Saturday, October 08, 2011

Futeni Tuition!

Hii imeandikwa na Mdau SK. Hata mimi naona siku hizi tuition imeua maana ya kusoma shule ya msingi, sekondari za serikali.
***************************************
Tuition Imeua Vipaji Vya Wanafunzi
Jamani kama kuna shimo la kufukia vipaji, na uwezo wa kufikiri kwa wanafunzi wetu ni TUITION. Sijui wazo hili lilitoka kwa nani. Tution ilizaliwa miaka ya 1990s na mbaya zaidi baada ya mwaka 2000. 
Tuition inafanya wanafunzi wasijiamini kabisa. Wanaona mwalimu wake darasani hawezi kumfundisha hadi aelewe na ndio maana anamtafuta mwalimu mwingine huku akijua msemo wa kiswahili usemao, wapishi wengi huharibu mchuzi.
Wanafunzi wa siku hizi hawapewi tena HOME WORK,  badala yake akitoka shule akienda nyumbani anamkuta mwalimu mwingine akimngojea. Wanafunzi wetu hawajui kujisomea wenyewe au kutumia maktaba, hata kufungua vitabu na kutafuta mada anayokusudia hawajui, maana muda mwingi wanazunguka na vipeperushi vilivyochakachuliwa na waalimu wa Tuition. Vitabu vya literature ambavyo enzi za 1980s tulivisoma vizima kama vile MINE BOY, THINGS FALL APART, THE RIVER BETWEEN, nk siku hizi wanafunzi hawavijui hata sura yake kwani wanasoma vipeperushi tu. Uwezo wa watoto wetu umewekwa kapuni.
Enzi zangu nikitoka shule nikenda nyumbani nilikabidhiwa jembe kulima ili kuchangia ada. Siku hizi wanafunzi wetu hawana nafasi ya kazi za mikono maana wamezungukwa na waalimu pande zote. Wamezoea kulishwa tu, SPOON FEEDING. Tunakwenda wapi?
Zamani tulifundishwa na kuzoeshwa kuwa ili ufaulu 60% ni juhudi ya mwanafunzi mwenyewe na 40% ni msaada wa mwalimu. Siku hizi wanafunzi wetu wamegeuzwa, wanajitegemea 20% na 80% ni kutegemea mwalimu. Wanafunzi hata wenye uwezo hawajiamini kufaulu bila dudu hili TUITION. 
Ninaomba serikali ifute mchezo huu mchafu wa TUITION kwani HUUWA VIPAJI NA UWEZO WA WANAFUNZI WETU KUFIKIRI. Serikali ilipe waalimu vizuri ili nao wafundishe vya kutosha na si ovyo ovyo kama ilivyo sasa na hatamae wanawaelekeza wanafunzi kuwa ukitaka kujua zaidi njoo jioni. Hii njoo jioni mabinti zetu hugeuzwa kuwa wake za waalimu. Mnafahamu hilo 
Mwasemaje?

2 comments:

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

Anonymous said...

Da Chemi usemayo ni kweli lakini itkuwa vigumu sana kuua tuition kwa sababu mfumo mzima wa nhi yetu umeharibika kuanzia Elimu hadi Hospitali. Kama ulivyosema enzi zetu unatoka shule na unafanya shughuli za nyumbani na pia kama sikosei hizi shule za serikali sasa hivi zinaongoza kwa divIV nazero lakini enzi zetu shule za serikali zilikuwa first class. Hii ni kwa sababu hata mwalimu alikuwa na hadhi na serikali ili weka pese nyingi kwenye budget ya Education hata Uni watu walisoma bure bila matatizo.Ukianza na shule za serikali wote tulisoma shule moja kuanzia mtoto wa rais mawaziri hadi wa mlala hoi na kama sikosei hata hali zetu ilikuwa siyo rahisi kujua kama huyu ni mtoto wa mkubwa au wa kabwela lakini sasa kuna mabadiliko makubwa sana huwezi kumuona mtoto wa kiongozi yeyote au hata mfanyabiashara ana soma Zanaki, Jangwani au Azania n.k watoto wao wote wanasoma shule kama Maian n.k kwa hiyo hawawezi kuzijali au kuwajali walimu wa shule zetu za serikali, Na walimu nao hawana cha kujisaidia kimfaacho mtu ni chake kwa hiyo wanatumia elimu tao kujisaidia kwani idara husika imeshindwa kuwasaidia ndiyo wakabuni tuition kama Madaktari wanavyofanya part time kwenye Private Hospilals na daktari huyohuyo ukikutana naye Muhimbili au Mwananyamala anakuwa tofauti na ukikutana naye Hindu Mandal