Thursday, May 24, 2012

Mwanangu Apata Nondoz!

Wadau, nafurahi kuwatangazia kuwa mwanangu Elechi Henry Kadete amepata shahada, Degree of Bachelor of Arts' kutoka Chuo Kikuu cha Brandeis (Brandeis University), Waltham, Massachusetts.  Major yake ilikuwa ni Business.  Sherehe ilikuwa jumapili iliyopita. Kweli safari ilikuwa ndefu na kulikuwa na matuta mengi njiani, lakini kafika. Baba yake marehemu Prof. Henry Kadete, lazima anatabasamu kutoka mbinguni.

Brandeis ni Chuo Kikuu cha Wayehudi, lakini wanapokea wanafunzi kutoka nchi mbalimbali na dini mbalimbali.  Imam alisoma sala ya kufungua sherehe. Baadaye Rabbi wa kiyehudi, na Padre wa Kikristo walitoa sala za kufunga sherehe.


Hongera Elechi!


L-R Dr. Aleck Che-Mpomda (babu), Mimi, Elechi, Camara (kaka), Malaika (mama mdogo) na Mrs. Che-Mponda (bibi)  Watoto wadogo ni watoto wa Malaika
Mimi na Elechi
Elechi na Bibi na Babu yake

Mama na Mwana

Graduates wa  Bachelor of Arts wakitoka ukumbini
Elechi akiwa na siku tatu tangu azaliwe,, Hapa ni 21 Kileleni Road UDSM 1989
Imam akisuali kabla ya ceremony kuanza

Elechi na Babu yake, Dr. Aleck Che-Mponda

12 comments:

Yasinta Ngonyani said...

HONGERA SANA KWA KUFIKIA HAPO ULIPOFIKIA ILA NAKUTAKIA MEMA UENDELEE. NA HONGERA PIA KWA WAZAZI

Anonymous said...

Hongera sana Mama Elechi, Umemlea mwanao hadi amepata Degree yake. Mungu amjaalie sana Elechi, na huo uwe ndiyo mwanzo tu wa Mafanikio M. Mungu amjaalie hadi aje apate Ph.D.

Nakutakia heri wewe na mwanao.

Exaud said...

Hongera, mwambie aje kuchangia maendeleo ya TZ.

Anonymous said...

Hongera Elechi, Hongera Da Chemi kwa malezi bora.

Anonymous said...

Hongera sana kijana pia na mama hongera zake kwa malezi bora hadi ukapata ufahamu wakusoma.

Anonymous said...

Hongera.

Anonymous said...

hongera mdau kwa nondoz...halafu da chemi umefanana sana na mtoto wako.hivi ilo jina elechi linatokana na yule elechi amadi nini?

Chemi Che-Mponda said...

Anony 6:21PM, marehemu Prof. Kadete alisoma Undergraduate Nigeria enzi za Inter Africa university miaka ya 70. Pia tulikuwa wapenzi wa African wrters series.

Anonymous said...

Dah! Kweli mama yako ni mungu wako hapa duniani. Hiyo picha inayokuonyesha umekabeba ka-Elechi kakiwa na siku tatu tu nimeipenda sana. He should show this to his grandkids someday. Time really flies and I hope Elechi understands just how valuable you are to him. Hongereni sana Da Chemi na Elechi.

Mdau,
Dar es Salaam.

Mbele said...

Hongera sana. Shukrani kwa kumbukumbu zote hizo, hadi Kileleni, UDSM. Kila la heri.

Anonymous said...

Hongera kijana. Namkumbuka marehemu baba yako alinifundisha pale udsm mwaka wa pili. Alikuwa mwalimu mzuri sana na alitujenga katika kujiaminimi.

John Mwaipopo said...

i can see another profesor kadete in making. hongera mama, babu na bibi.

da'chemi you resemble your son sana, pia features nyingi mmechukua kwa babu, hasa pua.