Friday, January 28, 2011

Mtoto wa Miaka Mitatu Abakwa Kimara

Kuna mdau kutoka Kimara, Dar es Salaam ambaye ameleta habari hizi za kusikitisha na kutisha!

********************************************************************
MIMI NI MKAZI WA KIMARA STOP OVER GARAGE- KUNA MTOTO WA MIAKA 3 ALIBAKWA HAPA MAENEO YA KIMARA GARAGE MBELE KIDOGO YA KIMARA STOP OVER,,,KWA KWELI MKASA WENYEWE UNASIKITISHA UWEZI AMINI KAMA WATU NA AKILI ZAO WANAWEZA KUFANYA KITENDO CHA KUSIKITISHA HIVI HASA JESHI LA POLISI,,,,STORY YENYEWE ILIANZA HIVI,,,MTOTO MDOGO KWA JINA TUNAMHUIFADHI ALIRUDI KWA MAMA YAKE MCHANA KWEUPE AKILALAMIKA MAUMIVU SEHEMU ZA SIRI.

MAMA YAKE BAADA YA KUMPEKUA AKAMKUTA AKIVUJA DAMU KIBAO ILIYOCHANGANYIKA NA MBEGU ZA KIUME,,HUKU SEHEMU ZAKE ZA SIRI ZIKIWA ZIMECHANIKA KABISAAAAA. MTOTO BAADA YA KUULIZWA NANI KAKUFANYA HIVI AKASEMA FULANI (JINA TUNAMUHIFADHI)KWA KWELI MAMA ALIPIGA UKUNGA MAJIRANI WAKAJAA PALE,,BAADA YA KUAMBIWA KILICHOTOKEA WATU WAKAKIMBILIA KWA MBAKAJI NA MAWE NA MATAIRI WAMCHOME MOTO.

JAMAA TAYARI ALIKUWA KASHATOROKA SAA NYINGI,,IKABIDI WATU WAMSAIDIE MAMA KUMBEBA MTOTO NA KUMKIMBIZA KITUO CHA POLISI CHA MBEZI KWA YUSUF(MBEZI LUIS) WAKAPATA PALE PF3 YA MATIBABU NA RB YA KUMKAMATA MBAKAJI NA KESI IKAFUNGULIWA PALE,. KWA KWELI ILIBIDI UFANYIKE MCHANGO KIDOGO KUMSAIDIA YULE MAMA MAANA ALIKUWA HANA MUME WALA UWEZO KAZI YAKE YEYE NI KUWACHOTEA MAJI MAJIRANI NA KUPATA VIJISENT ANAVYOJIKIMU YEYE NA MWANAWE,.

MTOTO AKAPELEKWA MWANANYAMALA AKALAZWA...JIONI SASA NDO IKAWA KIMBENDE MAANA YULE MVUTA BANGI AU MBAKAJI ALIRUDI NA KUANZA KUWATUKANA WATU KWAMBA HAWAWEZI KUMFANYA LOLOTE,, ALIKUWA ANATUMIA JEURI YA KAKA YAKE ANA PESA NA HATA MKIMUWEKA NDANI ATATOKA TU (KAKA YAKE ANAFANYA KAZI TBL).NA POLISI AKIENDA ATATOKA TU ATA KWA UCHAWI.

WATU WAKAPIGA SIMU POLISI DEFENDER YA POLISI IKAJA IKAMBEBA SAA 5 USIKU AKALALA KITUO CHA POLISI MBEZI KWA YUSUF,,ALILALA LITUONI SIKU MBILI BILA HATA KUPELEKWA MAHAKAMANI. ,KATIKATI YA HIZO SIKU 2 SIJUI NDO MPELELEZI WA KESI AU POLISI HATA HATUJUI (HAWAKUWA WAMEVAA UNIFORM)KUTOKA KITUO CHA POLISI MBEZI WALIENDA HOSPITAL YA MWANANYAMALA NA KUMLAZIMISHA DAKITARI ANAYESIMAMIA VIPIMO VYA UBAKAJI AWAPE FAILI WARUDI NALO KITUONI DAKTARI AKAKATAA KATA KATA KUWAPA,,(KISHERIA HAMNA DHAMANA KWA MBAKAJI NI MAGERZA TU).

CHA AJABU SIKU YA 3 KESI IKACHAKACHULIWA NA POLISI ANAYEIPELELEZA! YULE MBAKAJI AKAPANDISHWA MAHAKAMANI KWA KESI YA UKABAJI BADALA YA UBAKAJI PATAMU HAPO..CHA AJABU HATA MJUMBE WA NYUMBA KUMI KUMI NDO ALITOA KIBALI CHA DHAMANA. HIVI KWELI HII TANZANIA TUTAFIKA KWELI KWA UNYAMA HUU? NASIKIA MAMA WA WATU KAJIFUNGIA NDANI NA MWANAWE KAZI YAKE NI KULIA TU. WATU WALIPOJARIBU KURUDI KITUONI PALE MBEZI ASKARI WAKASEMA ETI WALIKOSEA BADALA YA KUANDIKA MBAKAJI WAKAANDIKA MKABAJI.

WALIPORUDI KUJA KUMKAMATA YULE MBAKAJI TAYARI ALIKUWA AMETOWEKA KUSIKOJULIKANA. KAKA WA MBAKAJI ALITOKA AKAENDA KWA MAMA WA MTOTO NA KUANZA KUMTISHA KAMA AKIFUATILIA ZAIDI HII KESI ATAMHUAMISHA MJINI. INASIKITISHA JAMANI HEBU MTUSAIDIE HATA KUISUKUMA HII MSG TAMWA HATA KWENYE VYOMBO VYA HABARI ILI HAWA POLISI WALIOCHUKUWA PESA WASHITAKIWE....NAOMBA MSINITAJE JINA MIMI NILIERIPOTI VITISHO VIMEKUWA VIKUBWA !

ASANTENI SANA

MLALAMIKAJI

12 comments:

Anonymous said...

Huo kaka mtu apigwe! Khaa!

emu-three said...

Sasa nyie wananchi ndio mumeamua nini...mujue kuwa jana ilikuwa kwa huyo kesho ni kwenu...si na nyie muna watoto...haya,...kaeni kimya muone adhabu ya mungu itakavyowashukia...kutaneni, muoneni hata diwani au ikibidi muoneni mbunge...au watafuteni watu wa ustawi wa jamii/haki za watoto na akina mama...HAKI ICHUKUE MKONDO WAKE...Ikishindikana, MNAJUA LA KUFANYA...Kumbekeni, leo kwake, kesho...!

Anonymous said...

sijapata kuona nchi iliyokufa kama Tanzania

Malkiory Matiya said...

Utawala wa sheria haupo tena!

Anonymous said...

"Utawala wa sheria haupo tena"

Kwani lini ulikuwepo? au unataka kutuambia kwamba haya mambo ni mapya na yameanza juzijuzi tuu?

Anonymous said...

Inasikitisha kweli. Hapo mbo justice ikifanya kazi na kumwua huyo mbakaji ni halali kabisa!

Anonymous said...

Jamani, jamani jamani... Watanzania tunakwenda wapi.??
Wewe kaka unayejifanya una hela sana, kwa taarifa yako atakayefuata kubakwa na huyo mdogo wako ni mwanao. Hapo ndo utaenda vizuri kumuwekea dhamana.

Anonymous said...

Sasa we uliyeleta hii habari huyo mbakaji atakamatwa vipi kama hata jina hajulikani, mtaje jina huyo mtu ili iwe rahisi kumpata

Anonymous said...

Habari za asubuhi wapenda maendeleo

jana nimeshangaa sana nilijisikia kuumwa muda wa kama saa 3.30 usiku, nikaone niende hospitali au hata zahanati yoyote ya karibu nikaonane na mtaalamu wa afya,

nikaanzai elly charitable center- kuna mgao so wamefunga yaani hakuna umeme

aar- moroco- muda wa kazi umeisha

mount mkombozi ndo iliyonifanya niandike hii mail eti kutokana na mgao hadi wagonjwa wadini wanatumia mishumaaa!!!! kuna watoto wanalia ndani ya wadi hizo kwa maana wamelazwa ila kwa kutumia mwanga wa mshumaaa , hakuna hata genereta, sikutaka kuilaumu mamlaka haraka nilianza na wagonjwa wliopo pale ndani inakuwaje tunakubali kulazwa hospitali isiyokua hata na jenereta itakuwaje mtu akitaka kuwekewa oxygen au operation ya haraka, pale wamama wanajifungua, inakuage in case of any emergency?

kunawanaotumia insuarrance kama medex, aar,strategies, bima ya afya na wanaolipa cash woote hao wamekaa kimya kuhudumiwa pale . watanzania tutataka serikali itufanyie hata hilo............

Anonymous said...

Annoni wa February 01, 2011 7:19 PM, tufanyeni kama Misri tu hivihivi ni bora na wewe uingie kwenye utapeli tu, wanasema "if u can't bit them join them" hufungwi ukiwa tapeli Tanzania hii never, mi nishaamua kuingia huko naanza kujifunza kidogo kidogo tena kwa kuanzia naanza na uganga wa kienyeji mapemaa

Anonymous said...

Sad and shameful situation. Utterly disgusting:(

Anonymous said...

MPAKA FALSAFA YA "GIVE ME FREEDOM OR GIVE ME BULLET" ITAKAPOTUINGIA AKILINI WATANZANIA NDIO TUTAKAPO ONDOKANA NA HUU UOZO. VINGINEVYO TUENDELEE KUIZOEA HII HALI AU KAMA NDUGU ZETU WAKENYA WANAVYOTUITA BONGO LALA.