliza Jeshi bila shuruba zozote kwa sababu walikuwa wanagawa uroda kwa huyo jamaa na rafikiye hadi mwaka ukaisha wanapeta kabisaaaaa?

Kama kuna huo mtaji tena kwa vijana wa kidato cha sita kwa kweli nawahurumia mno.Bahati nzuri wanangu ninao ughaibuni tena mwingine ndo angeingia jeshini mwaka huu kma angekuwa bongo.

Kina dada unyanyasaji kijinsia uko kila mahali,hasa maofisini huko bongo ndo usiseme.Na kwa sasa hivi watoto wa kike wananyanyasika sana wanaomaliza vyuo wanapotafuta kazi,yaani suipime rushwa ya kwanza ni ngono kwe kwenda mbele. Wakipewa kazi basi ni difu ya boss kila wakati wengine wakitoka lazima binti abaki kumhudumia mzee kabla hajarudi kwa mke wake.

Jinamizi hili inabidi kina dada mjiweke kidete kuonyesha kuwa mnaweza maisha bila misaada ya hao waheshimiwa.Lakini kitu njaa kibaya sana jamani,maana kinachowafanya mabinti wengi waingie mitego hiyo ni kukosa namna ya kujikimu kimaisha.

Asante Chem, Tuombe Mungu awanusuru mabinti zetu jamani maana kama mwingine alivyosema ukimwi utawamaliza kizazi kijacho.

Hellen Attar Gupta said...

Chemi, POLE SANA/HONGERA SANA.
Hakika, habari yako inagusa moyo wa mtu yeyote yule mwenye imani na mwenye kumwogopa Mungu.
Hapa sasa, kwa faida ya wengine wa sasa na wajao, tuangalie pande zote mbili, kwako na kwa Kapteni.

KWAKO:-
* Japo ulikuwa na uhusiano wa karibu na wa heshima na Kapteni kama kaka, ulikosea kukubali kualikwa chumbani kwake.

* Hilo la kula biskuti na kunywa juice, sijaliona kama tatizo sana, kwa sbb kwa muda mrefu mlikuwa na mazoea ya kaka na dada, na hata vyakula huenda alikuwa anakupatia kwa kukuhurumia unapika na mara nyingine unakosa.

Kwa hiyo wakina dada wajifunze kutokana na makosa.

KWA KAPTENI:
* Amekulipa ubaya kwa wema uliokuwa unamtendea.
* Alidhani labda unampenda kimahaba, ila kwa kawaida mwanamke huwa sio rahisi kumtongoza mwanaume moja kwa moja. Hivyo alivyokualika ukakubali kwenda CHUMBANI KWAKE, alijua tayari umekubali kiaina, hisia zake na kila kitu chake kikawa kimeamka.

Mwanaume rijali, akishaamka ki hivyo, unapomkatalia anakuwa kama kichaa. Laiti kama angekuwa mstaarabu, akagundua kuwa hukwenda kwake ki hivyo, angeuambia MOYO WAKE utulie, atulie, akuache. Lakini huenda alikuwa pia hajapata huduma kama hizo kwa muda mrefu!! Ulitegemea nini natayari upo ndani???

Wanaume, muwe na ufikirio kwa wenzenu. Hata Mungu hapendi mambo ya nguvu na ukatili. Ngono za kupita (Hit and run) zinatesa maisha YOTE kwa mtendewa. Mwisho wa yote mnapata kitu gani???(Kwa wanaume wenye tabia kama hizi). Tendo la ndoa linataka maelewano. Vinginevyo unakuwa kama umekwenda chooni kujisaidia!!!!!

Mhusika akisoma makala hizi, inafaa amwombe Mungu msamaha, na amwombe Chemi hata kupitia mtandao huu. Na kama atakuwa na toba ya kweli, KUTOKA MOYONI, Mungu atamsamehe. Kama hana, hukumu ya Mungu inamngojea.

Atakayependa, asome Mathayo 7:12. Kanuni hii ya Biblia, kama wote tukiitumia maishani, hakutakuwa na ubakaji KAMWE.

Anonymous said...

Pole sana dada lakini Soma comment(s) zangu hapa

Anonymous said...

Yani we dada hujijui jinsi ulivyo shupavu. Bahati mbaya umezaliwa Tanzania nchi yenye upuuzi kuanzia level ya rais mpaka mjumbe wa nyumba kumi. Hafadhali sikuenda huko JKT maana hasira zangu hizi mbona wanajeshi wangeniua. Anayetaka kurudisha JKT ni mpuuzi tu maana hii nchi inamatatizo ya kutosha na wala haiitaji matatizo mapya muda huu. Big up dada. Heshima tele kwako kwa kuwa muwazi.

Anonymous said...

Mmh pole, inauma wewe acha tu watu hawajui inavokua wanazani ni masihara

Chemi Che-Mponda said...

Mdau wa 1:52PM, kijiji cha Mbola naikumbuka. Unadhani ni hao to waliokuwa wanakwenda huko! Duh, wengine walikuwa wanafanya porini! Yule accountant wa kikosi alikuwa na mchezo huo wa kuwafanya wasichana kwenye kilekichaka nyuma ya Officer's Mess!

Halafu mimi nilisulubiwa vibaya baada ya kumsema dada fulani aliyekuwa antembea na yule Deputy CO Mzanzibari! Mrefuuu, unamkumbuka? Nililamika kwa sababu tulikuwa tunapewa miraba yake tulime wakati yule binti anapelelekwa kushugulikwa na afande. Afanda kusikia hivyo wacha anipe adhabu ya kulima miraba kama kumi pekee yangu! Nilishinda shambani siku nzima ya jumapili peke yangu! Na kama unakumbuka miraba ya Masange ilikuwa mirefu kweli!

Ningenyamaza na kujidai sikuona kitu nisingepewa adhabu! Huyo afande aliniita na kuniuliza kama ni kweli nililamika kuhusu huyo binti! Wala sikukataa nilimwambia NDIYO! Yaani kwa mdomo nilikuwa out of place maana nilikuwa nawasema watu!

Anonymous said...

Yaani nimesoma maneno ya watu hapa mpaka nimelia machozi. Mimi nilishuhudia dada zangu wakinyanyaswa na maafande lakini nilishindwa kusema kitu kwa kuhofu Extra Drill. Naona haya, lakini ndo woga niliyokuwa nayo wakati ule. Kwa waliopita JKT wanajua kuna maneno ya Kuruta haina maana! You are nothing hivyo they can do anything to you! Umwambie matron, umwambie afande hawatakutetea hata kidogo! Afande mwenye anamwogopa ule afande juu yake!

Kama JKT itarudishwa basi kuwe na sehemu ambao vijana wataweza kupeleka malalamiko yao bila hofu.

Anonymous said...

dada Chem, tukirudi nyuma dada ni kwamba na wewe ilibweteka sana kusema ukweli.Ulikuwa unajua hakika jinsi maafande hao wanavyokula mbuzi pale jeshini,halafu wewe mtu anakukaribisha hadi chumbani unaenda,unapewa soda na biskuti unakula kwa kwenda mbele,hahahahaaa ulidhani wewe ni mwanaume mwenye maziwa tu au?Lazima pale ungejua kuna kulipa dada?

Kwanza zile dalili za mwanzo ulizoelezea kuwa jamaa alianza kukutomasatosamasa zilitosha kabisa kukuondoa maeneo yale, lakini ukazidi kugiribiwa kuendelea na soda na biskuti dada,bila kujijua na kujibaini uko mikononi mwa kinywa cha simba ukakaa hapo zaidi?mmmmhhhhhh hapo sijui ulikuwa unagoja nini dada Chem?

Dada Chem, tangu lini mbuzi ajitupe mikononi mwa simba halafu atoke salama bila majeruhi.La sivyo iwe huyo simba katoka kula kashiba hapo atakusitiri bila hiana.

Lakini tu nisema kisa chako kimeleta changamoto nzuri hapa ili watu wafumbuke macho kwa mengi yanayowatokea wadada mahali pengi hasa maofisini, vyuoni, mashuleni na sehemu yoyote ya kazi.Mimi mwenyewe nimeshuhudia manyanyaso ya wadada sehemu nyingi nilizofanya kazi, na vyuoni utakuta kuna wadada wasiojiweza kimasomo na ni wazuri basi Maprofesa wanachukua loophole hizo kuwatandika na mihogo yao halafu wanawaongezea vialama kwenye mitihani.

Hata wanafunzi kwa wanafunzi ni hivyohivyo wadada wanaopenda kudesa wanaliwa kishenzi kwa kuandikiwa materm paper. Kwa hiyo changamoto hii umeleta hapa kuwamulika kina dada ili waweze kujichunga na kujithamini zaidi kuliko kuuza utu wao kwa vitu kama hivyo.
Mwisho dada Chem,ulikuwa ngangali sana ukamshinda jamaa ndani ya chumba,licha ya kuwa hadi chupi ilivuliwa tena ilichanwa,na jamaa likuwa na mbinu za kijeshi zote.Mmmmhh hapo ilikuwa noma,inaelekea lijamaa lilikojoa mapema kutokana na kuhemka muda mrefu likisaka namna ya kukutrape. Na lilipokupanua miguu likawa tayari sasa halina nguvu maana mhogo ukiishatema basi gemu kwisha,hahahahaaaaa pole sana dada yangu.Nimekuaminia!!

Anonymous said...

Tatizo la wasichana na sasa wavulana kunnyanyaswa kijinsia nikutokubali hali halisi na kutaka wasivyoviweza Nimeshuhudia ayo nikiwa JKT 1977 kuna wasichana waliokuwa wakakamavu na ambao walijrahisi Hali ni hiyo pia vyuoni sasa Cha maana ni kugangamala tu gumegume. ndoano uliokula illiwaponza wengi wakiwa naive au kwa kutaka Pole

Anonymous said...

Mmmmmhhhhhhhh kisa chako kimenichekesha kwa kweli.Lakini wewe kweli ulikuwa mgumu sana pamoja na ukame wote wa jeshini muda mrefu ukawa ngangari kiasi hicho CHem? Angalau unemuonjesha tu jamaa basi yaishe,hahahahahaaaaa

Mmmmh funzo kubwa sana kwa akina dada jamani kwani mnanyanyaswa sana mahali pengi.nanyi mnajitia udhaifu hata wakati mna ujasiri wote.Fumbukeni jamani mtawapa wangapi kama hali ndiyo hiyo?

Esie Mae said...

Nyie mnaomlaumu Chemi kuwa alijipeleka mwenyewe mnasahau kuwa huyo afande alitengeneza mazingira ya kujiaminisha kwake kabla hajaamua kumtenda. Na ndivyo ilivyo hata watoto wetu majumbani wako hatarini kubakwa na watu wanaowatrust na sio strangers.

Tena umenikumbusha kisa changu, mimi huyo afande alikuwa rafiki ya kaka yangu, na akisoma hapa atajijua manina zake. Kipindi hicho mwaka 1989 nilipangiwa kwenda kambi ya Mgambo Tanga, basi kaka yangu akasema huko ni mbali na pagumu sana utateseka na haitakuwa rahisi kukuona. Alinionea huruma kutokana na matatizo yangu ya kiafya tangu utotoni. Basi akanikokota asubuhi moja hao mpaka makao makuu ya jkt pale Mlalakuwa, akamtafuta huyo rafiki yake akampata lakini hakutusaidia lolote ikabidi niende tu huko Mgambo karibu na Kabuku.

Huyo afande alikuwa Kapteni kipindi hicho, basi akaja kikazi huko Mgambo, nikasikia ninaitwa officers mess, nikaenda, akanambia nina mzigo wako kutoka kwa kaka yako twende ukachukue na kwa kuwa ni rafiki ya kaka yangu wala sikumtilia mashaka. Tutakota hapo mess kwenda rest house na ni mbali unapita mashamba na vichaka ingawa ni ndani ya kambi. Njiani si jamaa akanigeuzia kibao, akaanza kuniongoza na kunambia maneno ya kipuuzi. Nikasema mungu niokoe tuko wawili tu si atanibaka huy? Basi bahati akatokea kuruta kama mimi nikaona ndio hapa hapa nikamwambia mie narudi zangu kombania huo mzigo nitakuja uchukua kesho. Sikurudi na wala sikumuona tena nahisi kesho yake ndio aliondoka.

Sasa huyo fedhuli baradhuli aliponikosa Mgambo JKT akataka kunibaka Mlimani kwenye chumba chake. Yaani dunia ni ya ajabu hii wakati mimi naanza Mlimani mwaka wa kwanza na yeye akaja kuanza kusoma degree yake ya kwanza vile vile. Sasa kuna wakati tukawa tunashea darasa anakuja kusoma kozi kwenye department yetu. Tunaazimana vitabu, madesa (hii nayo ina kisa chake cha wanaume wa Mlimani kutumia madesa kutaka kulala na wasichana). Basi siku moja akaazima docs zangum kila nikimwambia nirudishie anatoa jibu la ntakupa kesho kesho. Sasa siku hiyo akasema nimeyasahau chumbani kwangu tukitoka darasani twende nikakupe. Tukaenda, mpaka chumbani kwake, jamaa akataka kufunga mlango anibake. Uzuri wakati tunaenda mie nikapitia floor nyingine jengo hilo hilo nikamwambia boyfriend wangu wakati huo (mume wangu sasa hivi) kuwa nakwenda chumba cha fulani kuchukua docs zangu nikitoka huko ninakuja huku. Basi jamaa akaanza tena ujinga wake loo nikamwambia ukirogwa kufunga mlango tu nitapiga kelele watu wajae! Ikabidi aniachie niende zangu.

Esie Mae said...

Lakini huko JKT jamani wasichana waliteseka sana, wengine walitoka na ulemavu wa kudumu. Mimi nakumbuka kuwa tulipofika tu Matron wa kambi alituita wasichana wote akatwambia kuwa tusikubali hata kama wakitutisha namna gani kwani sheria zinatulinda. Lakini pamoja na kulindwa kote na sheria za mdomoni mimi nakumbuka niliteseka sana kisa ni msichana sitaki kulala na afande. Na sio mimi tu maana niliwatesa hata wenzangu niliokuwa nao kombania moja, kisa nimekataa kulala na afande. Kila siku push up mpaka magoti yanachunika, kila siku kuviziana na kutafutiana makosa na hao wavulana waliokuwa marafiki zangu wa kawaida walipata adha na tabu kubwa lakini kila siku walikuwa wananiambia sisi tunapata tabu na shuruba kwa ajili yako ni bora uendelee na msimamo wako huo huo na tuko tayari kuteseka. Tunaadhibiwa kombania nzima kisha platuni nyingine wanachujwa, mpaka inabaki platuni yetu, na hapo anahakikisha mpaka inabaki section yetu ndio anatusulubu tani yake.

Kwa kweli nawashukuru sana marafiki zangu ambao nilikuwa nao section moja Mungu awabariki huko waliko maana sijui wako wapi hivi sasa nitaweka jina langu walokuwa wakiniita huko.

Na hata nilipokimbia porini huko Mgambo na kupelekwa Mgulani kujiunga na jeshi kuwa afsa kadet bado tabu hazikuniisha, nakumbumbuka kupangwa guard usiku tena geti lile la kubwa la kuingilia Mgulani karibu kila siku mpaka watu wakajua kuna kitu tu, lakini nililinda guard wee, mpaka nikamaliza jeshi!

Na kama sio guard basi Afande Kitomari atupeleke Quatter Guard karibu kila siku kula extra drill mpaka wale MP wakawa rafiki zetu tukifika wanatupa mifagio tunafagia kisha wanatwambia jimwagieni maji, kisha mkimbie na lile vumbi la kufagia na maji tukirudi jamaa anaona katukomesha. Huyu Kitomari alikuwa na ugonjwa na wasichana wadogo wadogo.

Nikimbuka tabu za huko, kujificha maporini, kufanyishwa kazi kama punda, kukimbia marathoni kila siku, kufyatua matofali, kubeba zege, kulima, kukata kuni, nakubali kuwa mengi yalinijenga na unyanyasaji wao ulinifanya niwe mgumu zaidi na mjeuri, mpaka siku moja nikamwagiwa maji usoni kisa ninaringa. Hiyo siku ndio niliamua kuwa sasa basi nitakwenda Monduli nirudi na nyota yangu niwakomeshe, lakini sikwenda badala yake nikaenda zangu Mlimani. Aagh sitaki kabisa binti yangu aende jeshini.

Anonymous said...

JKT irudishwe lakini iwe kwa wavulana peke yao. Wasichana wasipelekwe JKT.

Chemi Che-Mponda said...

Asante Esie Mae kwa kushare habari zako! Wanawake wengi wana stori za kubakwa jeshini. Yaani, waseme iwe siku ambayo wanawake watakuwa huru kutoa habari zao bila hofu Bungeni, utaona msururu wa wanawake wakijazanza huko! Story za mimba za maafande acha tu! Story za kuwa mboga ya viongozi na maafande!

Anonymous said...

Pole sana Dada Chemi kwa manyanyaso na hongera sana tena sana kwa ujasiri wa kuweza kusema.

Naomba kuwaliza nyie watu mnaomsema Dada Chemi kajitakia, mnafikiri hichi kitu kimetokea jana??? ingekuwa jana wala hata asingeingia kula soda na biskuti, lkn alikuwa mdogo...with no experience!! Kuna mambo mangapi ambayo ilipokuwa mdogo uliyafanya kwa kutokuwa na uelewa!! Acheni kuwa judgemetals!!!! Mmenikera kuliko hata huyo askari aliyebaka (Sorry dada Chemi, lkn mimi hawa wanaosema umejitakia ndio wameniudhi zaidi!!)

Anonymous said...

Mdau wa 1:52AM ni kweli kuna ile naivety ya kutokujua wala kufikiria ninia inaweza kutokea. Wasichana wengi wadogo wanajikutua kwenye situations za ajabu na hawajui wafanye nini.

Chambi Chachage said...

http://udadisi.blogspot.com/2012/07/na-haya-ya-jkt-tutayarudisha-pia.html