Saturday, June 22, 2013

Mwanafunzi wa UDSM Auwawa na MajambaziMwanafunzi mmoja kati ya wanafunzi wanne wa mwaka wa IV wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kampasi ya Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo katika eneo la Yombo la Chuoni hapo. 
 
Inataarifiwa kuwa waanafunzi hao walikuwa wanajisomea na kuandaa “dissertation” zao kwa mwaka wao wa mwisho wa masomo, na ghafla wakavamiwa na watu waliowaamuru watoe kompyuta zao na pochi za fedha. Wanafunzi hao walikubali shuruti hiyo lakini mmoja wa wanafunzi alipoomba walao wachukue nakala ya documents zao kutoka kwenye computer hizo, ndipo mmoja wa majambazi hayo alipomoiga risasi ya tumbo mwanafunzi huyo, ambaye alianguka chini.

Imeelezwa kuwa wanafunzi wengine kuona hivyo waliwasiliana na uongozi wa Chuo kuomba gari la kumwahisha mwenzao Hospitalini.
Taarifa zaidi za hali ya majeruhi huyo bado hazijawekwa bayana.

Kwa siku za hivi karibuni kumekuwa na matukio ya kuwavamia wanafunzi vyuoni kwa nia ya kuwapora ama kuwabaka, jambo ambalo limewaacha wengi wakiwa na hofu juu ya usalama wao, baada ya wenzao kupoteza vifaa vyao ama kujeruhiwa na wengine wakipoteza uhai.

Baadhi ya matukio haya yameripotiwa na wanafunzi kuandamana katika vyuo vya St John's Dodoma, IFM Dar, Uhasibu Arusha na sasa Mlimani, Dar.

Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2WrTyqTKa

No comments: