Wednesday, October 06, 2010

Spike Lee Boston University Leo


Watu wakisubiri kupata autograph ya Spike Lee

Leo nilienda Boston University kumsikiliza Muongoza Sinema/Mcheza Sinema Spike Lee akiongea kuhusu jinsi alivyokuwa na mafanikio katika sinema Hollywood. Alialikwa na mwanafunzi mweusi ambaye anasoma filamu hapo chuoni. Alivyokubali mwaliko Chuo waliamua kudhamini safari ya Spike.
Wanafunzi wa BU na watu kutoka jamii ya sinema hapa Boston karibu 800 walihudhuria. Ukumbi ulijaa.

Spike aliongea kuhusu jinsi sinema inavyotawala fikra za watu. Alisema lazima uwe mwangalifu unaleta picha gani. Mfano, watu wanaweza kudhani weusi wote ni maskini, wauaji na watumia madawa ya kulevya na wanawake weusi wote wanagawa mavituuz ovyo kutokana na vitu walivyoona kwenye sinema. Alisimulia mkasa wa weusi fulani walioenda Ulaya na kukuta watu walidhani wao wako hivyo kutokana na mambo walioona kwenye sinema.

Alizungumzia jinisi ilivyo ngumu kwa Hollywood kutoa hela kutengeneza sinema inayoleta picha nzuri kuhusu weusi maana hizo picha zinazoleta picha mbaya zinalipa zaidi.

Spike alisema kuwa hivi karibuni ataanza kutengeneza sinema nyingine. Hakusema itahusu nini lakini ametunga yeye mwenyewe.

5 comments:

Mbele said...

Shukrani kwa ripoti hii nzuri. Mawaidha hayo ya Spike Lee uliyotuletea ni sahihi kabisa.

Anonymous said...

Ni kweli watazamani au mashabiki wanapenda kununua aina fulani ya picha, eti kwasababu inavutia, hata kama haina ukweli.
Kwa mfano hapa Tanzania kuna wagombea wengi, lakini kila gazeti sasa hivi kwenye ukurasa wa mbele wanavitangaza vyama viwili, eti sababu ndio inavutia wateja!

emu-three said...

Ni kweli watazamani au mashabiki wanapenda kununua aina fulani ya picha, eti kwasababu inavutia, hata kama haina ukweli.
Kwa mfano hapa Tanzania kuna wagombea wengi, lakini kila gazeti sasa hivi kwenye ukurasa wa mbele wanavitangaza vyama viwili, eti sababu ndio inavutia wateja!

Simon Kitururu said...

Napenda sana kazi za Spike Lee ila kuna wakati nahisi anatumia sana kupitakiasi race card katika issues.

Anonymous said...

Ni bahati mbaya mara nying rangi nyeusi imehusishwa na ubaya. Hivyo sisi weusi tunakazi kubwa sana kubreak hiyo colour barrier. Mara nyingine hata mafanikio ya kweli utaambiwa umebebwa.
Changamoto anayoitoa Spike ni kuwa tukaze buti iko siku mambo yatakuwa sawa.
Ni juzi tu nimeona tangazo ambalo rangi nyeusi inatukuzwa kuonyesha mwongezeko na kukua kwenye taasisi za fedha.