Wednesday, December 14, 2011

Hali UDSM Sasa ni Shwari!


Kuna vijana kadhaa huko UDSM ambao walileta fujo hapo Mlimani katika siku chache zilizopita. Hivi, hiyo migomo inasidia kweli au watu wachache ndo wanaumia?  Na wakiharibu mali ya watu inasaidia nini? Hao waliofukuzwa wataenda wapi? Ada zao zimepotea.

Mdau FK ambaye yuko UDSM campus (Mlimani) ameleta taarifa hii:
***********************************************************

Ukweli ni kwamba hapa chuoni kwa sasa ni shwari kabisa. Walimu tunaendelea na ufundishaji kama kawaida ingawa siku kadhaa hivi vipindi vya kuanzia saa 5 vilikuwa havifundishwi kutokana na wanafunzi kugoma. Kimsingi waliokuwa wanasababisha hali kutokuwa shwari ni wanafunzi wachache amabao walikuwa wakiwahimiza wenzao wawaunge mkono kwenye mgomo. Mwanzoni madai yao yalikuwa ni kupewa mikopo kwa wale waliokuwa wamenyimwa na baadaye wakabadili madai kwa kutaka wenzao waliokuwa wamesimamishwa kuachiwa pasipo masharti bila ya kuangalia kama baadhi yao walikuwa na kesi mahakamani.


Kwa tarehe 12, yaani juzi jumatatu, wanafunzi hao waliamua kuleta vurugu hapa chuoni kwa kwenda cafeteria kuwamwagia wenzao chakula, kuweka mchanga kwenye chakula kilichokuwa jikoni na kwenye masufuria na kuvunja majokofu yalioko cafeteria. Pia waliharibu mabasi yanayotoa huduma kati ya hosteli ya mabibo na chuo na kusababisha huduma hiyo kusitishwa mpaka leo. Ila jana Makamu Mkuu wa Chuo ametoa tamko na Baraza la Chuo na kuamua kwamba wanafunzi 8 wanasimamishwa masomo, 35 watasimamishwa kwa miezi 9 na 15 watapewa onyo.

Hata hivyo, bado polisi wanachukua tahadhari kwa kuhofu kuwa huenda wakajipanga tena kuja kuleta vurugu. Kimsingi inasemekana kuwa hao wanafunzi waliosimamishwa wanataka kupanga vurugu ili chuo kifungwe na wote warudi nyumbani. Kwa sasa hapa chuoni kuna landcuiser tatu za FFU lakini hakuna askari wa kutosha na hawana maji ya kuwasha zaidi ya kuwepo tu kwaajili ya tahadhari. Uamuzi wa kutowatawanya jana kwa virungu kumesadia sana kuiweka hali ya chuo kuwa shwari.

3 comments:

Anonymous said...

Nadhani we mleta mada ni TUTORIAL ASSISTANT hapo UDSM, sasa unaona tayari kushakuwa mwalimu, nyambafu!

Unaongea kinazi na kinafiki, hayo maelezo yako yanaonesha low level ya elimu yako (Bachelor degree), waaalimu wenyewe (PhD holders)hawawezi kuongea upuuzi huo uloongea wewe, ukitoa Mkandara, na wasaidizi wake, ambao ndio wakandamizaji wa haki za hao wanafuzi!

Wewe unalia na outcomes (results) unashindwa kuangalia mzizi wa tatizo, hayo yakuvunja magari, kumwaga chakula ni just outcomes ya matatizo yaliyopandikizwa na na huo utawala hapo UDSM! Nna hakika hili unalijuwa vizuri, ni unafiki wako tu na ulimbukeni! Unashabikia wanafunzi wamwagiwe maji ya kuwasha wakidai haki zao, hivi wewe uligoma mara ngapi wakati wa Bachelor yako? (Kama ulisoma UDSM), Unataka askari waongezwe kuzuia watu kufikisha malalamiko yao, hivi wewe ni msomi wa aina gani? Hopeless kabisa!

Anonymous said...

Nimeangalia katika taarifa ya habari ya saa 2 usiku, Makamu Mkuu wa chuo hicho akitangaza kuhusu uamuzi wa kuwafukuza zaidi ya wanafunzi 40 katika chuo hicho na kuwa hawataruhusiwa kusoma katika chuo chochote cha umma nchini. Kitendo hicho kimetokea baada ya mgomo na uharifu uliotokea wiki hii pale chuoni.

Lakini Je, hii ni njia sahihi ya kutatua matatizo ya wanafunzi?
kwanini wanafunzi waligoma? mie najua hawa wanafunzi sio wehu na si
vichaa kabisa. Serikali ifikie wakati itambue mahitaji ya wananchi wao na si kutambua tu mahitaji ya wabunge na vigogo wengine serikalini.

Mimi nafananisha kitendo cha wanafunzi kugoma na kitendo cha wabunge
kujiongezea posho kijinga tu, tatizo tu ni kwamba wanafunzi kila
wakifanyacho wanaonekana ni wahuni tu!!!

Nachukia sana na maamuzi yanayochukuliwa na viongozi wetu bila hata ya kufikiria!!!!

Anonymous said...

Kilichowafanya waaribu magari ya watu nini jamani ndo waliwanyima pesa yao, mi naona poa wakafungwe na kurudisha magari ya watu haraka aisee.Nimesoma pale lakini ni ujinga kuaribu mali aiseee!