Tuesday, August 19, 2014

Rais Kikwete Atoa Rambirambi Kwa Familia ya Jaji MakameRais Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwafariji wafiwa walipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.

 Mama Salma Kikwete akiweha saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kutoa pole nyumbani kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kwanza wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu, Mheshimiwa Lewis Makame Masaki jijini Dar es salaam aliyefariki  katika Hospitali ya AMI Trauma Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.

PICHA NA IKULU

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Rais  wa Jamhuri  ya  Muungano wa Tanzania,  MheshimiwaDkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za  RambirambiMwenyekiti  wa  Tume ya  Taifa  ya  Uchaguzi,  National  Electoral Commission  (NEC)  kufuatia taarifa  za  kifo  cha  aliyekuwaMwenyekiti wa Kwanza wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu, MheshimiwaLewis  Makame  kilichotokea  katika  Hospitali  ya  AMI  TraumaCentre Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Agosti, 2014.

 “Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifocha  Jaji  Mstaafu  wa  Mahakama  ya  Rufaa  Tanzania  naMwenyekiti  wa  Kwanza  wa  Tume ya  Taifa  ya  Uchaguzi(NEC)  chini  ya  Mfumo  wa  Vyama  Vingi  vya  Siasa,Mheshimiwa  Lewis  Makame  ambaye  amelitumikia  Taifaletu  katika  Utumishi  wa  Umma  kwa  uaminifu,  uadilifu,bidii  na  umahiri  mkubwa”,  amesema  kwa  masikitiko  RaisKikwete katika Salamu zake.

  Katika utumishi wake, Marehemu Jaji Lewis Makame, enzi zauhai wake, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kabla yakuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa na baadaye Mwenyekiti wa NECambayo  aliiongoza  kwa  miaka  17  mfululizo  hadi  alipostaafumwaka 2011.  Uongozi wake ulichangia sana kuimarisha amani,utulivu, umoja na mshikamano wa kitaifa katika mazingira mapyaya demokrasia ya vyama vingi vya siasa hapa nchini.“Ni  kwa  kutambua  kipaji  kikubwa  cha  uongozialichokuwa  nacho  Marehemu  Jaji  Lewis  Makame,  Taifa.

No comments: