Friday, February 20, 2009

Maiti Yakutwa Gesti Tabata!

Nadhani huyo jamaa alikuwa 'mule' (mtu anayesafirisha madawa ya kulevya). Kipaketi kilimpasukia tumboni. Rest in Peace.

********************************************************

Kutoka Lukwangule Blog:

Maiti iliyokutwa nyumba ya kulala wageni ya Big Brother iliyopo Tabata, Dar es salaam na fedha kibao za Marekani, Brazil, Kenya na Tanzania ilikuwa na kete 57 ya dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi kanda Maalumu, Suleman Kova aliwaambiawaandishi wa habari leo kuwa mtu huyo ambaye anasadikiwa amekufa kutokana na madhara ya dawa hizo.

Mtu huyo ambaye alijiandikisha kwa jina la Haji Hamis katika gesti hiyo alikuwa na hati ya kusafiria yenye jina la JordanBenedict (33).Inaaminika kuwa mtu huyo ni mfanyabiashara wa mitumba na mkazi wa Kijitonyama.

Maiti hiyo ilipatikana jana baada ya wenye gesti kuwa na mashaka baada ya mgeni wao kutotoka tangu ameingia chumbani mwake na kuwaita polisi.Kova alisema maiti huyo alikutwa amepiga magoti na kuegemea kitanda.

Chumbani kulikuwapo na chupa ya plastiki ya maji, hati ya kusafiria, dawa paketi tatu aina ya dawa za kuongeza nguvu baada ya kuharisha sana na pochi iliyokuwa na fedha za Brazil 2000, Kenya 2000, dola za Marekani 27,000 pamoja na Sh za kitanzania 150,000.

No comments: