Sunday, February 10, 2013

WITO KWA MABLOGA WETU KUWA WABUNIFU BADALA YA KUIBA AU KUNUKUU TU KAZI NA PICHA ZA WENZAO BILA IDHINI

WITO KWA MABLOGA WETU KUWA WABUNIFU BADALA YA KUIBA AU KUNUKUU TU KAZI NA PICHA ZA WENZAO BILA IDHINI

by Kitoto
Ukingoni mwa Ziwa Nyasa- Revo Meza
Wimbi la “blogging” liliikumba dunia kati ya 1995 hadi 1998 na kuanza kumea kwetu Tanzania kupitia mwanahabari Ndesanjo Macha miaka kumi iliyopita. Wakati Ndesanjo anaanza kublogu si wengi tuliomwelewa. Nakumbuka alivyokua akiniongelea juu ya fani hii kwa hamasa kwenye 2002. Baadaye kidogo aliendesha Jikomboe, blogu lililokua na taswira ya majani mabichi ya ukoka. Enzi hizo hakukua na hata senti moja aliyoichuma.
Ndesanjo Macha
Ndesanjo Macha- mwasisi wa blogu Tanzania
Ndesanjo alikua akisema blogu ni dunia ya kesho ya mawasiliano.
Wakati huo vyombo vikubwa vya habari nchi zilizoendelea vilianza kuona umuhimu wa blogu vikaanza kuunda idara pembezoni mwa tovuti zake mama. Kwetu wenye magazeti wengi hawakupenda wanablogu;waliwaona washindani.
Mwaka ambapo wanablogu wetu walianza kuchomoza ilikua 2006 baada ya kifo cha wapenzi wawili wa Kitanzania waliouliwa kinyama Marekani. Blogu la Michuzi (ambalo halikua maarufu kama leo) na Radio Butiama (inayojulikana kwa jina Podcast) zilisimama dede kutangaza habari hizo. Hapo ndipo miye binafsi nilipoanza kuona namna blogaz walivyokuwa na mwendo mkali - zaidi ya vyombo vya habari vya kijadi.
Nilianza rasmi kublogu mwaka 2007- nikisaidiwa na Ndesanjo na wanabloga wengine walionitangulia; akina Simon Kitururu, Jeff Msangi (Bongo Celebrity) mathalan. Nilichogundua siku za mwanzo ni kwamba Blogaz husaidiana sana. “Ukiwa mbinafsi huendelei kama Bloga” alisisitiza Ndesanjo.
Goats feeding on rubbish
Mbuzi wetu Bongo wakila kila aina ya takataka mitaani. Nyama yake tamu. Lakini je, ina nini kinachotudhuru tusichokijua? Nilipiga picha hii, Zanzibar, mwaka 2011.
Leo Jikomboe na ule ukoka havipo tena.
Ndesanjo, mwasisi wa blog za Kiswahili duniani, anafanya kazi shirika la habari- Global Voices. Kati ya mamia ya waandishi wa shirika hilo la kimataifa, Mtanzania huyu anaongoza kwa habari asilia za uchambuzi zaidi ya 4,200 . Tofauti ya mtu kama Ndesanjo na baadhi ya blogaz ni kwamba yeye kiasilia ni mwanahabari hivyo anachanganya ujuzi na mitindo hii miwili ya kusanifu matukio. Si ajabu mwaka jana Ndesanjo alishinda tuzo la Mwanablog bora wa Afrika.

KWA HABARI ZAIDI BOFYYA HAPA:

No comments: