Wednesday, December 05, 2012

Warsha Kwa Vyombo Vya Habari London 6/12/12

WARSHA FUPI YA VYOMBO VYA HABARI KESHO ALHAMISI LONDON


Na Michael Zetulla

Jumuiya ya Urafiki kati ya UIngereza na Tanzania (Britain –Tanzania Society) itaendesha warsha juu ya vyombo vya habari Tanzania, kesho Alhamisi.

Semina hiyo itafanyika chumba namba 4421 katika chuo kikuu cha lugha SOAS (School of Oriental and African Studies) kilichoko Russell Square, katikati ya London, saa kumi na moja hadi saa moja jioni.

Mtu yeyote anaweza kuhudhuria na hakuna malipo yeyote yanayotakiwa.

Mzungumzaji mkuu atakuwa Ben Taylor wa Daraja ambalo linasimamia magazeti kadhaa mjini Njombe na Iringa ikiwemo Kwanza Jamii. Mwenyekiti wa warsha atakuwa Freddy Macha mwandishi na mwanasafu mkazi London.

Kufuatana maelezo yaliyotolea na jumuiya ya BTS, mada ya warsha itakuwa : “Habari na demokrasia Tanzania”. Shughuli hii ni sehemu ya warsha mbalimbali zilizofanywa na jumuiya ya BTS toka mwezi Oktoba kuzungumzia na kuangalia mada mbalimbali za Tanzania. Mwezi jana Waziri wa Uchukuzi , Dk Harrison Mwakyembe alialikwa kuzungumzia suala la katiba na usafiri katika ukumbi wa Central Hall, mjini London.

Habari zaidi tembelea:

http://www.btsociety.org/events-and-announcements

Au piga simu

+44-20-7727-1755
+44-7721-869-215

No comments: