Saturday, March 22, 2008

Katumwa!!!!

Samaki aina ya Sting Ray aliyoua!

Huyo mdudu/samaki pichani (Sting Ray) kamwua mwanamke Florida siku ya Jumatano wiki hii. Kwa maelezo ya familia yake, Judy Kay Zagorski, 55, alikuwa anaota jua kwenye boti yao. Ghafla huyo mdudu katokea majini na kuruka kwenye boti na kumgonga huyo mama aliyekuwa anaota jua. Yule mama alikufa papo hapo. Ni ajali ya ajabu.

Na huko Bongo lazima watu wangesema, "KATUMWA!" Watasema lazima alimkera mtu fulani, au kamkosea mtu au mtu kamwonea wivu, hivyo walitambika na kumtuma huyo mdudu kwenda kumtoa roho huyo mama.

Mwaka jana, samaki kama huyo alimwua yule mtaalam wa wanyama, Steve Irwin, wa kumchoma kwenye moyo akiwa anaogelea baharini.
Kwa habari zaidi someni:

3 comments:

Anonymous said...

Na kweli katumwa hiyo!

Anonymous said...

Kweli tuna amaini uchawi. Tunaweza kusema ni kweli katumwa.

Anonymous said...

Kwanini unakuwa na mawazo duni na wabongo namna hiyo, kwanini hudhani kwamba watachukulia kama wao huko walivyolipokea. Tusiwe tunajifikiria tupo chini sana kimawazo namna hiyo. Ukombozi wa kifikra huanzia kwa kujiamini kwanza na namna yetu ya kufikiri na jinsi kutathmini mambo!. Ni mtizamo wangu!