Tuesday, March 11, 2008

Marekani warahisisha process ya kuomba Visa Dar

Hivi huyo rais Bush kapewa nini alivyokuwa Tanzania? Ngojeni mtaona wimbi la watu kutoka nchi zingine za Afrika wakifika Dar kuomba visa za USA sasa!

*************************************************************************
Kutoka ippmedia.com

Ule msoto visa za Marekani sasa basi!

2008-03-11

Na Mwandishi Wetu, Jijini

Ubalozi wa Marekani nchini umetangaza hatua kadhaa zilizochukuliwa kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa viza za kuingia nchini humo na kupunguza kero iliyokuwa ikiwakabili watu wanaotaka kibali cha kuingia Marekani.

Mkuu wa Idara ya Uhamiaji kwenye Ubalozi wa Marekani, Bw. Robert Hannan amesema hatua hizo ni pamoja na kuwekwa kwa muda mfupi wa kungoja usaili ambapo alisema katika kipindi cha miezi 18 iliyopita, wasafiri watarajiwa wamekuwa wakipangiwa muda wa kusailiwa ndani ya siku mbili.

Kadhalaika alisema kupanga muda wa kusailiwa kupitia mtandao kumesaidia ambapo waombaji wa viza wamekuwa wakipanga muda wa kusailiwa moja kwa moja kupitia mtandao. Alisema kabla ya hapo, waombaji walilazimika kuchukua muda wa kusailiwa uliokuwa unafuata, bila kujali usumbufu waliokuwa wanaupata. `

`Hivi sasa, waombaji wanaweza kuchagua tarehe na saa inayowafaa. Taarifa zaidi zinapatikana kwenye tovuti ya Ubalozi wa Marekani: www.tanzania.usembassy.gov`` akasema.

Kuhusu viza za muda mrefu, Bw. Hannan alisema Serikali ya Tanzania, chini ya maagizo ya Mkurugenzi wa Uhamiaji, Bwana Kinemo Kihomano, imefikia makubaliano na Marekani kwa nchi zote mbili kuongeza muda wa viza kutumika, kutoka miezi 3 mpaka mwaka mmoja.

``Kwa hivi sasa, watu wanaofanya safari nyingi watahitaji kuomba viza mara chache zaidi,`` akasema. Kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo, Bw. Hannan alisema maombi ya ``dharura`` ya kufanyiwa usaili kwa safari za haraka limekuwa tatizo kubwa kwao.

``Kwa kawaida, hakuna sababu nzuri kwa maombi kama hayo,`` alisema Hannan. ``Kama wasafiri watarajiwa wanajua kuwa wanaenda kuhudhuria mahafali mwezi wa Juni, au kushiriki mkutano mwezi wa Septemba, wanaweza kuomba viza sasa hivi.

Kupitia utaratibu wa viza ya muda mrefu ulioanza kutumika mwezi wa Novemba mwaka jana, waombaji sasa wanaweza kupata viza watakayoitumia kwa kipindi cha mwaka mzima.

`` Hannan aliongezea kuwa, viza zote za Marekani kwa shughuli za utalii, biashara, na masomo, ni viza za kutumiwa zaidi ya mara moja - zinaruhusu mtu kufanya safari nyingi katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.

SOURCE: Alasiri

2 comments:

Anonymous said...

Nitawaambia wadogo zangu waombe visa! Tuone kama watapata! Walishanyimwa!

Anonymous said...

waaache wadogo zako wakae Tanzania,haya sio maisha.