Saturday, July 09, 2011

Tapeli MNigeria Asafiri Bure kwenye Ndege za Marekani

Kuna habari kuwa Tapeli Mnigeria, Olajide Oluwaseun Noibi, alifanikiwa kusafiri kwenye ndege kutoka New York hadi Los Angeles mwezi uliopita kwenye ndege ya Virgin Atlantic bila tiketi. Habari zinasema kuwa jamaa alikuwa na Boarding Pass feki zaidi ya 10. Moja iliibiwa kutoka kwa mtu aliyepanda treni kuelekea uwanja wa ndege!

Kweli hao matapeli wa Nigeria wana buni kila aina ya utapeli! Ajabu hao walinzi wa TSA wanasechi watu mpaka kwenye chupi, wanadhalilisha watoto wadogo na wazee lakini walishindwa kumkamata huyo Tapeli!

Mnaweza kusoma habari zaidi pampja na Affidavit ya FBI kwa kubofya HAPA:

\

2 comments:

Anonymous said...

Ama kweli mtumwa ni mtumwa tuu. M-Nigeria kamuibia mzungu, house slave anasema "The nigeria man steals from us".

Wa-Nigeria wakiwaibia wazungu wewe tatizo lako ni nini hasa? kipi kikuwashacho?

Anonymous said...

Ukisafiri na ndege ni lazima ununue tiketi. Hakuna kusafiri bure. Jamaa ni mnigeria na pia ni mwizi. Itabidi waeleze jamaa alivyoweza kupita walinzi wa TSA. Lazima jina la kitambisho imechi jina kwenye boarding card.