Monday, July 11, 2011

Kero ya KuBeep

Mdau African Man ameleta swali kuhusu simu za mkononi (Cell phone)kwa wadau, karibuni mchangie mjadala wake.

******************************************************************************

Assalam aleikum waungwana.

naomba uniwekee swali langu nipate michango ya wadau kuhusu hiki kitendo cha kubeep kwenye simu ya mtu. mimi ni mmoja wa watu wanaosumbuliwa sana na kukerwa na kitendo cha kubeepiwa katika simu. ninavyojua mimi simu ina huduma kama nne hivi ambazo ni kupiga simu (call), ujumbe wa sauti (voice mail), ujumbe mfupi (sms) na internet kama simu yenyewe ni smartphone. sijaona wala kusikia kuwa kuna huduma ya kubeep.

sasa inashangaza mtu kununua simu ya bei mbaya kisha kuanza kubeep watu ukimuuliza anasema hakuwa na salio. utashindwaje kununua vocha ya shilingi 5000 wakati una simu ya shilingi laki5? na mbaya zaidi unapompigia mtu anayebeep huwa aidha hana la maana la kusema au atajibu NILIKUWA NAKUSALIMIA MKUU!!!!. sasa hujiuliza kusalimia ndio huku au? mara kadhaa wanaobeep huharibu utulivu wa vikao maofisini, kusababisha ajali barabarani na hata vifo nk. baadhi ya ofisi hupiga marufuku simu kwenye vikao kwa sababu ya kero za wanaobeep.

kwa mtazamo wangu kubeep kutakuwa na maana iwapo kutakuwepo mazingira yafuatayo:

1. iwapo wahusika walikubaliana kuwa nikikubeep namaanisha kuwa nimemaliza kazi au nipo tayari kwa safari au utoke nje tuonane na mfano wa hayo.

2. iwapo wahusika wamekubaliana kuwa nikikubeep namaanisha kuwa unipigie kwa kuwa sina credit ya kutosha.

3. iwapo wahusika wamekubaliana kuwa nikikubeep namaanisha kuwa kuna ujumbe mfupi (sms) nimekutumia na umepita muda mrefu sijapata jibu hivyo nasisitiza kuwa unijibu hiyo sms.
ukiondoa sababu hizo hapo juu ambazo ni lazima wahusika wawe wamekubaliana kabla, kubeep kutaendelea kuwa kero na maudhi kwa wamiliki wa simu. inasikitisha kuwa watu wengi wanaendeleza tabia hii ambayo kwa hakika inakera sana. baadhi wakibeep usipowapigia hununa na kukasirika. sasa hujiuliza nini maana ya kubeep? ulitaka nikupigie kwa nini usipige wewe? au jee tuliweka makubaliano hayo kuwa ukibeep nikupigie? maswali ni mengi na majibu ni machache.

nadhani kuna haja ya makampuni ya simu kudhibiti hali hii aidha kwa kutoza fedha kidogo kwa wanaobeep au kuchukua hatua kali zaidi juu yao. kuwe na system kuwa ukibeep ovyo unaweza kufungiwa line yako nk. wakati mwengine mtu hubeep zaidi ya mara 10 na unapoamua kumpigia kwa kudhani kuwa labda kuna emergency au ana shida muhimu unaishia kupata majibu ya kijinga...aaah niliona nikusalimie tu mzee....au aah nipo hapa klebu karibu na kwako... na majibu mengine kama hayo. wakati mwengine ulikuwa umelala kabisa umechoka na mizunguko ya maisha au upo na kazi very sensitive na mtu anakuondoa stimu kwa beep za kijinga.
naomba wadau wanisaidie mawazo yao jee kubeep hasa kuna maana gani maana mimi nimechoka na hii kero.

mdau

1 comment:

Anonymous said...

Kwa nini umbeep mtu ili akupigie, si akupigie tu!