Showing posts with label Blog. Show all posts
Showing posts with label Blog. Show all posts

Saturday, April 07, 2018

Serikali ya Marekani Kufuatilia blogu zote DunianI!

Kama una blogu, serikali ya Marekani itakuchunguza!  Watafuatlia zipi zina nguvu ya kushawishi wasomaji....pia watafuatilia waandishi wa habari, magazeti na wahariri.

******************************************

Homeland Security to Compile Database of Journalists, Bloggers

The U.S. Department of Homeland Security wants to monitor hundreds of thousands of news sources around the world and compile a database of journalists, editors, foreign correspondents, and bloggers to identify top “media influencers.”

It’s seeking a contractor that can help it monitor traditional news sources as well as social media and identify “any and all” coverage related to the agency or a particular event, according to a request for information released April 3.

The data to be collected includes a publication’s “sentiment” as well as geographical spread, top posters, languages, momentum, and circulation. No value for the contract was disclosed.

“Services shall provide media comparison tools, design and rebranding tools, communication tools, and the ability to identify top media influencers,” according to the statement. DHS agencies have “a critical need to incorporate these functions into their programs in order to better reach federal, state, local, tribal, and private partners,” it said.

The DHS wants to track more than 290,000 global news sources, including online, print, broadcast, cable, and radio, as well as trade and industry publications, local, national and international outlets, and social media, according to the documents. It also wants the ability to track media coverage in more than 100 languages including Arabic, Chinese, and Russian, with instant translation of articles into English.

The request comes amid heightened concern about accuracy in media and the potential for foreigners to influence U.S. elections and policy through “fake news.” Nineteen lawmakers including Reps. Josh Gottheimer (D-N.J.), Lee Zeldin (R-N.Y.), Ron DeSantis (R-Fla.), and Sen. Ted Cruz (R-Texas), sent a letter to Attorney General Jeff Sessions last month, asking whether Qatar-based Al Jazeera should register as a foreign agent because it “often directly undermines” U.S. interests with favorable coverage of Hamas, Hezbollah and al-Qaeda’s branch in Syria.

The DHS request says the selected vendor will set up an online “media influence database” giving users the ability to browse based on location, beat, and type of influence. For each influencer found, “present contact details and any other information that could be relevant, including publications this influencer writes for, and an overview of the previous coverage published by the media influencer.”

A department spokesman didn’t immediately return a phone call and email seeking comment.

Responses are due April 13. Seven companies, mainly minority- or women-owned small businesses, have already expressed interest in becoming a vendor for the contract, according to the FedBizOpps web site.

Saturday, November 23, 2013

Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu - Rais Kikwete awaambia Watanzania

Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu, Rais Kikwete awaambia Watanzania

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  • Teteeni nchi badala ya kuiponda kwenye mablogu, Rais Kikwete awaambia Watanzania 

Watanzania waishio nje Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema wajibu mkuu wa Watanzania wanaoishi nje ya nchi ni kuisemea vizuri, kuihangaikia na kuitetea nchi badala ya kushinda kwenye mablogu wakiiponda, kuibeza na kulalamika.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa kuishi kwa Watanzania nje ya nchi kutaonekana jambo la maana zaidi ikiwa watatumia rasilimali na fursa wanazozipata ugenini kusaidia kubadilisha hali na maisha ya ndugu zao waliobakia Tanzania.

Rais Kikwete pia amewaonya Watanzania hao wasije kuchanganyikiwa na kujichanganya wenyewe kwa kuiga tamaduni za kigeni kupita kiasi. 


Rais Kikwete alikuwa anazungumza na Watanzania waishio nchini Poland usiku wa jana, Alhamisi, Novemba 21, 2013, kwenye Hoteli ya Bristol mjini Warsaw ambako alifikia wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku nne katika Poland.

Aliwaambia Watanzania hao na familia zao: “Matumaini na matarajio yetu sisi tuliobakia nyumbani ni kwamba mtaisemea vizuri nchi yetu, mtaitetea nchi yenu, mtaihangaikia nchi na kuleta faida nyumbani. Ni jambo haliingii akilini kuwa baadhi yenu mnaweza kuishi hapa na kazi yenu ikawa ni kushinda kwenye mablogu mkilaumu nchi yenu wenyewe. Nchi mbaya,
viongozi hawafai..mnapata faida gani. Mnazo nchi ngapi?”

Aliongeza Rais Kikwete: “Kuhangaikia nchi yetu ni wajibu wenu ambao hamwezi kuukwepa. Matumaini yetu ni kwamba asukuma mbele maslahi ya nchi yenu, mtatetea ustawi wa nchi yenu na ndugu zenu. Fursa zilizoko hapa mnazijua wenyewe, sisi hatuzijui. Nyie ndio mnaishi hapa, sisi tuko mbali na hatuwezi sisi kutegemewa na kutarajiwa tufanye
mambo ya hapa ambayo hatuyajui.”

Alisisitiza Rais Kikwete: “Mbona kazi za ma-Ngo’s mnazifanya vizuri bila kusukumwa ama kushawishiwa lakini kazi za kusaidia ndugu zenu hamfanyi? Kama hata hamwezi kusaidia ndugu zenu mnachangia nini nchi yenu?”
Rais amesema kuwa kwa Watanzania waishio nje kuonekana wanajali na kutetea nchi yao kutasaidia kujenga hoja ya msingi kuhusu umuhimu wa kuanzishwa kwa uraia pacha (dual citizenship) ambao Watanzania waishio nje wanaulilia. “Mnaweza kuhalalisha hoja ya uraia pacha kwa kuwa watu wenye faida kwa nchi.”

Kuhusu ombi lao la uraia pacha, Rais Kikwete amesema kuwa ni wajibu wa Watanzania waishio nje kuongeza kasi ya kuchangia mjadala kuhusu suala hilo ili likubaliwe kuingizwa kwenye Katiba Mpya.

“Rasimu ya kwanza ya Katiba ililikataa jambo hilo kwa sababu hili ni jambo lisilokuwa na ushabiki na upenzi mwingi nyumbani. Ujumbe wangu kwenu ni jipangeni vizuri kutetea hoja yenu hii. Saidieni mjadala wa jambo hilo badala ya
kushinda kwenye mablogu mkijadili siasa na hivyo kusahau yenye maslahi kwenu.”

Kuhusu kuiga tamaduni za nchi nyingine na kusahau za nyumbani, Rais Kikwete aliwaambia kuwa inaelekea kuwa baadhi wachache wanaoishi nje ya nchi, wamejichanganya na kuchanganyikiwa kiasi cha kusahau mambo ya kwao.

Rais Kikwete alitoa kauli hiyo baada ya mmoja wa Watanzania kudai kuwa suala zima la mahari limepitwa na wakati na kuwa kutoa mahari ni sawa ni kuwauza watoto wa kike.

Rais ambaye alionyesha kushangazwa na kauli hiyo, alijibu: “Msiige mambo ya kigeni kiasi cha kuanza kuchanganyikiwa.”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

22 Novemba, 2013

Sunday, March 17, 2013

Mjengwa asitisha mahusiano na Ludovick Joseph kwa Tuhuma za "Kuhusika na matukio ya kigaidi'

TAARIFA RASMI KUTOKA Mtandao Wa Kijamii Wa MJENGWA BLOG

Sunday, 17 March 2013 | Written by Mjengwa Blog

Ndugu zangu,
Kutokana na kuwepo kwa taarifa rasmi za kipolisi zenye kumtuhumu Ludovic Joseph kuhusika na matukio ya kigaidi.

Uongozi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog unasitisha rasmi, kuanzia leo Jumapili, Machi, 17,2013, kuwa na Ludovick Joseph kama msaidizi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Maggid Mjengwa,
Mmiliki wa Mjengwablog /Kwanzajamii

Thursday, March 07, 2013

Tollyzkitchen Blog Kuhusu Chakula na Mapishi


Keki Enye Hadhi ya Kitaifa

Breakfast au Lunch Safi Sana

Maandazi

Wadau, tembelea Blog ya Tollyzkitchen kwa ajili ya kupata ushauri kuhusu  vyakula na mapishi bora, na recipes safi.

Sunday, February 10, 2013

WITO KWA MABLOGA WETU KUWA WABUNIFU BADALA YA KUIBA AU KUNUKUU TU KAZI NA PICHA ZA WENZAO BILA IDHINI

WITO KWA MABLOGA WETU KUWA WABUNIFU BADALA YA KUIBA AU KUNUKUU TU KAZI NA PICHA ZA WENZAO BILA IDHINI

by Kitoto
Ukingoni mwa Ziwa Nyasa- Revo Meza
Wimbi la “blogging” liliikumba dunia kati ya 1995 hadi 1998 na kuanza kumea kwetu Tanzania kupitia mwanahabari Ndesanjo Macha miaka kumi iliyopita. Wakati Ndesanjo anaanza kublogu si wengi tuliomwelewa. Nakumbuka alivyokua akiniongelea juu ya fani hii kwa hamasa kwenye 2002. Baadaye kidogo aliendesha Jikomboe, blogu lililokua na taswira ya majani mabichi ya ukoka. Enzi hizo hakukua na hata senti moja aliyoichuma.
Ndesanjo Macha
Ndesanjo Macha- mwasisi wa blogu Tanzania
Ndesanjo alikua akisema blogu ni dunia ya kesho ya mawasiliano.
Wakati huo vyombo vikubwa vya habari nchi zilizoendelea vilianza kuona umuhimu wa blogu vikaanza kuunda idara pembezoni mwa tovuti zake mama. Kwetu wenye magazeti wengi hawakupenda wanablogu;waliwaona washindani.
Mwaka ambapo wanablogu wetu walianza kuchomoza ilikua 2006 baada ya kifo cha wapenzi wawili wa Kitanzania waliouliwa kinyama Marekani. Blogu la Michuzi (ambalo halikua maarufu kama leo) na Radio Butiama (inayojulikana kwa jina Podcast) zilisimama dede kutangaza habari hizo. Hapo ndipo miye binafsi nilipoanza kuona namna blogaz walivyokuwa na mwendo mkali - zaidi ya vyombo vya habari vya kijadi.
Nilianza rasmi kublogu mwaka 2007- nikisaidiwa na Ndesanjo na wanabloga wengine walionitangulia; akina Simon Kitururu, Jeff Msangi (Bongo Celebrity) mathalan. Nilichogundua siku za mwanzo ni kwamba Blogaz husaidiana sana. “Ukiwa mbinafsi huendelei kama Bloga” alisisitiza Ndesanjo.
Goats feeding on rubbish
Mbuzi wetu Bongo wakila kila aina ya takataka mitaani. Nyama yake tamu. Lakini je, ina nini kinachotudhuru tusichokijua? Nilipiga picha hii, Zanzibar, mwaka 2011.
Leo Jikomboe na ule ukoka havipo tena.
Ndesanjo, mwasisi wa blog za Kiswahili duniani, anafanya kazi shirika la habari- Global Voices. Kati ya mamia ya waandishi wa shirika hilo la kimataifa, Mtanzania huyu anaongoza kwa habari asilia za uchambuzi zaidi ya 4,200 . Tofauti ya mtu kama Ndesanjo na baadhi ya blogaz ni kwamba yeye kiasilia ni mwanahabari hivyo anachanganya ujuzi na mitindo hii miwili ya kusanifu matukio. Si ajabu mwaka jana Ndesanjo alishinda tuzo la Mwanablog bora wa Afrika.

KWA HABARI ZAIDI BOFYYA HAPA:

Monday, November 26, 2012

Friday, June 29, 2012

Miss Utalii Blog



Tunawatambulisha Kwenu Blog maalum ya Miss Utalii Tanzania/Miss tourism Organisation.


Miss Utalii Tanzania, tofauti na mashndano mengine ya urembo, ni zaidi ya shindano la urembo, kwani linalenga katika kutangaza na kuhamasisha Utalii,Utamaduni, Mianya ya Uwekezaji,Elimu,Afya ya Jamii,Utalii wa ndani,Utalii wa kitamaduni,Utalii wa Michezo na Utalii wa Mikitano Kitaifa na kimataifa. Shindano hili pia linahamasisha vita dhidi ya Umasikini,Iharibifu wa mazingira,uwindaji haramu,Uvuvi Haramu,Ujinga,Maradhi, Tamaduni kongwe na Potofu. Miss Utalii Tanzania pamoja na uchanga wake, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2005, ni shindano lenye mafanikio makubwa kuliko shindano jingine lolote nchini kitaifa na kimataifa kwani pamoja na kuipa heshima Tanzania ya kuwa wenyeji wa shindano la Dunia la Miss Tourism World 2006, shindano hili ndilo lililo andika historia ya Tanzania kutwaa taji la kwanza la Dunia kabla na baada ya uhuru, pale tulipo twaa taji la Miss Tourism World 2006, pia shindano hili ndilo pekee nchini linashikilia rekodi ya kutwaa mataji ya dunia katika kila shindano tulilo shiriki,tumetwaa mataji 6 ya dunia tangu 2005. Kutokana na mafanikio haya , Tumepewa heshima ya kuaandaa shindano la Dunia la Miss Umoja wa Mataifa mwaka 2013 hapa Tanzania. Ni shindano pekee nchini ambalo washiriki wake hawavai mavazi ya kuogelea, bali mavazi ya heshima yasiyo mdhalilisha mvaaji wala mtazamaji na yaliyo buniwa na kushonwa kwa malighafi za tanzania tu.

Link yetu ni : http://www.misstourismorganisation.blogspot.com/

Facebook Page: https://www.facebook.com/MissUtaliiTanzania

E-Mail: missutaliitanzania@gmail.com

Asanteni sana.
Miss Tourism Organisation Tanzania.

Tuesday, August 09, 2011

Blog Mpya ya Katuni



Njia za mitaani (Vichochoro) zimegeuzwa kuwa vyoo vya wapita nijia, Je, huu nao ni ujanja?? MUUNGWANA NI VITENDO


Kwa KATUNI, VIELELEZO na MICHORO aina zote mnakaribishwa Blog maridhawa ya katuni:
http://www.artsfede.blogspot.com/

Maoni na ushauri vinakaribishwa pia.

--
FeDe; Freelance Artist
P.O.Box 79267,
Dar-es-Salaam, Tanzania.
Mob; +255 783 006545
Blog; www.artsfede.blogspot.com

Father Kidevu ana Blogu Mpya

UNAKARIBISHWA FATHER KIDEVU BLOG www.mrokim.blogspot.com KUPATA HABARI KATIKA PICHA.

FATHER KIDEVU BLOG www.mrokim.blogspot.com , for local and International news in picture.

--

Mroki Mroki

Director MD Digital Company
General Secretary PPAT
Professional Photojournalist & BLOGGER
P.O.BOX 110097,
Mob: +255 755 373999 /+255 717 002303,
Email: mrokim@gmail.com.
Blog: www.mrokim.blogspot.com
DAR ES SALAAM, TANZANIA

Monday, July 25, 2011

Blog ya Picha za Wanamuziki




John Kitime ameanzisha blog eneye picha za wanamuziki wa Tanzania:

Angalia picha za wanamuziki mbalimbali na bendi nyingi zilizoko dar ambazo huwa hazipewi nafasi katika media ya kawaida tembelea www.musicintanzania.blogspot.com
--
http://www.wanamuzikiwatanzania.blogspot.com/

Tuesday, July 19, 2011

Udadisi Blog

UDADISI BLOG

My mission is to acquire, produce and disseminate knowledge on and about humanity as well as divinity, especially as it relates to Africa, in a constructive and liberating manner to people wherever they may be.

http://udadisi.blogspot.com

Twitter: @Udadisi

Friday, July 01, 2011

Taarifa ya MO Blog kwa Wadau

MO BLOG INAPENDA KUWAFAHAMISHA WADAU NA WASOMAJI WA BLOG HII KUWA TUMESIKITISHWA NA KUHUZUNISHWA NA TABIA INAYOENDELEA YA KUHUJUMIWA NA WAPINZANI WASIOPENDA MAENDELEO YETU KWA SABABU ZAO BINAFSI.

KWA MUDA MREFU TUMEKUWA KATIKA HARAKATI NA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA TUNAWAHABARISHA, ELIMISHA NA KUJADILIANA NA WADAU MBALIMBALI WA BLOG HII BILA KUINGIA UHURU WA WENGINE WALA KUKOSOA WENGINE, KWANI MAENDELEO YA KWELI YANATOKANA NA KUJIAMINI.

KWA MANTIKI HII TUNAOWAMBA RADHI WADAU WETU KWA KUTOKUWEPO HEWANI KWA SAA KADHAA LAKINI SASA MO BLOG IMERUDI NA ITAENDELEA KUWALETEA HABARI NA BURUDANI MBALIMBALI NANYI MSISITE KUTUSHAURI NA KUTUONGOZA KWA MAWAZO YA KUJENGA.

IKIWA NI MARA KWA MARA TATIZO HILI LA KUPOTEA NA KUPOTEZA KAZI ZETU KUTOKEA KATIKA BLOG YETU ,TUNAJIULIZA NI WAPI TUNAKOSEA AU KUHARIBU KATIKA UHABARISHAJI WETU WA HABARI NA MATUKIO ,AU KUFANYA HIVI NI MAKOSA..?!!! KWA KIFUPI MOBLOG INATEMBELEWA NA WATU 20,000 KWA SIKU NA HILI LINATUPA NGUVU NA KUFAHAMU KUWA WADAU WETU WANARIDHISHWA NA KUPENDEZWA NA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, BIASHARA, MICHEZO, BURUDANI NA INTERVIEWS ZA WATU MAARUFU WANAOJULIKANA NA WALE PIA WENYE VIPAJI WASIOJULIKANA. WADAU HILI NI KOSA…???

KWA MASIKITIKO MAKUBWA TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA KAZI ZOTE ZA MWAKA HUU 2011 ZILIZOPENDWA NANYI WADAU NA NYINGINE ZIKITOKANA NA MCHANGO WA NINYI WADAU NA WASOMAJI ZIMEPOTEA KWA LUGHA NYINGINE (ZIMEFUTWA/ZIMEPOTEZWA) KWA SABABU AMBAZO ZINATUTIA SHAKA NA KUTUPA HISIA KUWA NI ZA KIPINZANI.

TUSINGEPENDA KUSEMA MENGI NA WALA KUTAJANA MAJINA ILI KWA WEMA KABISA NA HEKIMA TUNAPENDA KUSISITIZA KUWA UPINZANI WA KUHARIBIANA SI MZURI NA HAUJENGI WALA KULETA MAFANIKIO KWANI MWISHO WA UBAYA NI AIBU.

HAIPENDEZI KUONGEA HAYA YOTE HAPA ILA YAKIZIDI NI AFUENI YA MOYO NI KUONGEA NA KUSEMA WAZI TUMECHOKA KUHUJUMIWA.

ASANTE KAKA MAKWAIYA KWA MSAADA WAKO, MKUBWA MICHUZI TUNAKUSHUKURU BILA KUMSAHAU MZEE WA FULL SHANGWE NA WENGINE KWA MISAADA MBALIMBALI NA USHAURI MLIOTUPA KWETU.

WADAU WA MOBLOG TUKO PAMOJA NATUTAENDELEA KULIJENGA TAIFA LETU KWA AMANI, UPENDO NA MATUMAINI.

TUNAWAPENDA, TUNAWATHAMINI, TUNAWAHESHIMU NA TUTAFANYA KAZI PAMOJA NA TUTAFIKA PALE TUNAPOKUSUDIA.
MUNGU IBARIKI MO BLOG NA WADAU WAKE WOTE.
Endelea kuperuzi MO BLOG www.mohammeddewji.com/blog

Wednesday, April 06, 2011

Blog ya Sanaa

Mdau Kennedy Mmbando ameanzaisha blogu kuhusu sanaa. Mtembelee... http://sanaakennedy.blogspot.com/

Saturday, March 12, 2011

Blogu Mpya - Tembea Tanzania

Kuna Blogu mpya kuhusu sekta ya Utalii Tanzania inaitwa:

TEMBEA TANZANIA.

**************************************************

Naomba kuchukua fursa hii kuitambulisha kwako Blog ya Tembea Tanzania
(http://tembeatz.blogspot.com/) Blog ya Kitanzania yenye kubeba habari mbali
mbali zinazohusu sekta ya Utalii ya hapa Nyumbani Tanzania.

Shukran na karibuni nyote

KK

Monday, May 17, 2010

Kaka Michuzi Anahamisha Blogu Yake!


Kutoka Kwa Kaka Michuzi:

Asalaam Aleikhum, Bwana Asifiwe, Tumsifu Bwana, Shalom, Namaste, konnichiwa, Nihao, olá.....
kwa heshima na taadhima nawaamkia wadau wote popote mlipo ulimwenguni. Salamu nilizotoa hapo juu naomba ifahamike kuwa hizo nilizozimudu ni kama kielelezo kwamba nia ni kumuamkua kila mmoja kwa nafasi yake popote alipo. Mie sijambo na naendelea na Libeneke kama kawaida.

Waama, baada ya salamu, napenda kuwafahamisha kwamba Globu ya Jamii hivi karibuni itaingia kwenye awamu mpya ya dot com, ikiwa katika jitihada za kuboresha Libeneke zaidi.

Imechukua muda kuchukua hatua hii kutokana na mazoea kwani toka September 8, 2005 hadi leo si kidogo ati. Hivyo mabadiliko kama yapo inabidi yafanywe kwa uangalifu wa hali ya juu ili kutoleta usumbufu wa aina yoyote kwa wadau wa Globu ya Jamii ambao kwangu ndiyo waajiri wangu wakuu.

Naam, wakati wowote kuanzia sasa libeneke la issamichuzi.blogspot.com litaingia katika awamu ya www.imichuzi.com. unakaribishwa kujaribu na kutoa maoni yako.
Mabadiliko haya tayari yameshaanza na sasa yako katika hatua za nchani. Kilichosalia ni kuhamisha 'mzigo' wote toka issamichuzi.blogspot.com na kuutua katika www.imichuzi.com ili libeneke liendelee vile vile kama siku zote, ukaicha mabadiliko kiasi ya muonekano.
Ni kweli jina litabaki lile lile la 'MichuziBlog' lakini si uwongo kwamba hivi sasa itakuwa tovuti kamili ila katika sura ya globu kama siku zote. Hii yote ni katika juhudi za kuongeza ufanisi, tija na vionjo vingi zaidi pamoja na kuondoa kero ya kusaka mitundiko iliyopita. Nadhani sasa itaeleweka kwa nini kulikuwa na kwikwi katika kutafuta posti za zamani.

Mdau usihofu kwamba labda utapata shida kusaka www.imichuzi.com. La, hasha. hautopata shida kwani hata kama utaingia Globu ya Jamii kwa kutumia issamichuzi.blogspot.com ama hata kwa kutumia 'michuzi' pekee utapelekwa moja kwa moja kwenye kurasa mpya bila matatizo. Isitoshe, posti zitabakia kwenye ukurasa wa mwezi husika na kuingia kwenye 'archive' baada ya mwezi huo kwisha.
Hivyo basi, kwa unyenyekevu naomba niwashukuru wadau wote popote mlipo kwa kampani yenu wakati wote huu ambayo kwa kweli bila nyie Libeneke lisingefikia hapa lilipo, hususan katika wakati huu wa kulifanya bora zaidi.

Maoni, ushauri na mawazo vinakaribiushwa kwa mikono miwili, pasina kusahau kukosoana kwa kujenga na mawazo mbadala ili kieleweke na Libeneke liendelee mbele.

Kwa kuwa nawapenda wadau wote, nitakuwa mtovu wa fadhila endapo kama sintowaonjesha Libeneke litalokuja kwa muonekano mpya. Hapo hapo naomba radhi kwa usumbufu wowote utaotokea kwani kama inavyofahamika si rahisi kwa binadamu kuwa sahihi kwa kila jambo. Hivyo n penye kwikwi na tusameheane na tushtuane haraka iwezekanavyo kupitia anuani ile ile ya issamichuzi@gmail.com ambayo nayo itabadikika mambo yakikaa sawa muda si mrefu ujao itakuwa info@imichuzi.com

Sunday, December 27, 2009

Salamu za Mwaka Kwa Bloggers

Amani, Heshima na Upendo kwako.

Kwanza napenda kumshukuru MUNGU kwa uhai wa kila mmoja wetu. Ni uhai huo unaotufanya sasa kuwasiliana hivi.

Pili napenda kutoa shukrani kwa kazi kubwa unayoifanya katika KUIELIMISHA, KUIBURUDISHA NA / AMA KUIKOMBOA JAMII YETU YA TANZANIA ambayo kwa hakika yatuhitaji sote. Tumekuwa pamoja katika kutimiza hili na najivunia uwingi wa blog zetu na utofauti wa maudhui yetu unaowafanya watu tofauti wenye kusaka "ladha" tofauti za habari-na-matukio kupata vyote toka kwetu.

Na sasa mwaka 2009 unakwisha na tunaelekea kuanza mwaka mpya wa 2010. Nakutakia mafanikio katika kila jema utendalo na hasa katika WAJIBU WETU WA HIARI wa kuisaidia jamii yetu ya Tanzania.

Lakini tunapoanza mwaka mpya, kuna mambo mawili ambayo ningependa kuomba na kusisitiza ndani ya jamii yetu.

Kwanza ni USHIRIKIANO. Tumeona ongezeko la wanajamii kwenye ulimwengu wa ku-blog na hili ni jambo jema. Lakini lina wema kama tutaweza kuungana na kuonesha UMUHIMU wa uwepo wetu. Tuko katika nyanja ama maudhui mbalimbali kama vile taswira, habari, uchambuzi, utambuzi, mitindo, mitazamo, imani nk, lakini sote twafanya haya kuiinua jami yetu ya Tanzania. Tunahitaji kuunganisha nguvu kwa kusomana, kutoleana maoni ambayo yanasisitiza, yanakosoa na kuelimisha zaidi jamii yetu.

Pili ni KUIREJESHEA JAMII. Kama sote twaandika kwa ajili ya jamii, basi tuwaze "ni kipi tutakachoifanyia jamii yetu kwa mwaka ujao kuionesha kuwa tuko pamoja nayo?" Binafsi niliwaza kuwa baada ya kumalizika kwa KONGAMANO LA BLOGGERS mwezi Februari, tuangalie namna ya kuunganisha nguvu na kufanya jambo moja la kuwajali walio katika mazingira magumu katika kuadhimisha SIKU YA KU-BLOG DUNIANI. Naamini tukianza mapema kukusanya michango kidogokidogo (hata kwa kutumia kamati itakayoaminika baada ya kongamano) tunaweza kufikia kiasi cha kubadili maisha ya jamii mojawapo. Iwe ni kuwanunulia mahitaji muhimu yatima ama kununua madawati, kujenga darasa, kusaidia maabara ama lolote litakaloonesha kuwa nasi tumetoka kwenye jamii hiyo, tunaikumbuka na tuko nayo katika kusaidia kutatua matatizo wanayokabiliana nayo. Tumeona mifano ya ndugu zetu waliounganisha nguvu na kufanikiwa kuibadili jamii (mfano ni hawa TUWA-USA http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/11/tuwa-usamashujaa-wetu.html)
Haya ni mawazo ambayo naomba yawe kama chachu ya kujua nini twaweza kufanya kwa UMOJA kama wana-blog na kuirejeshea jamii.

Nawapenda nyote, nawaheshimu na nawaombea pia
Kwa niaba ya familia yangu na wana-changamoto wote, NAWATAKIA KILA LILILO JEMA KATIKA KUMALIZA MWAKA HUU NA KUANZA UJAO
BLESSINGSNB: Hizi ni salamu binafsi na si chapishi.

"www.changamotoyetu.blogspot.com"

Tuesday, June 05, 2007

Tangazo


Naomba wasomaji wa blog hii waelewe kuwa blogu yangu siyo journalism, Hakuna editor (Mhariri), na wala si hoji interview na kuandika habari hapa, sina ratiba maalum ya kuandika na wala silipwi. Hii Blogu ni maoni yangu na naandika na kuposti kwa wakati wangu. Na wala habari zinazoandikwa hapa haziwezi ku-qualify kupata award ya journalism, bali zinaweza kupata award ya blogging. Mtu yeyote anaweza kuanzisha blogu yake mwenyewe… hakuna qualifications zaidi ya kujua kuandikia, kusoma na kutumia internet. Asanteni.

Tuesday, May 22, 2007

Kama Huoni Blog

Wapendwa wasomaji blog sizifuti. Hapana zinaingia Archives, na kila mtu anaweza kuziona. Kama kuna blog uliyopenda na kwa sasa huoni, uangalie upande wa kushoto wa blog, halafu u-clik kwenye Archives. Kama unakumbuka mwezi ulioiona u-click kwenye mwezi na mwaka. Pia, unaweza kufanya Search hapo juu kwenye upande wa kushoto.