Tuesday, August 26, 2014

Jamaa Aibiwa Baada ya Kutoka Benki Mlimani City

Hali inatisha.Allah atusalim salama! 


JAMANI HALI INATISHA SANA,NIPO HAPA NILIKUWA NA MTU NAFANYA NAE KAZI ANANIHADITHIA JINSI ALIVYOIBIWA PESA IJUMAA ILIYOPITA NIMEOGOPA,SIJUI TUFANYEJE TUWAPO NA PESA UUWIIIIIII.

NAHISI KABISA WAHUDUMU WA BANK AU MAMENEJA WA BANK WANASHIRIKI HUU MCHEZO,ANASEMA ALICHUKUA MKOPO NMB SH MILIONI 30!!KWA NIA YA KUMALIZIA UJENZI,SIKU YA IJUMAA KUNA KAZI ALITAKA KUFANYA NA FUNDI KUNA VIFAA WALITAKIWA WANUNUE PAMOJA NA GHARAMA ZA UFUNDI INGEFIKA KM MILION 10 HIVI,AKAENDA BANK MLIMANI CITY KUCHUKUA HIZO PESA,

AKIWA TAYARI AMESHAZICHUKUA FUNDI AKAMPIGIA SIMU KUWA AMEFIWA KWA HIYO KAZI HAITAFANYIKA KWA SIKU 3,YULE KAKA AKAONA ASIKAE NA PESA NYINGI HIVYO AKAAMUA AZIWEKE TENA MILION 7 ABAKI NA 3,NAHISI ALIVYOCHUKUA ZILE PESA AKAWA AMESHALENGESHWA,ALIPOTOKA TU BANK AKAPIGIWA SIMU NA MTU MWINGINE WALIONGEA DILI LA TILES KUWA AMRUSHIE M 1 KWENYE M PESA MAANA DILI LIKO TAYARI,AKAINGIA PALE VODA AKAWEKA PESA AKAMTUMIA AKABAKI NA M 2 AKAWEKA NA NYARAKA ZAKE FULANI MLE KWENYE BAHASHA YA FEDHA,AKATOKA,ANASEMA MUDA WOTE KUNA KIJANA ALIKUWA ANAMFATA NYUMA AKIINGIA SEHEMU YULE KIJANA ANASIMNAMA NJE KUZUGA LKN HAKUMTILIA MAANANI,AKAINGIA KWENYE GARI AKAONDOKA KUPITIA GETI LA UPANDE WA SURVEY,ILE ANAKATA KONA PALE ZINAPOPAKI BAJAJ KUNA PIKIPIKI IKAM BLOCK,AKAJA KIJANA MMOJA DIRISHANI ANA BASTOLA AKAMWAMBIA TUPE HIZO MILION 10 ZETU,USIPIGE KELELE KISHA ONDOA GARI FASTA,KWA KUKUHURUMIA HATUKUUI,TUPE HELA NA HUO MKOPO TUTAUTUMIA WOTE!!!.

YULE KAKA ANASEMA ALIBAKI MDOMO WAZI,HAWA WATU WAMEJUAJE KM NIMEKOPA??BASI ALICHOFANYA AKAWAPA ILE BAHASHA FASTA IKIWA NA MILION 2 LKN IMETUNA NA YALE MANYARAKA MENGINE WAKAJUA MILION 10 IKO MLE KUMBE MWENZAO ALIZIRUDISHA NYINGINE,AKAONDOA GARI MBIO,ANASEMA ILE TU KUNUSURIKA KUFA ALICHANGANYIKIWA AKATOKA MBIO MOJA KWA MOJA HADI MSIKITINI MWENGE,AKASWALI KUMSHUKURU MUNGU,AKARUDI NYUMBANI,ANASEMA ANAOGOPA KBS KWENDA TENA BANK NDO ALIKUWA ANAOMBA NIMUELEKEZE JINSI YA KUHAMISHA FEDHA TOKA KWENYE ACOUNT KWENDA M PESA ILI AWE ANATOLEA KWA WAKALA,TUWE MAKINI JAMANI PESA ZETU WENYEWE ZITATUUA!!!

 

3 comments:

Anonymous said...

Hapo mlimani city ni balaa. Same friday jamaa mwingine ametoka bank na 18m yake. Kufika gate la survey hao hao jamaa wa bodaboda wakamfuata na kumwambia tupe pesa uliyochukua bank. Akawapa, then akataka kimbia maana ofisi yake ipo maeneo hayo hayo. Aaah hawakumpa nafasi wakamlamba risasi. Ni marehemu sasa masikini baba wa watu.

Anonymous said...

Tanzania imekuwa crimanal. haifai. madawa ya kurevya, wahujumu wa mali ya umma, majambazi,alafu hao hao wafanyakazi wa benk ndio wanashirikiana na mijambawazi, kuwapoint watu wanaokuja chukua hela zao, tena wale watu wa kawaida,hawawapoint ile mjaamaa yenyemahela mpaka ya biashara ya midawa ya kulevywa, wanawogopa, kwa kwa kuwa wanmtandao mkubwa, ata wachukue sh. ngapi hawafwatili kwa kuwa ni criminal nao.kwa hiyo baadhi ya mifanyakazi ya benk ni micriminal mijambawazi,

Anonymous said...

What do you expect kama polisi wamekalia kukusanya rushwa tu? Wahalifu wanajua polisi wa Tanzania hawana muda wa kupambana na uhalifu.