Saturday, January 15, 2011

Bibi Mississippi Winn Afariki Dunia. Alikuwa na Miaka 113!

(Pichani Hayati Bibi Mississippi Winn)

Bi Kizee Mississippi Winn amefariki dunia huko Louisiana akiwa na umri wa miaka 113. Unajiuliza ni nani? Ni bibi aliyekuwa na umri mkubwa kuliko waMarekani weusi wote. Hakuolewa wala kuzaa mtoto katika maisha yake marefu. Alipenda kusema "Nitaondoka dunia hii siku Mungu Akipenda"

Wazazi wake walizaliwa katika utumwa Marekani amabayo uliisha mwaka 1864. Ajabu, Bibi Winn alikuwa na akili zake na afya njema hadi hivi karibuni. Hivi Tanzania si kuna wazee wenye umri mkubwa pia? Tungewapa heshima na kuwatuza kama wanavyofanya hapa USA.

Kwa habari zaidi someni:


REST IN ETERNAL PEACE

Kwa habari zaidi someni:

http://www.google.com/hostednews/ap/article/ALeqM5iBdLIQRxQqEghsDu8536YKOuQjBg?docId=fc753d0075d240bba11838be6f5dc9a6


http://www.miamiherald.com/2011/01/15/2017207/group-oldest-living-african-american.html

No comments: