Tuesday, June 05, 2007

Tangazo


Naomba wasomaji wa blog hii waelewe kuwa blogu yangu siyo journalism, Hakuna editor (Mhariri), na wala si hoji interview na kuandika habari hapa, sina ratiba maalum ya kuandika na wala silipwi. Hii Blogu ni maoni yangu na naandika na kuposti kwa wakati wangu. Na wala habari zinazoandikwa hapa haziwezi ku-qualify kupata award ya journalism, bali zinaweza kupata award ya blogging. Mtu yeyote anaweza kuanzisha blogu yake mwenyewe… hakuna qualifications zaidi ya kujua kuandikia, kusoma na kutumia internet. Asanteni.

11 comments:

Anonymous said...

Da Chemi ulisahau kuwaambia wasiotaka kuisoma blogu yako wasisome. Waende kwingine.
Endelea na kazi nzuri!

Anonymous said...

THere you go again,unatwist kiswahili kututukana,journalism or no journalism we want mambo ya kusaidia jamii,its like you are telling us indirectly,take it or leave it' YOU seem to be too much of a MSWAHILI more content on kubomoa then kujenga

Unknown said...

Mdogo Chemi, First of all let me tell u that u are a strong woman and u have always been cool, kuna siku nili comment juu ya ile story ya jeshini kwamba u did not have to tell the world ur experience ukanijibu kwamba "watasema mengi si unajua sisi waswahili tulivyo umbea hauishi..."

sasa naona ume loose temper kidogo kwenye hilo tangazo, just remain cool as always.

Moja ya vigezo ya kazi uliyo changua ni kuchukua all critisims as one of the factors to make your work progress and not discourage u.

Uliaamua kuwa na blog yako kwanza kwa ajili yako mwenyewe (kazi yako) then kwa uma. Ku-visit hapa ni kipenda roho.

Michuzi is doing a good job too lkn utakuta watu wengine wanamtukana mpaka natamani nipasue PC niwafuate walipo...lkn nimeelewa mwamba wengi wanaoingia hapa au kwa michuzi wana matatizo yao binafsi hawana inner peace! nikuwaombea tu, so just ignore na endelea na kazi yako nzuri!
Waridi

Chemi Che-Mponda said...

waridi,

siyo kuwa nime lose temper, ila watu wengi kuwa na hoja hiyo hiyo moja. Siwezi kuwa discouraged hata kidogo, huoni hata nimeongeza posting time.

Michuzi, tunawasiliana karibu kila siku, na mambo ambayo anablock utashangaaa. Bado sijafikia stega ya kublock maoni.

Lakini kama navyosema mtu mwenye serious hoja hajiiti 'anonymous'.

Anonymous said...

Mie nafikiri tatizo linakuja kama mtu anaanza mashambulizi kwa mwandishi wa blog (personal attack) badala ya kuchanganua mada ambayo ipo kwenye blog. Kama washabiki wa hii blog tutajifunza kuchanganua mada badala ya kumtukana mwandishi, basi nafikiri kila kitakachoandikwa kitakuwa ni halali.

luihamu said...

Da Chemi,

You have a point,binadamu yeyote mwenye hoya hawezi kutumia jina ANONYMOUS.

Da chemi hongera,kaza buti umesema ukweli ndiomaana inauma,hata kama nimimi lazima nirekebishe tabia yangu.

Nuff Nuff Respect.Jah live.

Anonymous said...

Chemi you need to know what a blog is. Nafikiri hiki kitu ulipaswa kikijua kabla ujaamua kujiingiza kwenye hii tech. Na kama unasoma blog za wenzio, ungekuwa mpole kwani binadamu wote hatuwezi kuwa na mawazo sawa ndo maana kila mtu anaandika anavyotaka sababu is a free space, hata wewe hulipi kitu.

Nafikiri binadamu tunakubali challenges, kuna posting nyingine unaziweka humu zinakushushia hadhi yako. Kwanza jiulize kwanini watu wengi watoa ctitique? so unachatakiwa chukua hizo critique kama constructive ctiticism ili ujenge blog bora. Kwani sometimes unaweka udaku, na athari zake watu wanatoa comment kama topic ilivyo.

Angalia blog za akina Ndesanjo, Mjengwa, nk, kwa kweli zinapendeza kwani ni very educative. Kama unavyosema unaaangalia blog ya michuzi, pale kila aina ya wazo utalikuta ila michuzi mwenyewe yuko normal sababu alishazoea tabia za binadamu.

Mwisho, kumbuka blogs zote hakuna mtu analipwa bali ni hobby, na kama wewe ni hobby kuwa na blog kuwa mstaarabu na mwelimishaji.

Anonymous said...

mwenzio michuzi anaita "waosho vinywa" kuonyesha ukomavu kwenye hii tech. We need your maturity sense.

Huyu LUIHAMU naye anafikiria kizamani na mwenye mawazo mgando, sasa kwanini neno ANONYMOUS likawepo kama haliwezi kutumiwa. Jamani wakati mwingine tumia busara na chagua maneno ya kutumia.

Anonymous said...

We Chemi sikia wenzio wanavyokushushua ulivyojikomba kwa mtoto wa Kikwete;

1.Tarehe June 7, 2007 8:24:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

Sasa wewe Chemi ndo nini kutoa email yako?, Grow up dada, wewe ni mtu mzima sana maana umesoma na dada zangu walionizidi miaka 10. Hata nikiwaambia umemwambia mtoto wa Rais akutumie email watakushangaa.
umemsifia kwanza ukidhani akisoma sifa ndo ataku email?, kama alikuwa hakujui kabla sahauu dada kupata email from him.


2. Tarehe June 8, 2007 1:55:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous
UMENIFURAHISHA SANA ANONY ULIYEMSHUSHUA CHE MPONDA I COULDN'T IMAGINE SUCH AN ACT FROM HER ETI ANATOA EMAIL ??!!! HA HA HA HA VERY FUNNY. KWANZA WE MTU MZIMA SANA ACHA KUJIAIBISHA I NEVER THOUGHT YOU ARE THAT CHEAP!!

Any way unaweza soma mwenyewe kwenye blog ya michuzi

Anonymous said...

Aliyeandika hizo habari kwa Michuzi ni wewe anonymous fala wa 7:08AM. Hukutosheka kuposti kwa Michuzi ikabidi uposti upuuzi wako hapa. Acha UTOTO wewe fala. Ujishushue mwenyewe.

Anonymous said...

Ingawa mimi si mwanablogu wala si Mtanzania wala sikai Marekani ningependa kukuunga mkono. "Hii blogu ni maoni yangu na naandika na kuposti kwa wakati wangu". Napenda tu kusoma maoni yako. Kuhusu kila kitu!

Ukitoa maoni yako, si kualika jamaa wafikiri kidogo. Hii si "kusaidia jamii"? Si kuwa "very educative"? Si kuwa "mstaarabu na mwelimishaji"?

Nakubaliana na yule aliyeandika "basi nafikiri kila utakachoandika kitakuwa ni halali"

Nirudie tu : "endelea na kazi yako nzuri!"