Showing posts with label Infectious disease. Show all posts
Showing posts with label Infectious disease. Show all posts

Monday, August 06, 2012

Ebola Virus Umeingia Tanzania - Taarifa Maalum!

Wahudumu Maalum wa Mortuary Uganda wakienda kumzika mtu aliyekufa kwa ugonjwa wa Ebola

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUWEPO KWA MGONJWA WA EBOLA, WILAYA YA KARAGWE MKOA WA KAGERA, TANZANIA 

Utangulizi

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma, kuhusu tetesi zilizokuwa zimeenea hapa nchini kutoka kwenye vyombo mbali mbali vya habari kuhusu kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola,wilayani Karagwe mkoa wa  Kagera.

Mnamo tarehe 3 Agosti 2012, Wizara ya Afya na Ustawi Wa Jamii ilipokea taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe ya kuwepo kwa mgonjwa aliyekuwa anahisiwa kuwa na dalili za ugonjwa wa Ebola, katika hospitali ya  Wilaya ya Nyakahanga.

Aidha,taarifa hiyo ilibainisha kuwa mgonjwa huyo alikuwa ni mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (6|)  kutoka katika kijiji cha Nyakatundu wilayani Karagwe. Mgonjwa huyu alikuwa na dalili za homa kali, kulegea, kutokwa damu puani, kutapika damu,  na kukojoa damu.

Maelezo kutoka kwa mama mzazi zilieleza kuwa mtoto huyu alianza kuugua kuanzia tarehe 30 Agosti 2012, ambapo alipatiwa dawa ya Septrin baada ya hospitali binafsi kuonyesha kuwa ana  ugonjwa wa“Typhoid”.

Uchunguzi wa awali katika hospitali ya Nyakahanga ulionyesha kuwa mtoto huyu  alikuwa anasumbuliwa na uambukizo kwenye haja ndogo (Urinary Tract Infection).Vile vile alifanyiwa uchunguzi wa kimaabara na Vipimo vya malaria, Hepatitis na Typhoid havikuonyesha kuwepo  kwa magonjwa haya. Hospitali inaendelea kumpatia matibabu mtoto huyu na imewaweka mgonjwa na mama yake anayemtunza kwenye chumba maalum (Isolatiom room) kwa ajili ya uangalizi zaidi.

Aidha mnamo tarehe 4 Agosti 2012, timu za wataalamu kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Kagera imeweza kufika na kumfanyia uchunguzi wa kina pamoja na kuchukua sampuli za damu kwa ajili ya uchunguzi zaidi katika maabara ya Taifa ya uchunguzi wa magonjwa na Maabara za nje ya nchi, ili kubaini kama ameathirika na ugonjwa wa Ebola.

Timu hiyo ya wataalamu imetoa taarifa kuwa hali ya mgonjwa huyu kwa sasa imeimarika ikiwa pamoja na kutokuwa na homa, kutapika na kukojoa damu kumekoma pia, uchunguzi uliofanywa kwa mama wa mtoto umeonyesha kuwa hana dalili zozote za ugonjwa wa Ebola.Vile vile hakuna taarifa ya mtu mwingine yeyote kwenye familia hiyo au kwenye maeneo ya kijiji hicho au cha jirani kuwa na dalili za ugonjwa huo.

Kufuatia taarifa hii, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Mkoa wa Kagera imechukua hatua zifuatazo;

  • Imepeleka timu ya wataalamu mbali mbali kutoka Wizarani na mkoa  kwa lengo la kwenda kufuatilia na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa huo. 
  • Imetoa elimu ya Afya kuhusu njia za kuzuia kuenea ugonjwa wa Ebola  pamoja na dalili za ugonjwa huu, kwa wananchi na watumishi wa afya katika hospitali ya Nyakahanga
  • Kupeleka vifaa kinga katika hospitali ya Nyakahanga pamoja na maeneo ya mipakani
  • Kutoa matangazo kwa jamii kwa kutumia vipaaza sauti na kupitia  radioni (Radio Karagwe) kuhusu ugonjwa huu.  Aidha, vipeperushi pia vimetolewa.

Hitimisho

Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa mpaka sasa hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola hapa nchini.Aidha, Wizara ya Afya imejiaanda kikamilifu kukabiliana na ugonjwa huu iwapo utatokea hapa nchini.

Kwa sasa timu za wataalum  zipo katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro na Arusha, kutoa elimu juu ya ugonjwa huu kwa wataalamu na kwa wananchi na vilevile kufuatilia ugonjwa huu sehemu za mipakani.

Wizara inaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa haraka kwenye kituo chochote cha kutolea huduma za afya, mara wanapoona dalili za ugonjwa huu.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano,
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,

Tarehe 6 Agosti, 2012.

Friday, July 06, 2012

Ugonjwa wa Ajabu Yaua Watoto Cambodia!

Kuna habari kutoka World Health Organization (WHO) kuwa watoto wengi nchini Cambodia wamekufa kwa ugonjwa wa ajabu. Ugonjwa huo unaathiri mishipa ya fahamu na mapafu. Wadau, tuombe huo ugonjwa wa ajabu usiingie barani Afrika. Watoto wetu watakwisha!

*********************************************************************
Kutoka CNN.com

http://www.cnn.com/2012/07/06/world/asia/cambodia-children-disease/index.html?hpt=hp_t2

Hong Kong (CNN) -- The World Health Organization (WHO) and Cambodian health officials are investigating why at least 61 children in the country have died mysteriously after suffering severe neurological and respiratory complications.


Dr. Beat Richner, of the Kantha Bopha Children's Hospitals who first alerted Cambodia's health authorities about the unknown disease said as of Friday, he knew of 64 cases, in which only two children have survived.

Countries surrounding Cambodia were informed of a deadly disease that killed dozens of children earlier this week, through the International Health Regulations event information system, which provides public health communications.

In Hong Kong, a major air hub in the region, health officials responded by alerting doctors to be watchful for patients returning from Cambodia who have respiratory symptoms. Travelers who have been to Cambodia were told to visit their doctors if they developed respiratory symptoms.

Kwa habari kamili BOFYA HAPA:

Wednesday, June 06, 2012

Kisonono Kisichotibika Unasambaa Duniani

Wadau,  kuna taarifa kuwa kuna aina mpya ya Kisonono kisichotibika unayoambaa duniani.  Zamani ilikuwa ukiambukizwa unachoma sindano ya PPF (Penicillin) gonjwa kwisha!  Sasa hizo sindano wala antibiotics za aina yotote hazitibu! 

Si itakuwa balaa ugonjwa huo ukiingia barani Afrika.  Kwanza waafrika wengi hawapendi kutumia kondomu. Wanataka mavituuz  (ngono) yao kavu au nyama kwa nyama!  Halafu wanaume wengine Afrika hawawezi kulala bila kupata vituuz! Ume ukisimama ubongo unahamia hapo.

Wadau fanyeni ngono kwa usalamaili tuepuke ugonjwa huo balaa.

********************************************

WHO: Sexually-transmitted superbug could be major crisis


A major public health crisis is emerging, in the form of a sexually-transmitted disease that doesn't respond to antibiotics, World Health Organization officials said Wednesday.

Gonorrhea is one of the most common sexually-transmitted infections. It is spread through oral, vaginal and anal sex. About 106 million people worldwide become infected every year.

"Once this organism develops full resistance to this last antibiotic that we have, we have nothing else to offer to these patients," says Dr. Manjula Lusti-Narasimhan, scientist at the Department of Reproductive Health and Research at WHO.

The organization has just released a global action plan encouraging greater awareness and advocacy, research, increased prevention efforts and monitoring of gonorrhea treatment failure. The same sorts of prevention messages apply for gonorrhea as for HIV/AIDS: Practice safe sex - correct and consistent use of condoms - and limit the number of sexual partners.

Australia, France, Japan, Norway, Sweden and the United Kingdom are among the countries reporting cases of gonorrhea that does not respond to cephalosporin antibiotics, which is the last treatment option against gonorrhea. These are developed countries with good health care systems, meaning countries less well off may be even more at risk for a crisis.

KUSOMA TAARIFA KAMILI BOFYA HAPA:

Friday, April 20, 2012

Vote and Help Tanzanian Children

Da Subi Ameleta taarifa hii:

Your vote will make a big difference to Tanzanian Children Dr. Nahya Salim of IHI, has applied for research grant. Kindly vote for her. Your votes counts a lot for her to be considered for this research grant. The more the votes the higher the chances. Lets join hands to support our fellow scientist. To do this follow the following steps: (and thank you for your vote!)

1. Click the link applications.grandchallenges.ca and choose rising stars for Global health (NOT Canadian stars)
2. Click on "LOGIN" and then "create new account" to register
3. Enter your details with your email address and passwords, go to your email inbox, find the automatic mail by grand challenge award administration, open it and click the long link provided and log in.
4. You will find many video with pictures, look for a video with title, "Every breath count; The role of standard case management of pneumonia in reducing overall child morbidity"
5. Click on presentation and go to "like this application" and click to thumb up for pneumonia. Log out and you are done. Remember your vote will make a big difference to Tanzanian Children. Lets start now lets do it! Thank you again, Dr. Nahya Salim MD, MMED (Paediatrics and Child Health Specialist)

Subi| wavuti.com

Tuesday, August 04, 2009

Ugonjwa wa Tauni (Plague) Yaikumba China!

Wadau, kuna ugonjwa hatari, tauni (pneumonic plague) ambayo umeuikumba sehemu fulani huko China. Huo ugonjwa ina mtu katika masaa 24 tu! Mgonjwa anaumwa kichwa, anaona shida kupumua, anajisikia mchovu na kukohoa damu!!!! SYMPTOMS/DALILI

Tuwe waangalifu. Tuombe Mungu uishie huko huko na hasa isifike bara Afrika!

Kwa habari zaidi someni:

http://latimesblogs.latimes.com/booster_shots/2009/08/pneumonic-plague-los-angeles-.html

http://ftalphaville.ft.com/blog/2009/08/04/65266/saying-boo-to-the-flu-and-the-plague/

*****************************************
What is pneumonic plague? Disease outbreak in China is similar to bubonic plague, highly contagious

BY Rosemary Black DAILY NEWS STAFF WRITER
Tuesday, August 4th 2009, 12:35 PM

The rare but deadly form of plague that has reportedly killed two victims in northwest China and caused authorities to seal off a town of 10,000 is treatable with antibiotics - but only if it's caught very early.

Pneumonic plague, which afflicts the lungs, is caused by the same bacteria responsible for bubonic plague, a less serious form of illness that is transmitted by certain fleas.

Read the whole story HERE: http://www.nydailynews.com/lifestyle/health/2009/08/04/2009-08-04_what_is_pneumonic_plague_disease_outbreak_in_china_is_similar_to_bubonic_plague_.html