Wednesday, November 02, 2011

King Kiki Safarini Boston

Saraji, Maneno, King Kiki, mimi na Charles Jackson

King Kiki Cambridge, MA leo jioni

Namkabidhi King Kiki Kanda ya Bongoland 2
Wadau, mwimbaji maarufu wa Tanzania, King Kiki, atafanya  Maonyesho maalum, huko Leominister, MA siku ya jumamosi.  Leo kanitembelea nyumbani kwangu Cambridge. Alikuja na vijana wengine wa Leominister ambao leo ndo nimewajua.  Nilikuwa nasikia majina tu. Nimefurahi mno kuwakaribisha ingawa kwa muda mfupi. Nilimpa  King Kiki zawadi ya DVD ya Bongoland II.

2 comments:

Mbele said...

Dada Chemi, shukrani kwa kutupa hii taarifa. Una bahati sana kukutana na Gwiji King Kiki, tena kakutembelea. Nimezipenda hizo picha. Vile vile, mahojiano ya King Kiki na blogu ya Vijimambo ilinielimisha sana. Gwiji anakumbuka mambo mengi sana, na anajieleza kwa ufasaha sana.

Chambi Chachage said...

dada chemi nipo cambridge, naomba unikumbuke kwenye matukio muhimu kama haya tafadhali, chambi