Friday, August 10, 2012

Misba Toronto, Canada - Ritha Kaduma

Kutoka Bongo Celebrity:

Marehemu Ritha (Fatima)  Kaduma

 Familia ya Bwana na Bibi Fredrick Kaduma wa Kimara-Dar-es-salaam,Tanzania na watanzania waishio Toronto,Canada wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wao, Ritha Kaduma (Fatima) (pichani) kilichotokea hapo jana tarehe 9th August, 2012 huko Toronto,Canada. Fatuma au Rita amefikwa na mauti katika hospitali ya St.Michael’s ya Toronto alipokuwa amelazwa kwa muda mfupi.

 Taratibu na mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi zinafanyika nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi na kaka yake huko huko Toronto,Canada. Ukiwa kama mtanzania,ndugu,jamaa au rafiki,popote pale ulipo, unaombwa kuchangia fedha,hali na mali kwa ajili ya kuwezesha kuusafirisha mwili wa marehemu kurudi nyumbani kwa mazishi mapema kadri iwezekanavyo kwani kama wengi wenu mnavyofahamu, mwili unavyozidi kukaa Funeral-Home,gharama ndivyo zinavyozidi kuongezeka.

Mwili utasafirishwa punde tu zitakapopatikana fedha za kutosha kwa ajili ya kulipia gharama husika. Gharama zimekadiriwa kufikia kiasi cha $24,000 ambazo zinajumuisha kuutayarisha mwili,kuutunza na kuuhifadhi na pia kuusafirisha mpaka nyumbani Tanzania. Unaweza kutuma mchango wako kwenye Account maalumu ya wafiwa kama ifuatavyo:

BANK : RBC (Royal Bank of Canada) ACCOUNT NUMBER: 5122551 TRANSIT NUMBER: 06742 INSTITUTE NUMBER: 003 SWIFT CODE: L0YCCAT2

 Vilevile unaweza kutumia E-mail Money Transfer kwenye anuani pepe gilfa36@hotmail.com .

Pia unaweza kuwakilisha msaada wako kwa kutumia anuani hii: 5-7 DRIFTWOOD CRESCENT NORTH YORK,ONTARIO M3N 2R1 Kwa mawasiliano zaidi unaweza kuwasiliana na wafuatao: Kaka yake Fatuma (Issa) kwa nambari hii-647-760-1051. Flora- 647-622-6361 Emmanuel -416-835-6778. Gabriel- 416-631-7762.

Kwa upande wa nyumbani Tanzania,tafadhali wasiliana na Fred Kaduma kupitia nambari 0655-888268 kwa taarifa zaidi.

Tafadhali chukua muda kuwafariji na kuwaombea ndugu,jamaa na marafiki waliofikwa na msiba huu. Tunatanguliza shukrani kwa misaada yote iliyotolewa na itakayotolewa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. Amen.

 Read more: TANGAZO LA MSIBA TORONTO,CANADA - BongoCelebrity

No comments: