Tuesday, November 06, 2012

Uchaguzi wa Rais wa Marekani ni Leo!

Wadau, leo waMarekani wanapiga kura katika Uchaguzi wa Rais.  Wagombea ni Rais Barack Obama kutoka chama cha Democrats na  Gov. Mitt Romney kutoka Chama cha Republican. Romney ni tajiri kupindukia na wanasema atakuwa rais tajrii kulio marais wote walioongoza Marekani!


Gov. Mitt Romney

Gov. Romney alikuwa Gavana wetu hapa Massachusetts na hakuwa Gavana mzuri.  Alichotaka ni cheo tu cha Ugavana ili aweze kugomgea urais.  Hata hakugombea ugavana mara ya pili kwa vile alipata alichotaka. Pia alivyokuwa Gavana alikuwa anasafiri sana na kuwa likizo mara kwa mara. Tulikuwa tunamwita Absentee Governor, yaani gavana ambaye hayupo.  Enzi za Romney nilipoteza kazi yangu kwa vile kazi zilipelekwa India.  Sijui hiyo kazi anayosema atawaletea wananchi zitatoka wapi. Labda kazi za kuosha magari yake na kusafisha nyumba zake.  Maana huyo Romney ndiye mpenzi wa kusafirisha kazi India na nchi zingine ambako watu wanalipwa hela ndogo.  Mtaona kwenye matokeo kuwa Massachusetts inamchagua Rais Obama.

Wadau, ubagauzi bado upo mwingi hapa Marekani. Yaani kuna wazungu ambao wanampigia kura Romney kwa vile ni mzungu bila kujali ubovu wake.

Mimi binafsi ninaomba Rais Barack Obama ashinde.  Atuongoze miaka minne zaidi. Aliposhika urais tulikuwa katika hali mbaya sana ...asante uongozi mbovu wa Raisi George Bush Jr. wa miaka minane. Bush Jr. aliobomoa hii nchi hasa kwa kuanzisha vita Iraq!  Rais Obama anaijenga nchi tena. Amefanya kazi nzuri ila kwa vile ni mweusi watu hawataki kutambua mafanikio yake.  Yaania Rais Obama anatahili kuwekwa Mt. Rushmore, lakini  hawataki kwa vile ni mweusi!

Haya wadau, huenda jioni tutajua mshindi ni nani, lakini wengine wanasema huenda uchaguzi huu ukawa na mushkeri nyingi na hatatjua kwa wiki kadhaa ikibidi kura zihesabike tena.

OBAMA/BIDEN 2012!


1 comment:

Anonymous said...

Asante Chemi kwa kuwa muwazi. Racism is very much alive, well and kicking in the US, which prides itself as the leader of the so-called free world.