Monday, February 09, 2009

Go Kanumba!!!!

Wadau, mcheza sinema maarufu wa Bongo, Steven Kanumba hachoki! Yuko katika harakato za kushuti sinema mpya, Hero of the Church.

HONGERA STEVEN KANUMBA!

*****************************************************************************
Maelezo na picha kutoka Abdallah Mrisho Blog:

Kinara wa filamu za Bongo, Steven Kanumba (shoto), hivi sasa yupo katika shooting ya filamu nyingine mpya ambayo anatarajia kuwashirikisha wasanii wa Africa Mashariki, filamu hiyo itajulikana kwa jina la Hero Of The Church na itaongozwa na Director kutoka Nigeria, Feme Ogodegbe (pichani kulia). kati ni Princess Sheila Mvununje kutoka Uganda ambaye naye atakuwemo kwenye filamu hiyo.
Baadhi ya mastaa wa falamu za Bongo watakaokuwemo ndani ya filamu hiyo ambayo imeanza kurekodiwa jijini Dar. Mnamcheki 'dogo' Ben (kushoto hapo) alivyojazia siku hizi?

Moja ya scene zitakazopatikana kwenye Hero of the Church......yetu macho!

14 comments:

Anonymous said...

DA CHEMI SOI SIRI HIZI MOVIE NI LOW QUALITY ONA IYO BASTOLA ILIVYOSHIKWA NA HUYO KANUMBA REACTION YAKE YAANI KANA KAONYESHEWA KIDOLE,I HATE THEM,SIO KWAMBA SIPENDI VITU VYA NYUMBANI ILA UKWELI NIKIANGALIA DAKIKA TANO TU USINGIZI SIPATI CONCENTRATION.

Anonymous said...

Dah! Sasa huyo dada na bastola vipi tena! Another cheap film. Lakini nampongeza kwa bidii ya kuwa film mill.

Anonymous said...

Kwa nini wabongo wanapenda kupondana? Heh? Namsifu Kanumba kwa juhudi zake za kutengeneza sinema hata kama ni kideo.

Anonymous said...

bastola haikamatwi hivyo. na ni lazima anaelekezewa bastola aonyeshe kuwa na hofu, wasiwasi au kuchanganyikiwa. hiyo bastola utadhani wapo katika rusha roho!!!!! bongo bwana kwani lazima mfanye??

Anonymous said...

hii bastola kama hair dryer !
poooooooor !

Anonymous said...

ANAJITAHIDI. AMELETA MGANDA NA MNIGERIA. MAENDELEO!

Anonymous said...

Ameshika bastola sasa huo mkono wa kushoto kifuani wa nini??Dada Chemi nakuomba uwape tips ili wajaribu kutengeneza filamu nzuri.Sound poor milio ya ajabu ajabu na mtiririko wa story ni very poor.

Anonymous said...

Tatizo lao hawasikii! Wanadhani wanajua kila kitu na sinema zao ni Hollywood quality. Kumbe ni kideo tu! Ona wameshindwa hata kumfumdisha huyo binti jinsi ya kushika bastola!

Maggie said...

Comments nyigi zinazotolewa hapa naomba zichukuliwe kama constructive comments,nikiwa na maana Watanzania tuwe tayari kukosolewa. In my opinion nawapongeza Watanzania kupiga hatua mpaka kufikia hatua hii katika ulimwengu wa filamu however bado safari ni ndefu, casting director anahitaji shule bado, kilakitu kuanzia title za movie, story yenyewe, lighting,na cast nzima kwakweli bado zinahitaji kazi sio mchezo.
Ninaamini wako waigizaji wazuri tu kuliko huyo Kanumba, hivi auditions za waigizaji zinafanyikaje huko bongo jamani? sio kila sinema Kanumba Kanumba, sura zile zile kila siku, realistically hizi sio films bali ni soaps(kama Isidingo etc, hizo ndio cast wanajirudiarudia kila siku na maneno ni mengi kuliko actions), acting sio lelemama, ushahidi huo hapo kwenye hiyo picha, hizo sura sio za actors wazuri, naomba hiyo bongowood ikubali kukosolewa na kuanza kufanya mambo kimataifa kidogo sio kubabaisha babaisha, othrrwise hakuna film industry hapo ila ni biashara tu kama biashara nyingine.
Napenda pia kumpongeza Kibira, yeye ni mfano wa kuigwa!!
Again this is just my opinion!!!

Anonymous said...

Kwa kweli hata mimi nimebaki kutabasamu mwenyewe nilipoona huyo dada na bastola yake! Jamani, who assist these people? Ni vitu vidogo, lakini kila mwenye jicho anaona kuna mapungufu.....ushikaji wa bastola is one thing, halafu mkono mwingine says something else, ambavyo ukiviunganisha kwa pamoja, they don't make sense...

Anonymous said...

magdalena, you have a point there! tatizo la watengeneza filamu wetu wa Bongo ni kudhani kuwa sura ndio zinafanya picha ikubalike!! ndio maana sasa tunashuhudia mlolongo wa Mamiss,Wanamuziki,wacheza mpira nk, wakiekti kwenye sinema potelea mbali kwamba hawajawahi hata kucheza michezo ya kuigiza ama kuimba kwaya walipokuwa shule za msingi!! Hili la kila sinema mpya kuwa na sura zile zile nalo pia linaboa!

Anonymous said...

Mtume!Haya huyo dada kashika bastola vibaya lakini mbona Kanumba hana reaction kwa bastola usoni kwake?

Anonymous said...

loooooooo aibu tupuuu

Anonymous said...

Kanumba jifunza kuwa professional. Hii sasa kama mchezo wa kuigiza wa primary school.