Tuesday, August 09, 2011

WaTanzania Wanaoishi USA Waandaa Maandamano kumpinga “Baba Ridhiwani”!

Kweli hali inazidi kuwa ngumu Tanzania miaka 50 baada ya Uhuru. Lakini Je, Rais Kikwete peke yake ni wakulaumiwa? Hebu watizime ile 50 year plan ya Mwalimu. Haikutekelezwa!

Vijana wa siku hizi hawakulelewa kama sisi. Tulikuwa hatuna TV, wala internet. Unasikiliza redio na ukipata BBC, VOA, Deutshe Welle, unaona mali! Enzi za Mwalimu ilikuwa ukisema kitu kibaya dhidi yake au kutaka kupinga, unapigwa, unatiwa ndani! Mbu walikuwa tele! Lakini tulikuwa na amani. Hali Tanzania inatisha sasa. Vijana hawajui yaliyopita na tulitoka wapi. Lakini hata mimi naona wananchi wa chini wamesahaulika. Ujamaa ulikufa na Ubepari umerudi kwa nguvu. UTabaka unazidi Tanzania na ndo chanzo cha chuki.

Sasa kuna habari ya kupinga Ziara ya Rais Kikwete kuja Marekani. Itasaidia kuboresha hali ya wananchi Tanzania?

**********************************************************

Kutoka:
http://mgonjahjr.blogspot.com/2011/08/tanzania-yaelekea-kusiko-shwari.html

TANZANIA YAELEKEA KUSIKO SHWARI

Wa Tanzania wanaoishi USA waandaa maandamano kumpinga “Baba Ridhiwani”, Hii ni sehemu ya maandalizi hayo kama yalivyoandikwa na ELIAKIM MALLYA.
Kutokana na kuchoka na hali ngumu inayoendelea hapa Tanzania, ndugu zatu wanaoishi USA wameandaa maandamano ambayo yatakuwa ya amani kupinga utawala mbovu wa “Baba Ridhiwani” hasa baada ya kushindwa kuwachukulia hatua masfidi hapa nchi.

Tunaandaa maandamano ya amani jijini Washington DC Rais Kikwete “Baba Ridhiwani” atakapowasili kwenye kikao cha DICOTA 2011. Tayari watu 150 wamekubali kushiriki kwenye maandamano hayo. Tunataka watu wengi zaidi kujitokeza. Hii ni kumshinikiza huyu fisadi papa na mzururaji kushugulikia matatizo yanayowakabili wananchi wa kawaida. Maandamano yetu yatahitimishwa na kupokelewa na viongozikutoka United States Department. Tayari tumetuma maombi kupinga misaada marekani inayopa Tanzania, kwani hayasaidii Jamii bali Kikwete na genge lake la majambazi

Wote mnakaribishwa karibishwa. Maandamano ya Amani yanaruhusiwa marekani ilimradi mtu hajavunja sheria nchini. Ukiwa na makaratasi yako, njoo tulikomboe taifa letu. Ukombozi wa TANZANIA upo mikononi mwetu. Mabango yanachapishwa tarehe 24, Tunaomba mawazo tofauti kuhusu ujumbe tutakaobeba kwenye mabango yetu. Tumechoka na Kikwete, dawa nikuanza maandamano. Tupo tayari kufa sasa. Tunisia iliokolewa na watu tu kama sisi, tukifa bahati mbaya vizazi vijavyo vitafaidi. Tafadhali sambaza ujumbe. Tutatoa tamko rasmi ya maandalizi tarehe 20 mwenzi huu Ukitaka kushiriki tuma barua pepe EliakimMallya@yahoo.com

Raia wa kawaida anayo haki ya kumfanya Kikwete Anyimwe VISA. Kwa Kupinga Ujio wa Kikwete, au yeye kunyimwa VISA tumeni emails nyingi iwezekanavyo kwenda East African Affairs Bureau. Email Adress wiegertjr@state.gov

UPDATE
Habari njema ni kwamba, kuna familia moja ya kitajiri ambayo ina interest kubwa Tanzania na wanashngaa kuona taifa letu linavyodidimia. Kwa maana hiyo, wamejitolea kulipia mabango, pamoja na mabasi sita.

1. Basi 2 yataanzia NY (Ni ya watu wa Boston, NY, Long-Island, etc...)
2. Yanayotokea Ohio (Ohio, Maryland, Pensylvania, Michigan etc..)
3. MaBasi ya mwisho yatatokea Atlanta Georgia (Texas, Virginia, Florida, Alabama,Kansas, etc..)

Kwa hiyo kaeni mkao wa Kula, mwisho wa mwezi huu, tunawapa ratiba kamili ya maandamano, yatakayoanzia sehemu ambayo tutawapa kuendelea kwenye Ukumbo wa DICOTA, Ubalozini na hatimaye kumalizika kwnye hoteli atakayofikia FISADI Kikwete. Tutakesha hotelini, chakula kitakuwepo na huduma zote muhimu pia zitakuwepo. Tuko pamoja hadi kieleweki. Wanaotaka kushiriki tumeni barua pepe, kwenda
eliakimmallya@yahoo.com. Mimi ni mwana CCM toka UVCCM lakini naapa ya Kwamba nimechoka na JK. Tunamsubiri Marekani, hata kama ni miaka miwili tunamsubiri, wadhamani wapo

13 comments:

Anonymous said...

sisi watanzania tunaenda wapi mwambie huyu eliakim aje Moshi ashukulikie masuala ya kijiji,wilaya,mkoa kwanza ndipo aje kitahifa yeye taharifa bila kukihakiki anakurupuka na mbona Mpaka mlikuwa amsemi kitu kuwapa uhuru wa kujua mambo ndiyo tabu
uwezi saidia nchi yako ukiwa nje unapokea taharifa tu kama mzungu badala uje uone hali halisi nyooo.

Anonymous said...

Anoni usiwadanganye wenzako unataka waje Bongo waandamane si watapigwa na virungu, mabomu ya machozi .maji ya kuwasha wewe unakuwa kama hujui mambo yaBongo bwana Majeshi yote kuanzia Polisi, JWTZ na kadhalika yote ni CCMna kama unbisha angalia viongozi wote kuanzia wa Pilisi mpaka wa JWTZ wakistaafu wanapewa posti ya Ubalozi au Ukuu wa mkoa. Mimi naona ni sawa tu andamaneni huko huko US mkija huku hao FFUwakirusha mabomu hayamchagui mtu yatawazuru hata watoto wetu wanao enda shule. Wanaoruhusiwa kuandamana hapa kwetu ni CCM tu.

Anonymous said...

Hii mijitu mioga kama hilo anon. la kwanza ndio inayotufanya tuwe masikini kila kukicha. Babu zetu wangekuwa waoga kama wewe mpaka leo hii ungekuwa unalima mashamba ya wakoloni, mbulukenge we!

Anonymous said...

anoni wa tatu umesema kweli kwa kuongezea tu siyo lazima waje nyumbani hata wakidai haki nje bado watasikika kwani wakija hapa nyumbani watapigwa virungu kabla hawajasema wanataka nini. Hata Samora alidai Uhuru akiwa Tanzania na aliupata Big up Wabongo mlioko US tuwakilisheni hapa hatuwezi kupata nafasi ya kusema kitu!

Anonymous said...

Hiyo hela ya kumlipia Rais safari ya Marekani ingekotosha kutibu wagonjwa wote Muhimbili kwa miezi mitatu! Fikiria Rais na entourage wanasafiri First Class, hoteli First Class. Chakula na vingeneo, hela ya shopping! Mwalimu hakusafiri kama huyo jamaa Kikwete anavyosafiri! DAH!

Anonymous said...

Rais Kikwete afikisha safari 313 nje ya TANZANIA!
Hebu fikiri ikiwa kila safari kwa uchache imetumia mil 15x313=4,695,000,000/- !

Anonymous said...

SAFARI za Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi, tangu alipoingia madarakani, zimeligharimu taifa mabilioni ya shilingi, MwanaHALISI limebaini.
Uchunguzi umeonyesha kuwa katika kipindi cha miaka minne tangu awe rais, Kikwete amekaa nje ya nchi kwa takribani siku 120, sawa na miezi minne.
Hadi mwishoni mwa mwaka jana, kiasi cha Sh. 2.4 bilioni zilikuwa zimetumika kwa ajili ya posho na gharama za malazi kwa rais na ujumbe wake nchi za nje.
Mara nyingi, ujumbe wa rais huhusisha mkewe, walinzi, waziri kutoka wizara inayohusika na safari, waziri wa mambo ya nje, pamoja na wasaidizi binafsi wa rais na wale wa mke wake.
Kwa mujibu wa uzoefu wa safari, ujumbe wa rais anaposafiri nje ya nchi huwa na kati ya wajumbe 15 na 22.
Kwa viwango vya serikali, watu wanaosafiri kwenye msafara wa rais hulipwa kiasi cha kati ya dola 350 na 500 (Sh. 600,000 kwa siku).
Hata hivyo, MwanaHALISI limeambiwa kuwa rais hutakiwa kulala katika hoteli yenye hadhi ya aina yake – ambayo gharama yake huwa kati ya dola 800 na 1,200.
Kwa kuimarisha ulinzi na kukabiliana na upweke, hoteli anakolala rais hulaza pia walau watu wanne, gazeti limeelezwa.
Hawa wanaweza kuwa walinzi wa rais, daktari na wasaidizi wake wa karibu ambao anaweza kuwahitaji wakati wowote.
Kwa hiyo, kwa msafara wa watu 20 ambayo ni idadi ya kawaida kwa msafara wa rais, hasa anapokwenda nje ya nchi, wastani wa matumizi kwa siku inaweza kufikia kiasi cha dola 15,000 (Sh. milioni 20).
Kwa safari kama ya Mei 12 hadi Mei 26 mwaka 2006, wakati Rais Kikwete alipokuwa nje ya nchi kwa karibu wiki mbili, kiasi cha Sh. 273 milioni kilitumika kwa ajili ya safari hiyo pekee.
Katika safari yake hiyo, Rais Kikwete alitembelea Uganda, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Ufaransa na Marekani.
Katika mahojiano mbalimbali ambayo MwanaHALISI limefanya na wafanyakazi wa ikulu pamoja na wizara ya mambo ya nje, gazeti limeambiwa kwamba kiasi hicho (Sh milioni 273) “si kikubwa sana” kwa viwango vya matumizi wakati wa ziara za wakubwa nje ya nchi.
Kwa safari hiyo pekee, Kikwete alitumia fedha nyingi kuliko kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya safari zake zote za nje ya nchi kwa mwaka huu wa fedha (2009/2010).
Kwa mujibu wa bajeti ya mwaka huu, rais ametengewa Sh. 115 milioni kwa safari za nje; takwimu ambazo zimeleta utata ikilinganishwa na matumizi kwa safari za ughaibuni.
Kwa mfano, bajeti ya safari za nje, kwa mujibu wa bajeti ya 2009/2010, imekuwa ndogo kiasi kwamba kwa uzoefu, fedha zote zinaweza kutumika kwa safari moja tu.
INAENDELEA

Anonymous said...

Aidha, bajeti ya ikulu ya safari za ndani ya nchi nayo imeongezeka kutoka Sh. 608,419,000 kwa bajeti ya mwaka 2008/2009 hadi Sh. 723,360,000 kwa mwaka 2009/2010, ikiwa ni ongezeko la Sh. milioni 114.9.
Kwa takwimu hizi, matumizi ya safari za ndani za ikulu (rais) yanaonekana kuwa makubwa kuliko yale ya nje, jambo ambalo wazoefu wa safari za ikulu wameeleza kuwa siyo sahihi.
Miongoni mwa mambo ambayo Rais Kikwete amekuwa akilalamikiwa na wanasiasa, wanaharakati na wananchi kwa jumla, ni wingi wa safari zake za nje ambazo zinaelezwa kuwa zinachota fedha nyingi kwa manufaa haba.
Rais alifanya safari nyingi mwaka 2006 hadi kulalamikiwa na wananchi. Miongoni mwa safari za mwaka huo pekee ni kama ifuatavyo:
•Tarehe 19-25 Januari alikuwa Khartoum, Sudan kuhudhuria mkutano wa nchi za Afrika (AU)
•23 Machi alifanya ziara ya siku moja ya kiserikali kujitambulisha Kigali, Rwanda.
•Tarehe 22 Machi rais alikwenda Kampala, Uganda kwa ziara ya siku moja ya kujitambulisha
•24 Machi alikwenda Nairobi, Kenya
•19-20 Aprili alikuwa Lesotho na Swaziland.
•Tarehe 21-22 Aprili rais alikuwa ziarani Maputo, Msumbiji;
•28 Aprili alikuwa Harare na Bulawayo, nchini Zimbabwe
•6 Aprili alikuwa Gaborone, Botswana.
•Rais alikuwa ziarani Namibia 10-12 Aprili;
•Tarehe 7-9 Mei alikuwa Pretoria, Afrika Kusini.
•Tarehe 12 Mei rais alianza ziara ya wiki mbili katika nchi za Uganda (13 Mei), Arabuni (15 Mei), Ufaransa (16-19 Mei) na Marekani (21-26 Mei).
•Tarehe 31 Mei hadi 3 Juni rais alihudhuria Jukwaa la Kiuchumi la Dunia mjini Cape Town, Afrika Kusini
•Tarehe 4 Julai alihudhuria mkutano wa AU, Banjul nchini Gambia.
•Julai 10-12 rais alikuwa Cape Town, Afrika Kusini kuhudhuria mkutano wa viongozi wa serikali ulioandaliwa na kampuni ya Microsoft ya Marekani
•20 Julai alihudhuria mkutano wa Leon Sullivan, Abuja nchini Nigeria.
•Rais alikuwa Berlin 21 na 22 Julai kwa ajili ya kuchunguza afya yake;
•Alihudhuria mkutano wa SADC, Maseru nchini Lesotho kati ya 19 na 20 Agosti
•Tarehe 21-22 mwezi huo alikuwa ziarani Angola.
•Rais Jakaya Kikwete alikuwa Cuba tarehe 12 Septemba kwa maandalizi ya kikao cha Nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM);
•15 Septemba alikwenda Madrid, Hispania kwenye Uwanja wa Mpira wa uwanja wa Santiago Bernabeau unaotumiwa na klabu mashuhuri ya Real Madrid.
•Septemba 15 hadi18, rais alikuwa Havana, Cuba kwa mkutano wa NAM
•Kati ya 19 na 25 Septemba, rais alikuwa kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, New York.

INAENDELEA

Anonymous said...

MwanaHALISI lina taarifa kuwa tayari matumizi ya serikali kwa jumla mwaka huu wa fedha yamezidi kiwango kilichoombwa wakati wa kikao cha Bunge la bajeti mwaka jana.
Enzi za utawala wa Rais Benjamin Mkapa, kuna wakati ilidaiwa kwamba Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, alitumia kiasi cha Sh. 500 milioni kwa safari moja tu nchini Marekani.
Pia mwaka 1990, msafara wa Tanzania ulioongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kwenye mkutano wa Dunia wa Mazingira uliofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil, ulinusurika kuzuiwa kuondoka baada ya kumaliza fedha zote zilizotolewa.
Miongoni mwa maofisa wa ngazi za juu wa wizara ya mambo ya nje waliozungumza na gazeti hili wiki iliyopita, wakati wa safari yoyote ya rais nje ya nchi, sharti msafara uwe na angalau dola 50,000 hadi 100,000 (kati ya Sh. 70 na 140 milioni).
“Unajua haya mambo wakati mwingine yanategemea na kiongozi wa nchi uliye naye. Kama unasafiri na Nyerere siyo sawa na kama unasafiri na Mobutu. Kama kiongozi ni mfujaji mtatumia fedha nyingi na kama kiongozi si mfujaji basi mtatumia fedha kidogo.
“Cha msingi ni kwa mkuu wa msafara kutoa taarifa serikalini kuhusu matumizi. Si kwamba kama utapewa dola 50,000 basi ni lazima uzitumie zote hadi ziishe. Lakini kama kiongozi anajua kutumia, hela zitaisha tu. Si mradi zitolewe maelezo tu,” alisema.
Uchunguzi umebaini kuwa tangu awe rais, Kikwete ameonekana kupendelea sana kwenda nchini Marekani na Uingereza.
Hadi mwanzoni mwa mwaka huu, Kikwete ametembelea Marekani mara nane na Uingereza zaidi ya mara nne; mara nyingine akipitia tu kutoka katika nchi nyingine.
Tathmini ya MwanaHALISI imeonyesha kwamba kwa wastani, ziara za Kikwete katika nchi za Afrika huchukua wastani wa siku mbili wakati Ulaya huchukua wastani wa siku tatu hadi nne.
Pia, Kikwete alifanya safari nyingi zaidi ughaibuni mwaka 2006 kwa lengo la kujitambulisha kwa nchi mbalimbali na mwaka 2008 alipokuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).
MwanaHALISI limefanikiwa kukusanya orodha ya safari zote ambazo Kikwete amefanya tangu alipoingia madarakani hadi mwanzoni mwa mwaka huu.
Gazeti toleo na. 188

MWISHO

Anonymous said...

No nation has the right to make decisions for another nation; no
people for another people. "Julius Kambarage Nyerere, from his A
Peaceful New Year speech given in Tanzania on 1 January 1968.

Nimesoma kwa masikitiko makubwa sana juhudi za Kundi la Wanaojiita watanzania wa nchini Marekani kufanya maandamano ya Amani kupinga Ziara ya Raisi wa Tanzania Nchini humo .


Nimejaribu kusoma Kundi hilo jina lake ni nini ? Sijapata , Kiongozi wake ni nani ? Sijaona popote badala yake nimeona watu wakijitambulisha kwa majina bandia ambayo sio yao kwa uhakika na matumizi ya Barua pepe wanazotengeneza Kila mara .

Kwa kawaida watu wanavyoitisha maandamano kwanza wanakuwa na Agenda zao baada ya kujipanga na kufanya majadiliano kadhaa pia wanakuwa wameomba ruhusa za maandamano hayo ili kuweza kupata ulinzi na miongozo mengine kwa ajili ya maandamano hayo na mwisho wa siku wanakuwa na viongozi wao .

Kutokuwa na viongozi pamoja na agenda na masuala mengine muhimu kwenye maandamano madhara yake yanakuwa kama nchi ya Misri inavyozidi kuangamia sasa hivi kwa kukosa viongozi baada ya maandamano ya kuondoa utawala Fulani madarakani sasa hivi nchini humo kila mtu hamwamini mwenzake na hata maandambano hayajulikani viongozi wake haswa ili waweze kuweka jamii na nchi yao sawa .

Utashangaa na kuona aibu ni maandamano gani yasiyokuwa na viongozi tena yanayofanyika katika nchi za watu na watu ambao hawajafika Tanzania kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita na hawajui shida zozote zinazoikabili nchi kwa sasa hivi kwa vitendo zaidi ya kusoma kwenye mitandao bila kuchukuwa hatua yoyote .

Hawa ni watu waliosomeshwa kwa kodi zetu wenyewe wakaamua kuasi na kubaki huko na sasa wanaanza kutumiwa na nchi hizo kama vibaraka kwa kificha nyuso zao , majina yao na hata kujitenga na jamii nyingine za watanzania zilizoko Ulaya na Marekani kwa sababu hata vyama na jamii hizo hazitambui wito wa maandamano hayo wala wale walioyaandaa .

Tunawataka watu hao warudi nchini , waje kujenga nchi na sasa hivi kuna fursa nyingi sana kwa sababu ya jumuiya ya afrika mashariki , Comesa , Sadc na nyingine nyingi ambazo nchi yetu imejiunga nazo .


Hizi ni Fursa ambazo waandamanaji hawajawahi kuzihoji wala kuzitumia badala yake ni kupanga maandamano ya kumdhalilisha kiongozi wa nchi pamoja na kuziba fursa nyingine kwa wale wanaotaka kujua zaidi kuhusu Tanzania haswa wageni na wawekezaji .

Ni matumaini yangu watu hao wanaojiita watanzania watabadilisha mawazo na muelekeo wao na kuacha kutumia jina la watanzania waishio marekani kwa malengo ya kuharibu jina la nchi na viongozi wake bila kujali itikadi ya vyama vyao , makabila wala dini zao .


Wengine tunaopata fursa za kutoa maoni yetu kwenye mijadala kama mimi hapa , tutumie fursa hizi vizuri na kwa uhuru katika kuelimisha watu bila kuchoka na bila kuogopa vitisho vyovyote toka kwenye makundi ya watu wowote .

"...intellectuals have a special contribution to make to the development of our nation, and to Africa. And I am askin understanding that they should possess, should be used for the benefit of the society of which we are all members."Julius Kambarage Nyerere, from his book Uhuru na Maendeleo (Freedom and Development), 1973

Anonymous said...

anoni wa 13/5/2011 Nafikiri waache waandamane kwani wewe unasema hawajarudi nyumgani miaka 10 iliyopita siyo kweli,napia walipelekwa kusoma kwa kodi zetu hiyo pia siyo kweli Tazania iliacha kusomesha watu nje zaidi ya miaka 20 iliyopita ispokuwa tu kwa watoto wa wakubwa au watoto wa watu waliokuwa kwenye system. Wengi waishio nje aidha wamepelekwa nataasisi zisizo za kiserikali,Greencard,au wengine kwa ukali wa maisha ya nyumbani wamejipeleka wenyewe na wanajua wametumia uongo gani ambao umewafanya wapate makaratasi ya kuishi.Hao watoto wa watu waliokuwa kwenye system wakienda huko lazima watarudi kwa kuwa wanakuwa wamekwisha andaliwa kazi. Halafu naomba usiwadanganye warudi watakuja kufanya nini hata kama wamesoma kazi zipo kwa kujuana kama huna God father utasota na kiji degree chako hupati hata kazi ya kufagia choo.Kwanza anzeni kuwapa wasomi wanaosota waliopo nyubani halafu ndiyo muwaambie walioko Marekeni warudi.

denyol said...

dada chemi na wadau wengine, sie vijana wa karibuni sio kwa sababu ya upya wetu ndio tunaongea sana kuhusu habari za hii nchi, ila utofauti wa sasa na enzi zenu za mwalimu, kipindi kile kweli mbu walikuwa wengi na amani ikawepo kwa vile hapakuwepo habai kama za hivi karibui za watu kujilimbikizia mapesa mengi, miradi ya serikali inafanyiwa ubadhirifu mchana kweupe, kazi halali hazilipi kama za haramu zinavyolipa na n.k, n.k... Ingekuwa wote tumejifunga mkana kama enzi zenu wala kelele hizi usingezisika, ila sasa hali ni mbaya sana kwa kweli, na wasiposikia mapema, hali itatumbuka, halafu tuanze upya! insha-allah tutashinda mapamabano haya.

Anonymous said...

Hali ya wananchi wa kawaida siyo nzuri, lakini viongozi wa serikali hili haliwasumbui kabisa, kwani maisha wanayoishi utafikili kwamba watu wanaowahudumia hawana matatizo ya aina yoyote ile. Haya mambo mwisho wake utakuwa siyo mzuri, kwa kuwa wananchi watachoka. Wanaoitetea serikali ni wale wachache wanaofaidika nayo.