Showing posts with label FFU. Show all posts
Showing posts with label FFU. Show all posts

Tuesday, September 04, 2012

Mauaji Iringa Yamtesa IGP Mwema!

Kutola Gazeti la Mwananchi

Tanzania Inspector General of Poice Mr. Said Mwema

Mauaji Iringa Yamtesa

Tuesday, 04 September 2012
AJICHIMBIA KUTETA NA VIGOGO WA POLISI, VIONGOZI CHADEMA, DK NCHIMBI AKATISHA ZIARA AREJEA NCHINI

Waandishi Wetu

TUKIO la kuuawa kwa mwandishi wa habari wakati polisi wakipambana na wafuasi wa Chadema mkoani Iringa, limelitikisa jeshi hilo na jana Mkuu wake (IGP), Said Mwema alilazimika kujifungia na vigogo wa polisi Mkoa wa Iringa kujadili suala hilo.

Wakati IGP Mwema akifanya mkutano huo, uliodumu kwa zaidi ya saa mbili na nusu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi amelazimika kukatisha ziara yake ya kikazi Afrika Kusini na kurejea nchini kushughulikia suala hilo.

Mwema alienda Iringa jana na kuitisha mkutano huo uliowahusisha pia viongozi wa Chadema, akiwamo Katibu Mkuu wake, Dk Willibrod Slaa katika mazingira yaliyoelezwa kuwa na ulinzi mkali.

Hii ni mara ya kwanza IGP Mwema kwenda mwenyewe kwenye mikoa kunakotokea vurugu kati na vyama vya siasa na baadaye mauaji ya raia.

Julai 15, mwaka huu vurugu za aina hiyo zilitokea mkoani Singida ambako Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Kata ya Ndago wilayani Iramba, Yohana Mpinga aliuawa kwa kupigwa na silaha za jadi.

Pia mkoani Morogoro, Ally Zona aliuawa katika vurugu zilizoibuka baina ya polisi na wafuasi wa Chadema katika haraka za jeshi hilo kuwasambaratisha wafuasi hao kwa kile ilichoeleza kuwa maandamano yao yalipigwa marufuku.

Katika vurugu zote hizo, IGP amekuwa akituma wawakilishi au kutumia polisi kwenye mkoa husika kushughulikia matatizo hayo.

Makubaliano ya Kikao

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zimeeleza kuwa polisi imekubaliana na Chadema na Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) kusitisha majadiliano yote yanayohusu kifo cha mwandishi huyo hadi mazishi yake yatakapokamilika.

Mwenyekiti wa UTPC, Kenneth Simbaya alisema baada ya mkutano huo kuwa wamekubaliana kuwa na mkutano mwingine baada ya shughuli za mazishi kukamilika.

“Tulichoomba kifanyike ni kwamba, tumzike mwenzetu halafu majadiliano mengine juu ya ilikuwaje kwa nini na nini kifanyike kwa siku za usoni yatakuja,” alisema Simbaya.

Alisema sasa wanasubiri mwili wa Mwangosi ufanyiwe uchunguzi na wataalamu kutoka Dar es Salaam kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Katibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Francis Godwin alisema uchunguzi wa awali wa IPC unapingana kwa asilimia zote na taarifa ya jeshi hilo kwa kuzingatia taarifa zilizotolewa na baadhi ya waandishi waliokuwapo katika tukio hilo.

“Taarifa kutoka katika vyanzo vyetu zinaonyesha kwamba Mwangosi alipigwa kwa virungu kabla ya kulipuliwa na bomu hilo ambalo kwa vyovyote vile mhusika wake mkuu anaweza kuwa jeshi hilo na ili taarifa hiyo potofu isiendelee kuugubika umma, IPC imeamua kutoa tamko linalolenga kuviarifu vyombo huru viingilie kati uchunguzi,” alisema Godwin.

Nchimbi Katisha Ziara

Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi jana alilazimika kukatisha ziara yake ya kikazi, Afrika Kusini na kurudi nchini ambako pamoja na mambo mengine, atazungumza na waandishi wa habari leo kuhusu tukio hilo.

Nchimbi anarejea nchini wakati Naibu wake, Pereira Ame Silima akikataa kulizungumzia akisema uchunguzi umeshaanza.

Silima alisema tukio hilo linachunguzwa kwa pamoja kati ya Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba na IGP Mwema... “Mwema na Manumba wanaelekea Iringa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo na baadaye ndipo jeshi la polisi litaweza kueleza ni kitu gani hasa kimetokea.”

Alisema kwa sasa lolote litakalozungumzwa juu ya tukio hilo litakuwa ni hisia tu na ukweli utajulikana baada ya uchunguzi huo kukamilika.

ongozi wa kampuni ya Africa Media Group ambao wanamiliki Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, umeitaka Serikali kuanzisha uchunguzi huru ili kubaini sababu na mazingira ya kuuawa kwa mwandishi huyo ambaye alijiunga na kampuni hiyo mwaka 2006.

Taarifa iliyotolewa na kampuni na kusainiwa na Mhariri Mkuu wa Channel Ten, Dina Chahali imetaka uchunguzi huru kufanyika na kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Tunalaani vikali tukio hili ambalo halikubaliki kwa jinsi yoyote ile, tunataka kuanzishwa uchunguzi huru na hatimaye nguvu za kisheria zitumike,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

CHADEMA Yamtaka Rais Kikwete Kuwawajibisha Polisi!

Mkurugenzi wa Habari na Uenezi Chadema, John Mnyika akionesha picha ya polisi wakizingira Ofisi ya Tawi la chama hicho katika Kijiji cha Nyololo, Mufindi iliyochapishwa na gazeti la Tanzania Daima

DAR ES SALAAM, Tanzania


CHAMA cha Demokrasi na Maendelea (Chadema), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwasimamisha kazi vigogo wote wa Jeshi la Polisi, ambao wamekuwa wakitoa taarifa mbalimbali za uongo kuhusu mauaji ya mwandishi Daudi Mwangosi, ama awatake wajiuzuru nyadhifa zao, kupisha uchunguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, John Mnyika, aliwataja vigogo hao wa polisi kuwa ni Kamanda wa Operesheni wa Polisi, Paul Chagonja na RPC wa Iringa, Michael Kamuhanda

Wawili hao kwa mujibu wa Mnyika, kwa nyakati tofauti walidai kuwa marehemu alifikwa na mauti baada ya kuchoropoka kutoka kwa kundi la wafuasi wa Chadema na kukimbilia mikononi mwa Polisi na ghafla kulitokea mlipuko wa bomu la machozi uliosababisha kifo chake, jambo ambalo sio la kweli.

Mnyika alisema maneno hayo yanayotafuatiana na kuyaita kuwa ni ya uongo ukizingatia kwamba picha mbalimbali zimeonesha ikiwemo waandishi waliokuwemo eneo la tukio kutoa ushuhuda wao.

Kutokana na hali hiyo, Mkurugenzi huyo alisema ipo haja ya vigogo hao kung’oka kupisha uchunguzi, ili uweze kufanyika kwa haki na kuongeza kwamba Rais atumie madaraka yake kuhakikisha askari saba wanaoonekana katika picha 'wakimsghulikia' marehemu kukamatwa haraka na kuhojiwa ni nani alifyatua bunduki, kwa namna gani na vigogo gani walitoa amri hiyo.

Kwa mujibu wa Mnyika, Polisi imekuwa na tabia ya kukamata raia wanaokuwa eneo la tukio pindi kunapotokea mauaji kama hayo, hivyo ni wakati sasa wa Polisi wanaoonekana katika picha wakimshambulia marehemu Mwangosi nao kukamatwa.

Aidha alilitaka Jeshi la Polisi nchini lisitumie vibaya fedha za walipa kodi kwa kuchunguza nani alihusika na mauaji hayo wakati wauaji wanaonekana.

Mwandishi wa Habari Auwawa na Polisi Bongo!

The Late Daudi Mwangosi
Tanzanian Journalist Killed Reporting Police-Opposition Clash

               SEE HOW HE WA MURDERED AND HIS BODY MUTILATED HERE:
By Fumbuka Ng'wanakilala

DAR ES SALAAM
Tue Sep 4, 2012
DAR ES SALAAM (Reuters) - A leading Tanzanian editor accused police on Tuesday of beating up and killing television journalist Daudi Mwangosi, who died on Sunday during clashes between anti-riot police and supporters of the opposition CHADEMA party.

A police commissioner denied police responsibility but said he had ordered a joint military-police inquiry into the killing. Photos of the victim were uploaded onto the Internet and published by local newspapers.

Opposition leaders and activists linked the incident to a wider trend of rapidly growing violence against dissent in Tanzania and called for an independent inquiry.

Mwangosi was killed in a village in the Iringa region, about 500 km (315 miles) west of the capital Dar es Salaam, while reporting the clashes between police and CHADEMA supporters.

It was the first time in modern Tanzanian history that a journalist had been killed while doing his job, the Tanzania Editors' Forum (TEF) said.

"It was a deliberate move by the police, who clearly targeted this journalist. Eyewitnesses said the journalist was surrounded by police, beaten up and brutally killed," TEF secretary-general Neville Meena told Reuters.

Police fired a tear gas shell into Daudi's stomach at close range, Meena said. "Photos of fragments of Daudi's blown-up body hit the Internet less than one hour after the incident. We believe that the police are deliberately targeting journalists in a violent crackdown."

The police denied responsibility and said they had moved in to disperse an illegal gathering of opposition supporters.

"Police deny any deliberate involvement in the death of the journalist," police commissioner of operations Paul Chagonja said in a statement. "A commission of inquiry comprising officials from the police and military has been formed to investigate the death of the journalist."

Journalists at the scene uploaded images onto the Internet that they said showed Mwangosi's mutilated body lying on the ground, his abdomen ripped open and intestines spilling out.

Local newspapers published photos that showed a man lying on the ground, surrounded by anti-riot police officers who were beating him. The newspapers identified the man as Mwangosi, though the face was not recognizable.

"We condemn the killing ..." the Guardian newspaper of Tanzania said in an editorial. "It is unacceptable for the government and the public to rely on police investigations, knowing only too well that they are in this case one of the parties being blamed for the death of our colleague," it added.

Mwangosi's death came a week after one person was killed and several were wounded when police fired tear gas to break up an opposition protest in Morogoro town, a stronghold of the ruling CCM party.

(Editing by Yara Bayoumy and Tim Pearce)

MNAWEZA KUONA PICHA ZA MAUJI NA MAZISHI YA MAREHEMU DAUDI KWA KUBOFYA HAPA:

Monday, August 27, 2012

Polisi Waua Morogoro Leo!

Marehemu Ally Zona,  alikuwa ni muuza magazeti. Alipigwa risasi kichwani akiwa ameshika magaztei yake!  Hiyo jieraha inaonyesha kuwa marehemu alikuwa anakimbia kutoka kwa polisi. Alipigwa kwa nyuma.


Hapo awali ilielezwa kuwa wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kikisitiza kufanya maandamano leo kisha mkutano mkubwa wa hadhara, kuliibuka mvutano baina yake na Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro, kufuatia Kamanda wake, Faustine Shilogile kupiga marufuku mandamano hayo.

Kamanda Shilogile alieleza sababu za kuzuia maandamano hayo kuwa ni udogo wa barabara za Morogoro na kwamba leo ni siku ya kazi hivyo yanawezesha kusababisha usumbufu kwa wakazi wa mji huo.

Wakati Shilogile akieleza kuzuia maandamano yanayotarajiwa kuanza saa 5 asubuhi, Mkuu wa Operesheni Sangara, Benson Kigaila, alisisitiza kuwa watafanya maandamano kwa kuwa waliskubaliana na Kamanda Shilogile kabla ya kuwageuka.

Kwa mujibu wa Gazeti la Nipashe la 27 August 2012, ilielezwa kuwa Kamanda Shilogile alidai kuruhusu baiskeli na watu kutumia barabara kwa sababu ya mikutano ya Chadema itakuwa ni kuwanyima haki wananchi wengine, na hivyo wataruhusu watu wasiozidi 50 kupita kwa wakati mmoja pasipo kuwa na ishara ya kuonyesha kama wanaelekea katika maandamano.

Pichani ni kijana aliyeelezwa kupigwa risasi kichwani katika tafrani hizo na baadae kupoteza maisha Ametambulishwa kwa jina la Ally Zona, ambae alikuwa ansoma magazeti katika stendi ya Msamvu. Tukio hili lilitokea mapema leo asubuhi kuelekea saa sita mchana wakati Polisi walipokuwa wakiwatawanya wafuasi hao wa chadema. Mtoa taarifa anasema Polisi wanadaiwa kutumia risasi za moto pamoja na mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamani hao.

Watu wengine waliojeruhiwa katika tafrani hiyo wameelezwa kuwa ni mwenesha baiskeli Hashim Seif ambae amejeruhiwa kwa risasi mguuni akiwa napita na baiskeli yake na kijana mwingine aliielezwa kuwa ni muuza matunda Frank Valimba ambae amejeruhiwa na risasi tumboni.


KWA HABARI NA PICHA ZAIDI TEMBELEA KIBONGO BONGO BLOG:

********************************
TAMKO KUTOKA TANZANIA JOURNALIST ALLIANCE (TAJOA)


Jumuia ya Waandishi wa Habari Tanzania (Tajoa) inalaani kwa nguvu zote mauaji ya makusudi yaliyofanywa na Jeshi la Polisi leo mjini Morogro. Inashangaza Tanzania sasa inataka kugeuka taifa la polisi wauaji. NI vyema busara, ujuzi na mbinu stahiki zikatumika badala ya kuendelea kuua raia hata wasiokuwa na hatia.

Hebu ona huyu masikini alivyouawa kwa kupigwa risasi kwenye paji lake la uso na kumsab
abishia kifo cha papo hapo. Inaelezwa alikuwa muuza magazeti aliyekuwa kibandani kwake. Sasa tusubiri taaria ya Polisi ambayo huenda ikasema alikuwa amebeba silaha.

Tanzania, tusikubali kuwa taifa la polisi wauaji.

Marafiki wa Tajoa, nini sasa kifanyike kukomesha hali hii ambayo inaonekana kuota mizizi? Toa maoni yako hapa ili nasi tuyapeleke kwa Jeshi la Polisi

— 
Wafuasi wa Chadema wakiwa na maandamao hayo mjini Morogoro


Moshi wa mabomu yaliolipuliwa kutawanya maandamano ya Chadema leo mjini Morogoro

Akina Mama wakikimbia mabomu ya machozi

Wednesday, December 14, 2011

Hali UDSM Sasa ni Shwari!


Kuna vijana kadhaa huko UDSM ambao walileta fujo hapo Mlimani katika siku chache zilizopita. Hivi, hiyo migomo inasidia kweli au watu wachache ndo wanaumia?  Na wakiharibu mali ya watu inasaidia nini? Hao waliofukuzwa wataenda wapi? Ada zao zimepotea.

Mdau FK ambaye yuko UDSM campus (Mlimani) ameleta taarifa hii:
***********************************************************

Ukweli ni kwamba hapa chuoni kwa sasa ni shwari kabisa. Walimu tunaendelea na ufundishaji kama kawaida ingawa siku kadhaa hivi vipindi vya kuanzia saa 5 vilikuwa havifundishwi kutokana na wanafunzi kugoma. Kimsingi waliokuwa wanasababisha hali kutokuwa shwari ni wanafunzi wachache amabao walikuwa wakiwahimiza wenzao wawaunge mkono kwenye mgomo. Mwanzoni madai yao yalikuwa ni kupewa mikopo kwa wale waliokuwa wamenyimwa na baadaye wakabadili madai kwa kutaka wenzao waliokuwa wamesimamishwa kuachiwa pasipo masharti bila ya kuangalia kama baadhi yao walikuwa na kesi mahakamani.


Kwa tarehe 12, yaani juzi jumatatu, wanafunzi hao waliamua kuleta vurugu hapa chuoni kwa kwenda cafeteria kuwamwagia wenzao chakula, kuweka mchanga kwenye chakula kilichokuwa jikoni na kwenye masufuria na kuvunja majokofu yalioko cafeteria. Pia waliharibu mabasi yanayotoa huduma kati ya hosteli ya mabibo na chuo na kusababisha huduma hiyo kusitishwa mpaka leo. Ila jana Makamu Mkuu wa Chuo ametoa tamko na Baraza la Chuo na kuamua kwamba wanafunzi 8 wanasimamishwa masomo, 35 watasimamishwa kwa miezi 9 na 15 watapewa onyo.

Hata hivyo, bado polisi wanachukua tahadhari kwa kuhofu kuwa huenda wakajipanga tena kuja kuleta vurugu. Kimsingi inasemekana kuwa hao wanafunzi waliosimamishwa wanataka kupanga vurugu ili chuo kifungwe na wote warudi nyumbani. Kwa sasa hapa chuoni kuna landcuiser tatu za FFU lakini hakuna askari wa kutosha na hawana maji ya kuwasha zaidi ya kuwepo tu kwaajili ya tahadhari. Uamuzi wa kutowatawanya jana kwa virungu kumesadia sana kuiweka hali ya chuo kuwa shwari.

Monday, November 14, 2011

FFU Watumia Mabomu Iringa, Waandishi wa Habari Wajeruhiwa Vibaya!


Wananchi wakiishambulia nyumba inayotuhumiwa kuwa na misukule kwa mawe


kamera ya mwandishi wa ITV ikiwa imevunjwa




Mwandishi wa ITV Iringa Laulian Mkumbata akionyesha kamera iliyovunjwa



Wananchi wakiwa wameizunguka nyumba inayodaiwa kuwa na misukule ndani ,huku ndani ya nyumba hiyo kukiwa na wanahabari pia

Askari wa kikosi cha askari wa kutuliza Ghasia (FFU) Iringa watumia mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wananchi waliovamia nyumba ya mtumishi wa Mungu kwa madai kuwa kuna watu 15 wanaodaiwa kufa na kuonekana katika nyumba hiyo ( misukule).


Wananchi hao wenye hasira kali zaidi ya 200 walitumia mawe kuwashambulia FFU huku wao FFU wakitumia mabomu ya machozi kupambana Huku wanahabari wa vyombo mbali mbali na askari polisi na mchungaji mmoja wakinusurika kuuwawa wakishambuliwa kwa mawe na wengine kuvunjiwa kamera zao na wananchi hao ambao walionyesha kuwachukia askari polisi pamoja na wanahabari ambao waliteuliwa na wananchi wenyewe kuwawakilisha katika kukagua nyumba hiyo bila mafanikio .


Tukio hilo lilitokea eneo la Frelimo katika Manispaa ya Iringa na kudumu zaidi ya masaa manne baada ya kuanza majira ya saa 8 mchana na kuendelea hadi saa 12.50 jioni .


Wakielezea juu ya tukio hilo wananchi hao walisema kuwa walipata taarifa kutoka kwa mmoja kati ya wananchi wa eneo hilo kuwa katika nyumba hiyo ya mfanyabiashara wa maji kumeonekana misukule 15 ambayo ilionekana ndani ya uzio wa nyumba hiyo.


Kutokana na uvumi huo wananchi kutoka pande mbali mbali za mji wa Iringa walifika katika nyumba hiyo na kuizingira kwa lengo la kutaka kuichoma moto kabla ya askari polisi kufika na kuwaomba wananchi kutofanya hivyo na badala yake kuteuwa wawakilishi ili kuingia ndani ya nyumba hiyo kujikagua misukule hiyo bila mafanikio .


Hata hivyo baada ya askari hao walioambatana na wanahabari zaidi ya sita kutoka vyombo mbali mbali akiwemo mwandishi wa habari hizi kushindwa kuona misukule hao baadhi ya wanahabari akiwemo mwandishi wa habari hizi waliamua kuruka ukuta baada ya kuona wananchi wakionyesha jazba zaidi .


Huku baadhi ya waandishi wakiongozwa na katibu wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) Frank Leonard ambaye ni mwandishi wa gazeti la Habari leo wakilazimika kujifungia ndani ya nyumba hiyo baada ya wananchi kuanza kuishambulia kwa mawe .


Hali hiyo iliwalazimu askari polisi zaidi ya 10 walikuwepo kuanza kutumia mabumu ya machozi kuwatawanya wananchi hao ambao walikuwa wakiimba kuwa mmekela rushwa wote wanahabari,wachungaji na polisi hivyo lazima mchomwe moto .


Katika tukio hilo mabomu ya machozi zaidi ya 30 yalipigwa hewani huku wananchi wakizidi kuongezeka na kupelekea askari hao kuomba msaada zaidi wa askari wa FFU ambao walifika wakiongozwa na mkuu wa FFU mkoa wa Iringa Mnunka na kufanikiwa kuwatawanya wananchi hao .

Zaidi ya watu 10 walikamatwa na jeshi la polisi kwa kujihusisha na vurugu hizo huku watu wengine zaidi ya 20 wakiwemo wanahabari familia ya mfanyabiashara huyo ,mchungaji aliyefahamika kwa jina la Mang’uliso walijeruhiwa kwa mawe .


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Evarist Mangalla hakuweza kupatikana kuzungumzia madhara yaliyojitokeza katika tukio hilo japo mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari matatu likiwemo la polisi yakiwa yameharibiwa vibaya kwa mawe.


ZAIDI SOMA HAPA

Thursday, July 07, 2011

Hakuna Machinga Aliyeuawa Mwanza!

Jana kulikuwa na habari kuwa polisi waliua machingas mjini Mwanza. Mwandishi wa habari, Frederick Katulanda aliyeoko kule anasema kuwa habari hiyo si kweli!

***********************************************************************

I. HAKUNA MMACHINGA HATA MMOJA ALIYEUAWA KATI YA SABA WALIOJERUHIWA KATIKA VULUGU HIZO.
Majeruhi saba ni:
1. Juma Machumu (23) aliyejeruhiwa uso na eneo la shingo ambaye alikuwa amepoteza fahamu, 2. Pastory Briston (25) ambaye amejeruhiwa kiuno wote wakiwa wamelazwa ICU katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando baada ya awali kufikishwa Hospitali ya mkoa Mwanza Sekou Toure na hali zao kuwa mbaya zaidi hivyo kulazimu kuwarufaa huko, wengine ni 3. Omari Abdalah (25) Fundi wa Koroboi eneo la Makorobohi aliyejeruhiwa mkono kwa mawe, 4. Kelvin Jeremiah (16) kijana ambaye amejeruhiwa kwa risasi mgongoni na kutokeza upande wa mbele begani akiwa eneo la sokoni kuu la Mwanza akiingia sokono ambako alikuwa ametumwa na mama yake.
Majeruhi wengine ni 5. Kulwa John, 6. Dotto Thomas, 7. Medard Benard ambao hawa walikimbizwa na Polisi hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu moja kwa moja.

II. KWA NINI MAENEO MENGI YA WATANZANIA WENYE ASILI YA KIASIA YAMESHAMBULIWA.
Kwa muda mrefu eneo la shughuli za biashara ambalo limekuwa likiombwa na machinga limekuwa ni makoroboi, na eneo hili ndilo ambalo limekuwa na msikiti na shule za WAASIA toka miaka ya 1970, wakati wakipewa eneo la makoroboi na mkuu wa mkoa Abass Kandoro kurejea katikati ya jiji walipewa kwa sharti la kutovuka shule na msikiti wa waasia hao, walivuka na leo walikuwa wakiondolewa eneo hilo tu la shule waliozidi na ndipi vulugu zikazuka.
Hata hivyo kuzuka kwa vulugu hizo kumekuwa sababu ya wao kushambulia mali za WAASIA, magari, misikiti hiyo Mtaa wa Makoroboi, Maduka hii ni kutokana na dhana kuwa wao wamekuwa wakibughuziwa na wafanyabiashara wa kiasia kuoachwa wakifaidi nchi hii.
Huku wakidai kuwa kuna taarifa kuwa wao wamekuwa wakilipia posho za Polisi kwa lengo la kuwaondoa MAchinga eneo la makoroboi kila kunapokuwa na Oparesheni za kuwaondoa hivyo kujenga chuki nao.

--
Frederick M. Katulanda

**************************************************************
Taarifa za muda mfupi uliopita zinasema kumetokea tafrani kati ya polisi na machinga mjini Mwanza na kwamba machinga wawili wamepigwa risasi na kufariki. Tunaendelea kupeleleza!

Tuesday, May 31, 2011

Wanafunzi wa Tosamaganga Wapigwa Mabomu ya Machozi - Mwandishi wa Habari Atiwa Mbaroni!


(Pichani wanafunzi wa shule ya sekondari chini ya ulinzi wa FFU kabla ya kupigwa mabomu ya machozi. Picha na Franci Godwin)
Wadau, kumradhi kwa kuchelewa kubandika habari hizi. Nilikuwa na matatizo ya kompyuta.

Habari kutoka Iringa zinasema kuwa Mwandishi wa Habari Francis Godwin ametiwa jela baada ya kuripoti kuhusu mgomo wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Tosamaganga na hatimaye kupigwa mabomu ya machozi ya FFU.

Nabandika habari alizoandika Kaka Francis. Kwa Picha na Habari zaidi BOFYA HAPA:

May 31, 2011

BREAKINGNEWS.....NIPO CHINI YA ULINZI WA POLISI YATOSA YAMENIPONZA

Mwandishi wa mtandao huu Bw Francis Godwin kwa sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi baada ya kukamatwa katika shule ya sekondari Tosa maganga akifuatilia sakata la mgomo wa wanafunzi
***************************************************
May 30, 2011

Hali ya usalama si shwari katika shule ya sekondari Tosamaganga wilaya ya Iringa mkoani Iringa hivi sasa wanafunzi zaidi ya 1000 wapo porini wakikimbizwa na polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia ambao wanatumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanafunzi hao ambao walikuwa katika maandamano ya amani kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa wa Iringa kuulalamikia uongozi wa shule hiyo.

Hadi hivi saa mabomu zaidi ya 10 ya machozi yamepigwa kuwatawanya wanafunzi hao ambao baadhi yao wanadaiwa kujeruhiwa kwa kuchomwa na miti wakati wakikimbia porini kukwepa mabomu hayo huku wananchi wa Mseke wakikimbia nyumba zao.

Polisi wamewazuia waandishi wa habari akiwemo mmiliki wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao waliokuwepo eneo hilo wakifuatilia tukio hilo kuendelea kuchukua habari hiyo .

Undani wa habari hii ya picha zaidi zitakujia hivi punde japo kwa sasa binafsi macho yanauma sana kutokana na moshi ya mabomu hayo kunikuta pamoja na mwanahabari mwenzangu wa Radio Ebony Fm japo

*****************************************************
May 30, 2011

Hari si shwari shule ya sekondari Tosamaganga Iringa wanafunzi wote zaidi ya 1000 wameandamana kwenda kwa mkuu wa mkoa Iringa kupinga madai mbali mbali sasa wanaingi barabara kuu upo uwezekona wa mabasi kuzuiwa FFU Watanda shuleni habari kamili na picha zinakuja!

**********************************************************