Thursday, January 27, 2011

Hii Winter ni Mbaya Mno!


Wadau, sijui huko ulipo lakini hapa Boston tunapigwa na theluji (snow) si kawaida. Sasa hatuna pa kuiweka. Wanasema kuwa snow ya mwaka huu itaingia katika vitabu vya historia. Sasa watu wanatania na kusema kuwa hali ikiendelea kama ilivyo sasa itakuwa kama wale wanaodesha magari yao pichani! Kama snow ingekuwa inayeyuka kabla ya nyingine kuanguka hali isingekuwa mbaya. Lakini sasa kuna milima ya snow kila mahala!
Kwa habari zaidi soma:

2 comments:

Malkiory Matiya said...

Poleni. Hapa kwangu nimebandika jinsi miti ilivyolemewa na snow.

Mtanzania Halisi said...

Khaa! Da Chemi, hiyo picha ni kweli au ni mambo ya photoshop?