Monday, January 31, 2011

Mimi na Tonye Patano

(Pichani mimi na mcheza sinema Tonye Patano)

Wadau, jana nilialikwa kwenda kuona mchezo wa kuigiza, RUINED hapo Huntington Theater Boston. Mchezo huo unahusu vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Congo na hasa jinsi wanawake wanavyonyaswa huko.

Stelingi wa mchezo ni Dada Tonye Patano . Ameigiza katika sinema kadhaa na TV shows, kama Weeds, Law and Order SVU, na One Life to Live. Alipoigiza katika sinema, The Company Men, ambayo ilipigwa Boston nilichaguliwa kuwa stand in wake. Kazi ya stand in ni kuwepo pale set ili wapime , sauti, taa, umbali kutoka kamera na mambo mengine wakati setlingi akijiandaa kupiga scene. Ukiwa Stand in unakuwa na haki kwenye set kuliko extra, wanakuyheshimu kweli kweli! Unavalishwa nguo sawa na stelingi. Unakuwa karibu na director na wengine.

Nilibahatika kuwa Tonye alinikumuka na kunialika kuona RUINED. Tiketi ni vigumu kupata kwa vile imependwa kweli. Nimeshangaa kuona mchezo wa kuigiza inayohusu vita Afrika inapendwa hivyo na wazungu. Mengi yanasemwa katika huo mchezo kuhusu jinsi waafrika wanayotapeliwa madini kama almasi na dhahabu. Pia jinsi vijana wanavyoharibiwa na kuwa wauaji na malaya.


3 comments:

malkiory said...

Ingefaa awape somo waigizaji wa Tanzania wanaojiita ma super star. Huku kila siku wakiandamwa na skendo mbali mbali.

Anonymous said...

Nice pic!

Anonymous said...

Mama Bishanga ametoa semina kwa wasanii Dar. Nawe ungeenda kuwapa somo. Wote mmependeza.