Thursday, July 07, 2011

Hakuna Machinga Aliyeuawa Mwanza!

Jana kulikuwa na habari kuwa polisi waliua machingas mjini Mwanza. Mwandishi wa habari, Frederick Katulanda aliyeoko kule anasema kuwa habari hiyo si kweli!

***********************************************************************

I. HAKUNA MMACHINGA HATA MMOJA ALIYEUAWA KATI YA SABA WALIOJERUHIWA KATIKA VULUGU HIZO.
Majeruhi saba ni:
1. Juma Machumu (23) aliyejeruhiwa uso na eneo la shingo ambaye alikuwa amepoteza fahamu, 2. Pastory Briston (25) ambaye amejeruhiwa kiuno wote wakiwa wamelazwa ICU katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando baada ya awali kufikishwa Hospitali ya mkoa Mwanza Sekou Toure na hali zao kuwa mbaya zaidi hivyo kulazimu kuwarufaa huko, wengine ni 3. Omari Abdalah (25) Fundi wa Koroboi eneo la Makorobohi aliyejeruhiwa mkono kwa mawe, 4. Kelvin Jeremiah (16) kijana ambaye amejeruhiwa kwa risasi mgongoni na kutokeza upande wa mbele begani akiwa eneo la sokoni kuu la Mwanza akiingia sokono ambako alikuwa ametumwa na mama yake.
Majeruhi wengine ni 5. Kulwa John, 6. Dotto Thomas, 7. Medard Benard ambao hawa walikimbizwa na Polisi hospitali ya rufaa ya Bugando kwa matibabu moja kwa moja.

II. KWA NINI MAENEO MENGI YA WATANZANIA WENYE ASILI YA KIASIA YAMESHAMBULIWA.
Kwa muda mrefu eneo la shughuli za biashara ambalo limekuwa likiombwa na machinga limekuwa ni makoroboi, na eneo hili ndilo ambalo limekuwa na msikiti na shule za WAASIA toka miaka ya 1970, wakati wakipewa eneo la makoroboi na mkuu wa mkoa Abass Kandoro kurejea katikati ya jiji walipewa kwa sharti la kutovuka shule na msikiti wa waasia hao, walivuka na leo walikuwa wakiondolewa eneo hilo tu la shule waliozidi na ndipi vulugu zikazuka.
Hata hivyo kuzuka kwa vulugu hizo kumekuwa sababu ya wao kushambulia mali za WAASIA, magari, misikiti hiyo Mtaa wa Makoroboi, Maduka hii ni kutokana na dhana kuwa wao wamekuwa wakibughuziwa na wafanyabiashara wa kiasia kuoachwa wakifaidi nchi hii.
Huku wakidai kuwa kuna taarifa kuwa wao wamekuwa wakilipia posho za Polisi kwa lengo la kuwaondoa MAchinga eneo la makoroboi kila kunapokuwa na Oparesheni za kuwaondoa hivyo kujenga chuki nao.

--
Frederick M. Katulanda

**************************************************************
Taarifa za muda mfupi uliopita zinasema kumetokea tafrani kati ya polisi na machinga mjini Mwanza na kwamba machinga wawili wamepigwa risasi na kufariki. Tunaendelea kupeleleza!

2 comments:

Anonymous said...

Tatizo la machinga mijini,ni matokeo ya viongozi wabovu,nina ushahidi usio na mashaka kuwa baadhi ya wafanyakazi wa halmashauri wanafaidi
uwepo wa machinga kwa kuwa kila mwisho wa wiki anapitia hela kwa
machinga!

Anonymous said...

Kwa mtazamo wangu hii mada ni ngum hivyo tunapaswa kuangali pande zote kabla hatuja tolea maoni yetu.

Wamachinga ni Watanzania wenzetu wanajitafutia kipato chao kwa njia hiyo kwa sababu ndio kazi anaeiweza na yote hayo yamewakuta kwa sababu ya kutokupewa elimu na hao hao serikali wanao jifanya wanatoa maeno kwa ajili ya biashara yao. Wao wamachinga wanajua wapi wateja wao wanapatikana hivyo ni ngum kumpangia sehem ambao anajua hakuna biashara.

Simaanishi kwamba natetea kazi ya umachinga bali namtete wamachinga mwenyewe, mazingira yetu pamoja na uchumi wa nchi kwa ujumla. Sote tunajua kwamba hizo bidha zinazo tembezwa na wamachinga wa Tanzania zimetengezwa ulaya na asia sasa kwanini serili ya Tanzania wanaruhusu bidhaza hizo kiholela bila kumwandaa muzaji mumachinga na mazingira yake?

Lengo na dhumuni la kuleta bidha hizo ziuzwa nchini ni kuongeza pato la taifa lakini lazima wauzaji wenyewe na wafanya bishara wenyewe waelimishwe kwanza. Sio kama hivi sasa wabafanya biashara wetu wakubwa ni hao wamachinga ambao hawana elimu ya biashara wala ya kutunza mazingira na nivyo jua mimi kutunza mazingira ni kitu cha mhim sana kuliko vyote. Tunajionea kwa macho yetu jinsi vijana wenzetu wanavyo teseka juani kutwa nzima huku warab na wenzao wapo kifulini kusubiri wamachinga walete pesa bila kuwapatia angalau elimu kutotupa matakataka kila mahali kama hivi sasa wakati bidha hizo wameleta wao.