Wednesday, February 25, 2009

Ndege Yanguka Uholanzi!

Wadau, ndege imeanguka huko Amsterdam, Uholanzi. Ilikuwa ndege ya Uturuki. Habari zinasema kuwa watu 9 wamekufa, na zaidi ya 5o wameumia. Ilikuwa imebeba watu 135. Ndege ilikuwa inatoka Uturuki kwenda Uholanzi na ilikuwa katika harakati za kutua kwenye uwanja wa ndege ya Schipol. Abiria waliopona wanasema kuwa wala hawakuonywa kuwa ndege inaanguka. Waliambiwa wafunge mikanda ya viti kwa ajii ya kutua.

Naona ndege zinafululiza kuanguka sasa. Ilianza na ile ya Continental Airlines Flight 1549 iliyoanguka mtoni New York. Watu 50 walikuwa baada ya ndege yao Continental 3407 kuanguka kwenye nyumba huko Buffalo, New York. Na kumekuwa na ajali kadha za ndege ndogo. Hata hapa Massachusetts ndege ndogo ilianguka na kwa bahati mwanamke aliyekuwa anaiendesha alipona na majeraha madogo.

Wadau, yaani wanasema kuwa kusafiri na ndege ni salama kuliko usafiri wa gari. Lakini mimi kila nikipanda kwenye ndege lazima niombe. Na tukitua salama lazima niseme sala ya shukurani.

Mungu alaze roho ya waliopoteza maisha yao katika hiyo ajali mahala pema mbinguni. Amen.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.telegraph.co.uk/news/worldnews/europe/netherlands/4805195/Turkish-Airlines-plane-crashes-at-Schiphol-airport-Amsterdam-at-least-nine-dead.html

http://www.google.com/hostednews/ap/article/ALeqM5g_wBSqw0Ju245UxNtpJZ329K0LJgD96IK4780

2 comments:

Anonymous said...

Kweli ukiingia kwenye ndege ni kuomba! Duh! Hasa hapa kwetu Afrika. Hata mkipona vibaka watawaibia palepale.

Anonymous said...

kuomba inatakiwa kila mahali ulipo unapoenda lazma uombe ulinzi wa Mungu. iwe majini anagani hata barabarani.

Ms GB