Saturday, July 02, 2011

OMBI KWA WAZEE WATARAJIWA WOTE - Tangazo

(Tandika Kilalakala - Wakina mama waliokusanyika sehemu moja kupata misaaada. wengi wao wana ulemavu wa kutembea, hawana kipato na mmoja ana wajukuu wawili walioachwa na wazazi wao)

( pichani - Magomeni Mzee Simba Maduwilo kwa sasa mlemavu wa miguu, na mkewe hali yake ya afya sio nzuri. Wanaishi kwa kumtegemea binti yao anaejishughulisha na mama lishe.)


Kwa mara nyingine tena TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION imetembelea wazee wanao ishi katika mazingira magumu na kutoa misaada mbali mbali.

TUSHIKAMANE PAMOJA FOUNDATION tunaomba watu watakaoguswa na watakaopenda kusaidia kikundi hiki kiendelee kutoa misaada kwa wa lengwa, tupigieni simu 0787 558550 au 0787 177077 au 0784 265560 au 0784 950250 Tunapokea nguo mitumba isiochakaa saaana, vifaa vya nyumbani, mashuka, vyakula vikavu, kama, unga, mchele, sukari, Mmaharagwe, majani ya chai n.k...

Bado wapo wazee wengi hatuja wafikia. Lengo letu ni kuwapa angalau vyakula kidogo mwezi mara moja.... TUSHIKAMANE PAMOJA TUFIKISHE MALENGO YETU.

No comments: