Tuesday, March 18, 2008

Dada Ummie Mafoudha Alley Hamid


Picha kutoka Michuzi blog
Kulia mwa rais Kikwete ni Dada Ummie Mafoudha Alley Hamid. Aliapishwa jana kuwa makamu mwenyekiti wa tume ya haki za binadamu na utawala bora (Tanzania Commission for Human Rights and Good Governance) . Mh. jaji Amiri Manento (kushoto), ni wenyekiti. Makamishna wa tume ni mh. Joaquine De Mello, mh. Zahoro Juma Khamis na mh. Bernadeta Gambishi.

Dada Ummie ni mwanachama wa TAMWA wa siku nyingi sana. Na amefanya mengi kuinua haki za akina mama Tanzania hasa Zanzibar.

Honger Dada Ummie!

5 comments:

Anonymous said...

Wanawake wa TAMWA yaani kila kiongozi wa kike ana uhusiano na TAMWA.

Anonymous said...

Hongera Dada Ummie, Mwenyezi Mungu akujaalie mafanikio katika kazi yako mpaya. Ameen.

Anonymous said...

Anonymous wa March 18 6.12 PM.
Mbona wapo viongozi wanawake tele ambao hawapo TAMWA?

Anonymous said...

Nafikiri umuombe msamaha huyu jamaa wa kulia mwa Kikwete. Sidhani kama kulia kwa Kikwete ni mwanamke...

Anonymous said...

Haya Umi katetee haki za wale walioacha nje baada ya kuvunjiwa nyumba zao, wakipatiwa viwanja vipya na wakalipwa pesa ili wakaanze ujenzi ndio mimi nitakupongeza kwa kazi yako. Kila la kheri!