Friday, May 11, 2012

Binti wa Kibongo Boston Adai Kabakwa Ovyo Tanzania!

Wadau, leo asubuhi kazini niliulizwa kama ni kweli Tanzania haithamini haki za akina mama na kama wnaawake wanabakwa ovyo!  Kisa, ni story iiliyotoka kwenye TV jana jioni kuhusu binti MTanzania, Queen Butahe (19) anayeishi na familia ya kizungu huko Franklin, Massachusetts.

Kwa bahati nzuri jana jioni nilikuwa naangalia taarifa ya habari hapa Boston Fox 25. Wakasema, lazima usikie story ya binti ambaye kateswa na kuishi maisha ya ajabu Afrika.  Basi nikangojea story na kujiuliza ni nchi gani!  Nilidhani Congo. Ajabu, nchi ambayo inadaiwa kateswa kupindukia ni Tanzania!  Story ilivyopangwa utadhani Tanzania ni nchi ambayo mwanamke hana haki, hakuna sheria na wanawake wanabakwa ovyo! Mwisho wakasema kuwa Queen ana mradi wa kukusanya hela kwa ajili ya kujenga maktaba Tanzania! Yaani wadau, utadhani kuwa Tanzania haina maktaba hata moja.  Huyo binti ni yatima, familia yake wamekufa kwa UKIMWI. Natoa pole sana kwake. Lakini jamani, kuponda nchi hivyo!


Queen Butahe

Mnaweza kuona Kideo hapa:

   http://www.myfoxboston.com/story/18288735/overcoming-the-odds-and-giving-back

BOSTON - Maria Stephanos introduces you to Queen Butahe, a senior at Franklin High School, who is originally from Tanzania. Queen lost most of her family in Tanzania by the time she was six to HIV/AIDS. Only she and her brother had survived, and she doesn't know where he is to this day. For years she had been abused, and raped, and four years ago she had the chance to come to America with some relatives. She now lives the life of a normal American teenager, but doesn't forget the life she escaped in Tanzania. She is now raising money to help improve the education for young people in Tanzania, and help to build a library there. ( Ile story haisemi lakini sehemu anyaotaka kujenga ni Kwala, Tanzania.  Sijui ni mkoa gani lakini.)

*********************************

Wadau, nia yangu si kumponda huyo binti Queen.  Na ninapongeza kwa moyo wake wa kutaka kusaidia watoto waliobaki Tanzania.  Lakini kukashifu nchi nzima jamani!  Sehemu yoyote ukienda duniani kuna watu wabaya na wazuri.  Kwa kweli nilishikwa na hasira baada ya kusikia hiyo story, lakini nilisema huyo binti ni mdogo na huenda ni kweli kashindwa kumwambia mtu yaliyompata.   Anasema kuwa kabakwa na hausgeli, madereva wa mabasi, mjomba wake, mwalimu. Anasema kapata mimba ya mjomba wake akiwa darasa la saba lakini aliitoa.  Mwanzo nilidhani ni yatima ambaye alikuwa anaishi mitaani, lakini baada ya kwenda kwenye website yake nikagundua kuwa huyo binti alitoka kwenye familia waliojiweza. Alisomeshwa Olympio Primary na pia alikuwa anapanda School Bus. Ni ndugu yake ambaye alikuwa hapa Marekani ndiye aliyemnunulia tiketi ya kuja Marekani.  Wakati yupo hapa ndo kakutana nahiyo familia Franklin na kwenda kukaa nao.  Alikuwa na nafasi nzuri kuliko wengine. Na nadhani shangazi yake na hata huyo ndugu aliyemwezesha kutoka Tanzania kuja Marekani akisoma alivyoaandika watasikitika mno.  Anasema kuwa hata huyo ndugu yake wa Marekani! 

Na tusisahau kuwa Tanzania ina wanawake wengi wasomi, viongozi, na katika vyombo vya dola na sheria.  Hao anaodai walimbaka wangeweza kufungwa maisha!  Sheria zipo kulinda watoto dhidi ya ubakaji, kumbuka Mzee Maumba. Naona Queen hana habari kuwa gereza za Tanzania zimejaa watu waliopatikana na hatia ya kubaka watoto na kufanya maovu dhidi ya akina mama.

Ningependa kusika maoni yenu. Na pia wenye comments waambie Fox 25 kuwa nchi yetu Tanzani si jungle na tunathamini maisha ya watu wote!

37 comments:

John Mwaipopo said...

wakati fulani vitu vingine vinafanikiwa zaidi endapo vitatiwa chumvi. pengine anatafuta mchepuo wa maisha. a niche.

Anonymous said...

Queen alikuwa mwingi. Pia alionekana kutunzwa vizuri hakuwa anaishi maisha ya dhiki. Aliondoka kwa mbwembwe kuwa anakwenda kusoma US. Mungu ambariki lakini dhaaa Tanzania si nchi ya kishenzi anavyodai.

Anonymous said...

Naamini alivyosema. nakaa karibu na Franklin lakini ninaogopakumwalika kwangu baada ya kusoma stor yake. Nikimwalika naona atadai kuna mtu alitaka kumbaka!

Anonymous said...

huyo alitaka kupata makaratasi kirahisi kwa kusema kabakwa ladda kaomba ukimbizi anataka kupata makaratasi kirahisi

Mrs. Smith said...

Yet another story about what a terrible place that Africa is! I read her story and it is appalling that no one helped her all those years. Who paid for her abortion? The uncle?

Anonymous said...

Tatizo la wazungu hasa wamarekani wanapenda sana kuamini uongo, au habari yoyote iliyotiwa chumvi.

Ukisema neno lolote zuri kuhusu Afrika wazungu wanakuwa wagumu kukuamini.

Ila ukisema habari mbaya mara moja wanakuamini na kukusaidia.

Anonymous said...

Mwongo huyo! Asylum seeker! Eti atakuwa next Oprah. Tumwumbue jamani! Atakkuwa famous kwa kuiponda nchi yetu! No way!

Anonymous said...

Ni miongoni mwa wapumbavu wengi duniania, wako tayari kujidhalilisha na hata kuzikashifu nchi zao ilimradi tu wapate makaratasi ya kuishi marekani au ulaya!Ni mwongo, stori ya kutengeneza, mvivu wakutafuta..msaka huruma na tapeli wakutupwa! Watu wa aina yake wapo hapa Sweden, hasa wa Iran, wakishafika hapa wanaiponda nchi yao ili wapate huruma za waswed wapewe makaratasi....SIWAPENDI watu wa aina hii!

Anonymous said...

sikati kila mtu kutafuta mlo wa kila siku lakini alivyofanya si vyame. Ubakaji upo lakini si kwa kiasi hicho. Da Chemi wewe ni mwanachama wa TAMWA nadhani ni waandishi wa habari kutetea haki za wanawake hebu tafuta habari toka TAMWA zenye takwimu za ubakaji nk then omba interview na huyo familia au tv station utoe kama story. kwa sasa wanaharakati tunatafuta pesa kwa ajili ya kutoa elimu ya mapungufu yaliyo katika katiba na kufanyia marekebisho vipengele vinavyofanya sheria inalegalega naomba chukua muda wako ni aibu kwa nchi. hata kama anatafuta pesa

Anonymous said...

kama anataka kupata asylum basi bora asingizie amelazimishwa kukeketwa maana jina lake kama mkurya hivi, lakini kubakwa ovyo NO labda anapenda wanaume anawatege ndo maana mwalimu, mjomba, houseboy wote wamemaliza. pili anaweza kuwa na tatizo la kisaikolojia baada ya kuondokewa na wazazi wake

MSJ said...

Ilibidi niende kwenye website yake kusoma habari zake! Anadai kabawa na madreva wa Schol Bus wakipokezana kumbaka! Jamani, waliweza kufanya wapi sote tunajua mitaa ya Dar. Na hakuna mtu anayependa kuona mtoto anadhalishwa. Binti mwongo huyo. Wazungu wapesi sana kuamnini uongo juu ya Afrika.Da Chemi hebu toa taarifa kwa FOx kuwa huyo binti ni mwongo. Umeona anavyodaui kuwa hata ndugu yake wa Marekani kambaka! Kila tu kambaka. Ana nini mpaka kila mtu anatak kumbaka!

Anonymous said...

Sad story [as she MIGHT not have been able to confide in anybody before, about the rape and "abortion"], but as somebody stated above, I too take the story with a pinch of salt.

Chemi Che-Mponda said...

I find it hard to believe that she could no find anyone to confide in while in Tanzania. I also find it hard to believe that drivers took turns raping her in broad daylight. If someone suspected that, those guys could have been beaten to death! Abusing small children is something that is not tolerated!

It was a schoolteacher who brought to light the case of Athumani Ally Maumba, the man molested over 40 schoolgirls. some of the girls were her students. She noticed a pattern. I followed the case keenly as a reporter for Daily News and it was a groundbreaking story for Tanzania. Since then these issues are publicly discussed.

Anonymous said...

Pole mama Chemi kwa kazi.
Nazani hakuna anayeweza kujua ukweli hila ni huyo binti tu. Sasa kwa umri wake siwezi kuchukua maamuzi ya haraka kwamba amewadanyanya hao wazungu hili haweze pata namna ya kuishi huko majuu. Kama hamedanganya ukweli sikuzote ujitenga na uongo. Naomba mama Chemi ufatilie habari za huyu binti na ukweli utakuja kujulikana hata ukichukua miaka kadhaa naimani hipo siku tutafahamu ukweli.
Napenda kuwaasa watz wenzangu tusipende kuwa hasi sana kwenye habari zinazo lenga mabaya ktk nchi yetu. Tuwe watafuta ukweli na tutafanikiwa sana.
asanteni

Anonymous said...

mimi simwamini lakini inaweza kutokea kuna driver mmoja wa school bus alikuwa anakalawti na kukabaka katoto ka miaka 4 mpaka kakaharibu bibi mtu ndo alikuja kugundu late na alikuwa akimrudisha akiwa mwisho ilikusudi asishutukiwe anakadanganya na pipi na soda halafu anamwambia usiseme ukisema utafukuzwa shule hivyo inawezekana akafanywa hivyo

Anonymous said...

Jamani, inawezekana kuna kitu kilitokea. Lakini mbona kabakwa na wengi? Lazma kuna kitu kwake. Kwa nini kila mtu anataka kumbaka? Nadhani ndugu waliomsaidia wanajuta.

Anonymous said...

Ukitaka kupata hifadhi kirahisi Marekani na nchi nyingine za Magharibi tumia uongo kama anaotumia huyu binti. Kama wewe ni mwanaume sema wewe ni (ashakum) msenge na unanyanyaswa na kuteswa sana Tanzania kutokana na usenge wako. Utapata hifadhi mara moja.

Anonymous said...

Kwa nini asiwashitaki hao waliombaka? Anaweza kuwashitaki akitaka. Statute of Limitations haijaisha!

Anonymous said...

Huyu mtoto hawajui vizuri wazungu, bora angebaki underground asingejitangaza kwenye vyombo vya habari. Mnamkumbuka yule mwanamke wa kisomali Hirsi aliyesema uongo mwingi ili apate Asylum huko Uholanzi? Asylum aliipata na akawa anahojiwa na vyombo mbali mbali vya habari na mpaka akaingia kwenye politics akawa mbunge huko Uholanzi. Kumbe muda wote huo kuna investigative reporter anafanya utafiti story yake akaenda huko kote alipopataja, akakutana mpaka na wazazi wake, mumewe wa zamani aliyeko Canada akawainterview wote alipomaliza kazi kipindi kikatoka kwenye television.

Yuwapi Hirsi now, amekimbilia US ambako bado kuna giza. Sasa iko siku tu ukweli utajulikana. Video za aibu na uongo wa Hirsi zinaonekana dunia nzima sababu ziko posted kwenye youtube. Ukweli una njia yake ya kutoka tu hata kama itachukua miaka kibao.

Anonymous said...

SASA WAJAMENI YAANI HAKO KADADA KANA MASHINE YA NAMNA GANI KIASI MPAKA KILA MTU BONGO ALIISHA KABAKA! MAMBO MENGINE NA WAZUNGU SIO WAJINGA HATA KAMA WAMETOA HIO ISSUE KATIKA TV LAKINI UONGO NA WAO WALIKWISHA UONA ,. LAKINI ANASTAHILI SIFA KWANI KAWAPA FURSA WAMAREKANI KUJA CHUNGUZA KAMA THIS SHOUL BE A TRUE STORY OR FIKTION.

MIMI NAISHI SCANDINAVIA DENMARK NA KESI KAMA HIZO ZA KUONGEA UONGO UONGO ZIKO SANA HUKU , MTU ANADANGANYA MPAKA KUUA BABA YAKE NA MAMA YAKE MZAZI ILI ASAIDIWE APATE MAKARATASI ,KAMA NDIO MCHEZO WENYEWE NDIO HUO BASI MUACHENI LAKINI SASA TANZANIA IMEZIDI KUPAKAZWA MAVI TENA YA KUSILIBA KWA MKONO- HAPA KUNA MAKESI YA HAWA JAMAA ZETU WA KIUNGUJA WANAOMBA UKIMBIZI ATI WAO NI WASENGE (GAYS) NA HAWAKO HURU KUFANYA MAMBO HAYO ATI WANAPIGWA MPAKA KUUWAWA,AMBACHO SI KWELI KABISA . RAFIKI YANGU MDENISH KANIULIZA SIKU MOJA KWA NINI MNAWABAGUA WASENGE MPAKA MNAWAUA TENA KWA KUPIGWA MAWE HADHARANI ? NATIONAL STADIUM KWELI HII NI HABARI YA KUIPONDA TANZANIA NAMNA HII HATA KAMA MTU HAIPENDI?
KAMA NI HAYO MAKARATASI YATAWATOKEENI PUANI SIKU MOJA NA UONGO WENU USIO KUWA NA UJANJA.
MUNGU AM BARIKI HUYO DADA AZIDI KUFANIKIWA LAKINI AJIJUE YUKO HATARINI KWA STORI KAMA HIZI HATA MIMI NDIO NAONA TANZANIA KUNA MAKOSA LAKINI SIWEZI IKANDIA NCHI YANGU KIASI HICHO. MWAMBIENI BASI AKAOMBE KAZI YA UYAYA KWA BARAKA OBAMA KAMA ATAPEWA

Anonymous said...

I am writing this in English for the sake of the gullible white Americans who believe this girl.

I have been to Tanzania. If Queen wants to she can prosecute the people who abused her. There is a justice system in place. But, I can assure you that while there may be some truth to what she said it has been highly exaggerated. I talked to someone who knew her and her family and they say that she came from a privileged family. In fact, the woman cried when I showed her this story, not out of pity but at the hurt Queen has caused. I hope she gets what she wants out if life and living off her story.

Anonymous said...

Habari za kazi, nashukuru kwa wote waliotoa comments zao, kusema kweli huyo Dada anaweza kuwa muongo au mkweli pia. Ila kubakwa inaweza kuwa ajili kama ajali zingine. Kwani alikuwa mdogo kiasi gani hata asiweze kusema?? au alikuwa akipenda kubakwa??? angejua hata kina mama walioolewa wakati mwingine huwa wanabakwa kwa kuto kujua haki zao za msingi wala asingesema. Kwa nini aelezee huko USA?? wakosaji wataachaje kunyanyasa kama yeye anaenda kusemea USA?????

Anonymous said...

MTOTO HUYU NI MUONGO KUPITA MAELEZO ALIKUWA JIRANI YETU AMETUNZWA KWA MAPENZI MAKUBWA KULIKO UNAVYOWEZA KUFIKIRI NILIKUWA NAMUONA MAENEO YA KINYEREZI FAMILIA ILIYOMTUNZA NI YA HALI YA JUU NADHANI AMELIMBUKA NA MAREKANI LAKINI MUNGU YUPO!

Rev. Gilbert Kutta said...

I am her Family Member Senior Guardian. My name is NOT ANONYMOUS! I am Rev. Gilbert Phillip Kutta, her Mother's Brother and second to the mother in our Family! Her mother passed away, what a tragedy to our family! She calls herself Queen Butahe? ----- Better the media call her again and get the name of her real Father! You may call me +255766551733! I did contact her when this sad news just came to my notice through the Web! She finay ended up blocking my email to her and said "It is bye bye to you"! She has a mission in mind. I will never allow it to take place the way she has planned by putting to shame my Lovely country TANZANIA and my good family! --- and me in effect! I want her to come out again and say the Truth. I don't brush out all what she said! But we have descent ways to deal with all that took place and not the way it seems her new American Caretaker is using! We do not work on half truth/half false and cooked up stories pitched for gain! I am in contact, and continue to contact all who did that interview to get to know what motivated them to shoot it to the mass! To defame? To what gain? How much did they first make due effort to search for truth? Is it just because a simple girl has come up with a story they see interesting they shoot it to the mass? I have plenty more to say! I have entered this debate because I feel this the only way to seek for cure!
god Bless TANZANIA my mother land! I love you and will protect you!
Please Contact me at rnaioth@yahoo.com. If you can help me clear THIS MESS and help Queen come back to her senses not to defame her Mother, please do!
I need that help!
thank you all-
God bless and keep my daughter safe!

regards to you all-
its me:
Rev. Gilbert Phillip Kutta
rnaioth@yahoo.com
+255766551733
Morogoro, Tanzania!

Chemi Che-Mponda said...

Wadau, nimeongea na mjomba wa Queen, Rev. Kutta. Kwa kweli amesikitika sana na story aliyotoa Queen na kusema mengi aliyosema si kweli. Nimemwahidi kuwa nitawasiliana na huyo mwandishi Maria Stephanos wa Fox 25 na kumwomba afanye follow up story na kusikia upande wa ndugu wa Tanzania. Maria akikataa nitafikisha habari kwa wakubwa zake. Mimi ninafanya kazi katika media Boston na ninaelewa mambo yao. Maria anaweza kuona aibu na kusema tuache story kama ilivyo! Lakini mimi siwezi kuvumilia nikiona jina la Tanzania inachafuliwa hivi hivi.

Pia anasema kuwa baada ya kusoma blog aliwasiliana na Queen, lakini sasa Queen amemblock! Kwa nini amblock? Anaogopa kuumbuliwa?

Anonymous said...

Asante sana dada Chemi. Mimi namfahamu vizuri huyu binti kwa kweli hata mimi niliposoma hiyo story imenisikitisha sana. Familia iliyomlea wanalia kwa uchungu sana. Alilelewa katika maisha mazuri kwa jinsi ninavyomfahamu. Alikata mawasiliano na member wa familia yake yeye mwenyewe. Kama kuna jinsi anataka kueleza matatizo yake ili asaidiwe ni bora atumie njia sahihi na si kuchafua NCHI YAKE NA FAMILIA YAKE. Kwa kweli hao watu wa FOX25 wanatakiwa watoe habari nyingine ya kufafanua na kuweka bayana ukweli wa mambo yote.

Anonymous said...

Story Website! -http://www.wavuti.com/4/post/2012/2/the-story-of-queen-b.html

By "hadija"
21/05/2012 16:52

Queen. We know you and your biological parents and your adoptive parents. You are a great lie. Watch out what you are saying in public in the expense of others. You stroy is not true. Remember those who you call them names in public news will one day sue you and you will find yourself into big problem. You have a freedom of speech but not freedom to lie without any legal consequence. If you are doing these for money, you better stop it. You will be in jail and loose all your scholarship.
These are lies about your story: You did not escape from Tanzania, your uncle who lives in Boston brought you to USA, For your own desire, you went to live in Franklin, and one time you tried to sue your family for lies which you lost all the cases in court. The legal sytem has already find you lie. Watch out.

Anonymous said...

myy
28/02/2012 01:55

acha uongo huoni aibu lol mwanake mabo unayoongea hayana ukweli kabisa

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/2/the-story-of-queen-b.html#ixzz1wMywe6nZ

Anonymous said...

Ananikumbusha kisa cha Ayan Hirsi, Msomali wa Kenye alivyowadanganya Holland kuwa ni mkimbizi wa kutooka Somalia. Umaarufu akaupata na sasa hivi raha mustarehe USA.

Huyu mtoto anatafuta umaarufu kwa njia ya mkato, nampa hongera kwa ubunifu na kisha fanikiwa.

Anonymous said...

Regards to you all!
Jamani! Naamini hii Blog inataka kusaidia. Tena si vema kutuma tu ujumbe ili mradi umepata nafasi ya kusema kujulikana pasipo kujulikana kwa kujiita "Anonymous" halafu kusema neno kama "Huyu mtoto anatafuta umaarufu kwa njia ya mkato, nampa hongera kwa ubunifu na kisha fanikiwa" kwa kadamnasi! Je una maadili gani binafsi na kwa jamii katika kusema hayo?
Tafakari!

Anonymous said...

The Story of Queen B, continues as Hadija chips in...

10/06/2012

0 Comments

I promoted this comment by Hadija which was posted under the initial blog post on this website, "The story of Queen B" to a post for the purpose of making it more noticeable as did with "Upande wa Pili wa The Story of Queen B" post following Reverend Kutta's repsonse to the initial post as well.

Hi.

My name is Hadija.

It is very unfortunately to follow up the story of Queen and how the so called Rev. Gilbert Kutta is trying to do. I know this family very well. I know Queen’s dad in Boston. I actually met with him recently trying to get the story right. I know Gilbert too. What I have learned so far brings suspicious feelings about the agenda of Gilbert Kutta. There a lot of things about this Kutta family need to scare out with Queen’s dad in Boston.

First of all, I want to tell the world that the so called Rev. Gilbert Kutta is not a Reverent at all of any church. He is simply a teacher and he was my teacher. He used to be work with Assemblies of God church in Morogoro with Rev. Maboya and he got busted. He has never be a pastor.

The reason I am bring it up is to raise a question. Why is mwalimu Gilbert use Uongo to try to clear “oungo”? What gain is he getting here by calling himself a Reverent? If he lies about himself how can we trust what he is saying? Second to this is the way mwalimu Gilbert Kutta is trying to defense the sexual offenders and especially his brother-in-law Robert Butahe whom Queen she identify him by name. When I talked to Queen’s dad in Boston, he made it very clear that he, as a loving and caring dad, his job is not to protect his sister’s husband Robert Butahe. He is now asked the Government of Tanzania to lead the investigation about the whole allegations and explore all possible legal actions after the investigation is over. I asked him why he does not write and respond in these blogs, and he said, his way of dealing with things is not by posting in public blogs. I have found him more reasonable. If you listen him and compared with his brother Gilbert Kutta, you will see two different motives: one is trying to cover up the truth and protect the public shame of Kutta’s family and the so called Robert Butahe, and Queen’s dad is seeking the justice of his daughter for such an insane act.

My fellow Tanzanias, this family has a lot of issues. There are so many factors which need to be addressed here. For example, do you know that their mother who was brought here in Boston by Queen’s dad is also living in Shelters? Franklin Butahe, who is Queen’s brother who was also adopted and brought to USA, is living in foster care homes? What is thins Tanzanias? The family which is posting itself as descent and rich their mother is homeless in USA streets? Where is Wanyenda Kutta who is rich in Dar-es-salaam and high officer in Tanzania government asking her own mother to go live in USA streets. I asked Queen’s dad about this and he told me that his Sister Wanyenda Kutta is the one who told their mother to go and live in shelters in what is look like to be the deep hatred against their brother in Boston.

I think Queen’s dad in Boston can tell us more credible stories about this family than the self-appointed Reverent Gilbert Kutta.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/06/the-story-of-queen-b-continues-as-hadija-chips-in.html#ixzz1xUVYbBRp

Anonymous said...

The Story of Queen B, continues as Hadija chips in...

10/06/2012

0 Comments

I promoted this comment by Hadija which was posted under the initial blog post on this website, "The story of Queen B" to a post for the purpose of making it more noticeable as did with "Upande wa Pili wa The Story of Queen B" post following Reverend Kutta's repsonse to the initial post as well.

Hi.

My name is Hadija.

It is very unfortunately to follow up the story of Queen and how the so called Rev. Gilbert Kutta is trying to do. I know this family very well. I know Queen’s dad in Boston. I actually met with him recently trying to get the story right. I know Gilbert too. What I have learned so far brings suspicious feelings about the agenda of Gilbert Kutta. There a lot of things about this Kutta family need to scare out with Queen’s dad in Boston.

First of all, I want to tell the world that the so called Rev. Gilbert Kutta is not a Reverent at all of any church. He is simply a teacher and he was my teacher. He used to be work with Assemblies of God church in Morogoro with Rev. Maboya and he got busted. He has never be a pastor.

The reason I am bring it up is to raise a question. Why is mwalimu Gilbert use Uongo to try to clear “oungo”? What gain is he getting here by calling himself a Reverent? If he lies about himself how can we trust what he is saying? Second to this is the way mwalimu Gilbert Kutta is trying to defense the sexual offenders and especially his brother-in-law Robert Butahe whom Queen she identify him by name. When I talked to Queen’s dad in Boston, he made it very clear that he, as a loving and caring dad, his job is not to protect his sister’s husband Robert Butahe. He is now asked the Government of Tanzania to lead the investigation about the whole allegations and explore all possible legal actions after the investigation is over. I asked him why he does not write and respond in these blogs, and he said, his way of dealing with things is not by posting in public blogs. I have found him more reasonable. If you listen him and compared with his brother Gilbert Kutta, you will see two different motives: one is trying to cover up the truth and protect the public shame of Kutta’s family and the so called Robert Butahe, and Queen’s dad is seeking the justice of his daughter for such an insane act.

My fellow Tanzanias, this family has a lot of issues. There are so many factors which need to be addressed here. For example, do you know that their mother who was brought here in Boston by Queen’s dad is also living in Shelters? Franklin Butahe, who is Queen’s brother who was also adopted and brought to USA, is living in foster care homes? What is thins Tanzanias? The family which is posting itself as descent and rich their mother is homeless in USA streets? Where is Wanyenda Kutta who is rich in Dar-es-salaam and high officer in Tanzania government asking her own mother to go live in USA streets. I asked Queen’s dad about this and he told me that his Sister Wanyenda Kutta is the one who told their mother to go and live in shelters in what is look like to be the deep hatred against their brother in Boston.

I think Queen’s dad in Boston can tell us more credible stories about this family than the self-appointed Reverent Gilbert Kutta.

Source: http://www.wavuti.com/4/post/2012/06/the-story-of-queen-b-continues-as-hadija-chips-in.html#ixzz1xUVYbBRp

Rev. Gilbert Kutta said...

Regards to you all again!
1. "First of all, I want to tell the world that the so called Rev. Gilbert Kutta is not a Reverent at all of any church. He is simply a teacher and he was my teacher. " from http://swahilitime.blogspot.com/2012/05/binti-wa-kibongo-boston-adai-kabakwa.html - Oh really? I taught you? Where? ...... would you doubt my credibility as your teacher then under my care? ...... Kindly remind me where!
Glad to hear you were my Student! ..... This gives me more credibility as you can testify on my genuine service to you/all my students in that matter ...... my point here is, does that prevent me being a Pastor? You simply know but a tiny part of the Complex me! Kindly avoid defaming! I repeat, you know very little of me!
2. Again, "He used to be work with Assemblies of God church in Morogoro with Rev. Maboya and he got busted. He has never be a pastor. " ...... Kindly get hold of my Passport and see that the Same church wrote a Covering letter to the Immigration office in full consent of my status! -Please be careful in all this!
3. "Why is mwalimu Gilbert use Uongo to try to clear “oungo”? What gain is he getting here by calling himself a Reverent? If he lies about himself how can we trust what he is saying? " - Well, does number 2 above show to the World that this is not true? Kindly address me as Pastor and your teacher next time!
4. "Second to this is the way mwalimu Gilbert Kutta is trying to defense the sexual offenders " - was there a need for this question at all? Can this contributor quote me anywhere in my contributions to the effect? ------ this comment only shows how my good contributor in this shaming message to the world about has a hidden agenda to defame for own reasons or has a hidden hand in all this under the name Hadija!

oops! will come back soon!
Regards!
Rev. Gilbert Phillip Kutta;
Teacher for many including Hadija!

Rev.Gilbert said...

I read this! "May 11, 2012 12:40 PM
Mrs. Smith said...
Yet another story about what a terrible place that Africa is! I read her story and it is appalling that no one helped her all those years. Who paid for her abortion? The uncle?" .................. Please? Who suggested about the uncle in favour of Queen's abortion? Which uncle? Certainly not me, Rev. Gilbert Kutta. did this person try to suggest the self acredited Queen's dad in Boston on the effect? --- May be!

Anonymous said...

nivizuri abakwe kweli sasa, mshenzi ametuchafua! hakuna anayeweza kumuadabisha? ningekuwa mbakaji ningembaka kama lawama tumepewa za bure! damn!....

Anonymous said...

Aerobic activities include activities that increase the heart rate and work the larger muscle groups.
Children are becoming more unfit by the year leading to massive health issues in years to
come. You are buying used fitness equipment so that you will be able to get your self in shape not so that you
have to worry about problems down the line.

Review my website :: cheap gyms

Anonymous said...

Hi there friends, its impressive paragraph on the topic of educationand completely explained,
keep it up all the time.

Feel free to surf to my web page เกมส์ pc