Nilipiga picha hii nikiwa kwenye ferry. Anguilla haina milima mirefu! Kutoka angani inaonekana fleti kama imepigwa pasi.
Ukihitaji maji unaletewa. Ukitaka tanki nzima ni dola $500! Watu wengi wanakinga maji ya mvua.
Mbuzi wa Anguilla ( Waingereza waliabika mwaka 1969 walipovamia Anguilla na kukutana wa wafuga mbuzi badala ya wapiganaji)
Mzungu akijipika juani! Wazungu huko wameungua na jua, wengine wekenduuu! Kwa nini wanataka kuwa weusi halafu wanadharau watu weusi?
Anguilla Health Authority
Huyo Rasta Man anamtungia huyo Bi Kizee wimbo hapohapo. Huyo Bi Kizee anaitwa Nancy na ilikuwa party ya kusherekea Birthday yake....ana miaka 75. Rum punch zilikuwa zimenikolea lakini wimbo ulisema kitu kama, Nancy is so beautiful but she got ugly man.
Usikojoe hadharani!
Barabara za Anguilla ni nzuri hazina mashimo. Kwa vile ni kisiwa kadogo, hakuna barabara enye njia zaidi ya mbili.
Niliamua kuingia kwenye maji, lakini yalikuwa baridiii! Mchanga kwenye beach zao ni mweupe halafu laini kama unga!
Hapa ni Blowing Point Beach
Ndege wa Taifa wa Anguilla ni Turtle Dove
Jogoo akitamba Anguilla
Watoto wa shule huko wanachukuliwa na School Bus, huduma ya school bus inalipiwa na serikali
Nyumba asili ya Anguilla. Nilibishana na watu huko kuhusu hizo nyumba, walisema eti nyumba asili (huts) za waafrika ni ndogo zaidi. Nikwaambia nyumba zao asili ni ndogo kweli!
Nyumba ya James Ronald Webster ambaye anaitwa mkombozi wa Anguilla. Bwana Webster aliongoza mapinduzi huko mwaka 1967. Mwaka 1969 waingereza walipavamia na walipokelewa kwa shangwe na wenyeji.


1 comment:
Asante kwa kutelemisha Da Chemi. Mimi ndo leo nimejifunza kuhusu hiyo nchi hata sikujua kama upo. Naijua Jamaica na Barbados.
Post a Comment