Monday, October 31, 2011

Kumbukumbu - Bernadette Wawuda Msafiri

KUMBUKUMBU


Marehemu Bernadette Wawuda Msafiri (pichani)

October 24, 1943 – November 1, 2010

Hatukujua asubuhi ile Mungu angekuita.Katika maisha tulikupenda na katika kifo hivyo hivyo. Tulivunjika moyo kukupoteza, hukwenda peke yako bali sehemu yetu ilikwenda pamoja nawe siku ile Mungu alipokuita nyumbani. Umetuachia kumbukumbu nzuri, upendo wako ni muongozo wetu. Japo hatukuoni wakati wote uko pamoja nasi. Kiungo katika familia yetu kimevunjika, maisha yetu hayako sawa tena. Lakini kadri Mungu atakavyotuita mmoja mmoja viungo vitaungana tena.

Unakumbukwa na Mume wako, watoto, wajukuu, jamaa na marafiki.

Kutakuwa na Misa ya Kumbukumbu siku ya Jumatano tarehe 2 Novemba 2011 saa 11 jioni katika makaburi ya KONDO ( Tegeta ), Dar es salaam

Nyote mnaalikwa.

No comments: