Thursday, November 15, 2007

Enzi za Mjerumani Tanganyika 1885-1918

Hii picha ilipigwa 1903. Sijui ni shule gani Dar. Je, ni shule ya Uhuru? Hakuna msichana hata moja darasani!
Mjerumani alivyowakuta mabibi na mababu zetu.

Hii picha ilipigwa 1910. Hotel zu Stadt - Sijui ilikuwa mtaa gani Dar?

Nani kasema Mjerumani mbaguzi! Huyo njemba alifanikiwa kwenda Ujerumani na kujiunga na jeshi lao huko huko!

Waafrika walikuwa wanabeba wazungu bila wasiwasi. Wazungu hawakupenda punda kwa sababu walikuwa wana jamba ovyo.

Kabla ya King's African Rifles (Mwingereza) kulikuwa na German Native Infantry (Mjerumani). Hao native infantry walipgana katika vitu kuu ya dunia ya kwanza (World War I).

Kwa habari na picha zaidi someni:

http://germanhistorydocs.ghi-dc.org/sub_image.cfm?image_id=1433&language=english

6 comments:

Anonymous said...

Dada Chemi haujamaliza

"Kwa habari na picha zaidi someni:"...

Anonymous said...

Chemi umenimaliza, mbavu mie sina, nimecheka nikilia maana hiyo 'comment' ya punda ni balaa!

Nimemuvuzisha 'link' kwa jeremani hapa najua nitanuniwa wiki

big up sis

Anonymous said...

aisee hii kali. lakini utumwa uliopo sasa east Africa ni mbaya kuliko huu wa jeremani, sijui kizazi kijacho cha wajukuu zetu watakuwa na yapi ya kusema. .....anyway

Anonymous said...

Tumetoka mbali! Hao waliokuwa wanabeba wazungu walikuwa hawajambi? Wazungu kwa starehe bwana!

Mashombe wangapi walikuwa conceived kwenye ile hoteli?

Anonymous said...

Chemi kweli hujui umenifurahishaje, mimi ni German Trained Engineer, nina very strong ties na Ujerumani... To make things good Babu yangu alikwa askari wa ajerumani alipigana vita vyote I-II... Kwa kunipa uhondo zaidi huyo askari mweusi anafanana naye...! Aisee sijui nikupe nini dada Chemi? Hapa nilipo naaza kuifanyia kazi na kama nita prove kuwa ni yeye basi nitakualika rasmi kwenye sherehe na Wajerumani.. Mengi zaidi tutawasiliana nami niko Ughaibuni... Nitakupa mawasiliano yangu next time... Aisee I am excited to the extent nasema UBARIKIWE NA MTANDAO uzidi kuturahisishia kazi. Thanks Mdau

Chemi Che-Mponda said...

Asanteni wote kwa comments zenu. Anony wa 7:40pm I hope utafanikiwa. Best wishes. Na ukinialika nitajitahidi kufika. Pia nimepata moyo wa kufanya Tanganyika Part II. Kutokana na feedback nayopata watu wamefurahia kweli hiyo posti ya Tanganyika.