Sunday, March 17, 2013

Mjengwa asitisha mahusiano na Ludovick Joseph kwa Tuhuma za "Kuhusika na matukio ya kigaidi'

TAARIFA RASMI KUTOKA Mtandao Wa Kijamii Wa MJENGWA BLOG

Sunday, 17 March 2013 | Written by Mjengwa Blog

Ndugu zangu,
Kutokana na kuwepo kwa taarifa rasmi za kipolisi zenye kumtuhumu Ludovic Joseph kuhusika na matukio ya kigaidi.

Uongozi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog unasitisha rasmi, kuanzia leo Jumapili, Machi, 17,2013, kuwa na Ludovick Joseph kama msaidizi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Maggid Mjengwa,
Mmiliki wa Mjengwablog /Kwanzajamii

3 comments:

Anonymous said...

Baada ya kuwekwa video ya kupanga mbinu za kuteka na kutesa inayo
muonyesha mkurugenzi wa usalama wa Chadema kwenye mitandao ya kijamii
tumeshuhudia uharaka wa jeshi la Polisi kumkamata, kumhoji na kumuweka
ndani kiongozi huyo, lakini pia hayakupita masaa 48 wakamkamata kijana
mwingine mwenye jina la Ludovick Joseph kwa kuhisiwa kuwa ameshiriki
kwa namna moja au nyingine kwenye uttengenezaji wa video hiyo japo
naye inasemekana siku aliyo tekwa Kibanda naye alitekwa na
kunyang'anywa vitendea kazi vyake pamoja na nguo alizo kuwa amevaa.

Kwa kuwa nchi iko kwenye mtanziko wa mauwaji ya raia wasio kuwa na
hatia ikiwa ni pamoja kutekwa na kuteswa kwa wanahabari na wengine
kuuwawa kinyama nimejikuta najiuliza maswali kadhaa.

1. Jeshi la polisi linashindwa nini kumkamata Mwigulu Mchemba aliye
wahi kusema kwenye vyombo vya habari kuwa ana mkanda unao onyesha
viongozi wa chadema wakipanga mauwaji?! Kwa nini jeshi la Polisi
lisipate mahali pa kuanzia kwa kumkamata kiongozi huyu wa ccm?! Kama
wamemkamata Rwekatare, wanashindwa nini kumkamata Mwigullu?

2. Kwa kuwa mitandao ya kijamii imekuwa chanzo cha kupatia taarifa
jeshi la polisi (kama video inayo muonyesha Rwekatare na hatimaye
kumkamata), je polisi inashindwa nini kumkamata Sheikh Illunga ambaye
naye video yake ya kuhamasisha waumini wa dini yetu (Kinyume na
mafundisho ya Quran) iko bado kwenye mitandao ya kijamii na watu
wakiendelea kuangalia na kusikiliza uchochezi wake?, mkumbuke kuwa
kuna tishio la viongozi wa dini nyingine kuuwa.

Naamini Tanzania ni yetu sote na hakuna aliye mtanzania zaidi kuliko
mtanzania mwingine. Kila mwenye makosa afikishwe kwenye vyombo vya
sheria na sheria zisiwe zenye meno kwa baadhi ya watu na sheria
hizohizo zisigeuke kibogoyo kwa watu wengine.

Tumeona mateso ya Dr Ulimboka na wahusika kutajwa kwenye baadhi ya
vyombo vya habari lakini mpaka leo wahusika hawaja chukuliwa hatua
zozote.

Anonymous said...

Habari zinatisha, kumbe LJ ni kijana wa Usalama wa Taifa?

Anonymous said...

Distancing from oneself! Mjengwa mnafiki sana!