Monday, March 10, 2008

Bongo E Harmony/ Great Expectations


Wadau, nimekuta hii posti kwa kaka Michuzi. Sasa nimeshindwa kujua kama huyo mtu yuko serious au ni utani. Mnasemaje? Inanikumbusha maombi ya watu wanaotafyta wapenzi kwenye E Harmony na Great Expectations Dating.


*********************************************************************************

HABARI ZA LEO WADAU,


NATAGEMEA MMEKULA WEEKEND YENU VIZURINAOMBA NITUMIE BLOG YAKO KUWEKA OMBI LANGU. MIMI NI MSICHANA WA MIAKA 28 NIMEZALIWA NA KUKULIA KATIKA JIJI LA KANDORO(DAR) KABILA LANGU NI MCHAGGA , NI MTOTO WA MWISHO KATIKA FAMILIA YETU NINA DADA WAWILI WOTE WANAISHI NA FAMILIA ZAO.

HISTORIA YANGU KWA FUPI:NILISOMA ELIMU YANGU YA MSINGI NA SECONDARY INTERNATIONAL SCHOOL OF TANGANYIKA, BAADA YA HAPO NILIFANIKIWA KWENDA ELIMU YA JUU OSLO UNIVERSITY COLLEGE (M Eng)SASA HIVI MIMI NI ACHITECT & BUILDER NAISHI DAR ES SALAAM LAKINI SINA STATION MAALUM NA SAFIRI SANA KIKAZI NDANI NA NJE YA NCHI NATEGEMEA KUFANYA PHD MIAKA YA BAADAE.

NIMESHAWAHI KUWA NA RAFIKI MMOJA WA KIUME LAKINI MUNGU AKUPANGA TULIACHANA BAADA YA MIAKA MIWILI (TULIKUWA NA MITAZAMO YA MAISHA TOFAUTI)ILA NI MARAFIKI TU.NADHANI MPAKA HAPO A SUCCESSFUL CANDIDATE ATAKUWA AMENIELEWE.

SIFA ZA MLENGWA KUAMBATANISHA CV YAKE IKIELEZA,SIFA MUHIMU ZIFUATAVYO:


1.MINIMUM QUALIFICATION 1ST DEGREE GRADUATE

2.AWE MUAJIRIWA/KUJIAJIRI

3.AWE MSAFI(ATLEAST ORGANISED),KUPANGILIA MAVAZI

4.SURA INATEGEMEA LAKINI SIO MUHIMU SANA

5.SENSE OF HUMOUR

6.AWEZE KUONGEA KIINGEREZA(BILA IAMMMM NYINGI )HII NI KUTOKA NA WAGENI NINAO WAPATA NYUMBANI KWANGU NISINGEPENDA KUMFANYA AWE LEFT OUT

7.UREFU NI MUHIMU KIMO CHA CHINI KABISA KIWE 5.9FT KWASABABU MIMI MWENYEWE NI 5.9FT

8.AWE ANAVAA KIATU SIO CHINI YA SIZE 9(SIO MUHIMU SANA ILA NINGEPENDA IWE HIVYO)

9.SIO LAZIMA AWE MCHAGGA

10.AWE HAJAWAI KUOA AU KUWA NA MTOTO/WATOTO

11.KUPIMA UKIMWI MUHIMU KABLA YA KUKUTANA (KIMAPENZI)

12.ASIWE MVUTA BANGI/KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA YA AINA YOYOTE

13.(ACADEMIC CERTIFICATE)VIAMBATANISHO(VIVULI) VYA VYETI NIMUHIMU ILI NIWEZE KUPIMA IQ YAKO

14.KUWA NA NYUMBA SIO MUHIMU(MIMI NAISHI KWANGU-NYUMBA YA WAZAZI) ILA GARI NI MUHIMU. MWANZO UNAWEZA KUTUMIA LA KWANGU WAKATI TUNATAFUTA JINGINE

15.ASIWE NA UMRI ZAIDI YA MIAKA 35

16.WATU WENYE UZITO WA KHALI YA JUU SANA HAWATA ZINGATIWA ,VITAMBI( BEER BELLY FAT)

17.SITAKI MTU MAARUFU(MACHO YA WENGI)

18.ASIWE ANAVAA HERENI SIKIONI. NO TATTOO. KUSUKA NYWELE, NO GRILLS

NATEGEMEA MAOMBI YANGU YATAELEWEKA NA NITAZINGATIA NO TIME WASTERS.

Asanteni Manka S Mushimankasolomon@yahoo.com

7 comments:

Anonymous said...

Ambaye atamjibu ni mwehu naye.

Anonymous said...

mwenyewe amejielezea kwani kuna ubaya gani

Anonymous said...

Huyo Dada ni mento. Ukute ni mwanaume aliyeandikia upuuzi huo!

Anonymous said...

Ameshasema no time wasters...kwa hiyo mnachosema ni moja kati ya matarajio ya mwandikaji/mwandishi...haijalishi...kama utamtukana au kujinadi na wewe na sera zako...kwani chochote utakachojibu hicho kinatuambia juu yako wewe na mtazamo wako kwenye hoja na upembuzi juu ya sanjari hizi... Binafsi naona, kuna ukweli fulani kwamba sisi wasichana mara nyingine huwa tunajisikia kufanya hivyo/kujinadi kihivyo lakini kunakuwaga na vikwazo ambavyo ni vitu kama staha tulizonazo, mila, desturi na tamaduni zetu tulizokulia hazikutupa vichocheo vya kuwa wa wawazi na wenye kujieleza hisia zetu hata tukasaidika; na hapo ndipo penye kwazo. Hivyo kama mwombaji (mwandishi) mtoa ombi ni mwanamme au mvulana ...ni nafasi ya mwengine pia kuliangalia kwa kina swala hilo...kwani kwa namna fulani limekuja kama hoja... ambayo shurti ihojoliwe. Asanteni shanGwe mwanGani

Anonymous said...

Dada Manka nadhani amesahau 1) kabati ya mbeho 2) Redio ya picha na 3) toyota stout ya kubeba majani ya ng'ombe. Haya dada yangu kaza buti, lakini umri ndo unayoyoma hivyo....O hoo!

Anonymous said...

kwa hakika huyo lazima awe ni malaika na si binaadamu. maana kwa binaadamu unaweza uwe na sifa mbili au tatu katika zile zilizotajwa. kuwa nazo zote kamilifu kama Dada Manka alivyoziweka nadhani si rahisi.Hata hivyo, huo ni mtazamo wake, anaweza akapata mtu mwenye sifa zote zile ila ni kazi ngumu

Anonymous said...

Miaka 28 bado ni umri mdogo tu na anaweza kuolewa kama akitulia vizuri ili wanaume watulivu wamuone. Mimi nilipooa sote tulikuwa na miaka 32 na tulifanya uchumba kwa mwaka mmoja, kwa hiyo alikuwa na miaka 31 tulipokutana mara ya kwanza. Sasa tuna miaka 41, watoto 3 na furaha tele. Ushauri wangu tu ni kuwa huyu Manka kama ni mtu wa kweli (i.e kama si hadithi tu ya kufurahisha blog) atulie, watulivu watamuona tu hapo alipo. Hii hadithi aliyotuwekea hapo inataka kuashiria kuwa hata kwenye social circles zake (kazini, kanisani, michezoni, majirani) hana watu kabisa, ama wapo lakini hawamuoni/hawamtaki/hawataki, na mtu yeyote atajiuliza kulikoni? Atakuwa na uhakika gani na mtu asiyemjua anayemtafuta kwenye mtandao? Au pengine hana social circles zozote (na hii ni sababu kubwa ya kukosa mwenzi, hakuna anayetaka kuoa mashine, kitabu, kompyuta nk, tunaoa binadamu mwenzetu wa kushea nae maisha, sasa kama mtu huwa hashei maisha na watu hakika hafai kuoa!). Kwa hiyo namshauri ajiangalie tabia yake na mwenendo wake mbele ya jamii ajirekebishe. Wakati mwingine unaweza kuhisi kuwa ukijirekebisha na kubaki hapo ulipo watu hawataamini umebadilika? Basi unaweza kuhamia sehemu nyingine, ukapanga nyumba (au kununua kama uwezo upo), ukaanza maisha mapya na kujenga social networks ambako watu watakuona na wewe utaona watu, so mtaonana na kuongea huko, utapata mwenzi tu. Na wala hutahitaji kutangaza vigezo vyake hadharani, utaangalia katika hao mnaokutana ni yupi anayefiti na utachukua hatua tu, wewe ndiwe utakayejua kwa nini umemkubali.

Dada Chemi hebu mfikishie Manka huu ushauri wangu kwenye email yake, maana sina uhakika kama anasoma kila kinachowekwa kwenye mtandao, na hasa kwa kuzingatia majibu makali aliyopata kule kwa Michuzi. Nitafurahi kupata feedback. ngalamba@yahoo.com