Saturday, May 05, 2012

Kwa Mara Ya Kwanza Nimembusu Mzungu!

Wadau, katika maisha yangu sikutegemea kuwa nitakuwa na uhusiano wa kimapenzi na mzungu. Wiki iliyopita nilimbusu mzungu mdomoni kwa mara ya kwanza! Duh! Ajabu ilikuwa ni sawa na kumbusu mweusi, sema lips zao nyembamba zaidi.

Add caption
Ni  hivi, nilikuwa katika mchezo wa kuigiza, 'Can I Buy You a Drink?' ambayo ilikuwa moja wa micheo katika Six Playwrights in Search of a Stage. Ilifanyika Roxbury Community College, MainStage Ijumaa iliyopita. Katika ile rehearsal ya mwisho (yaani Dress Rehearsal) hakutokea kijana (Jeff pichani) ambaye alikuwa anaigiza kama mume wangu.   Basi Cliff  Blake (pichani) ambaye alikuwa anaongoza mchezo wetu, alishika nafasi yake. Ilipofika sehemu ya busu, tukapiga busu kama kawaida.  Makofi!!!!!   Cliff Blake ni msanii Professional hasa!  Karibu ataenda Broadway.

Katika mazeozi, nilikuwa na cheka maana huyo Jeff ambaye alikuwa anaigiza kama mume alikuwa ananiogopa kwanza. Alipoambiwa anibusu kasema, 'kwa kweli hajisikii vizuri kufanya hivyo'. Mwongozaji Mkuu, Marshall Hughes, kamfokea " Kijana, wewe ni msanii hebu fanya kazi yako!"  Na mimi nikamwambia Jeff, "Ushukuru hatuvuii nguo hapa!" Kacheka, kanibusu....hakuota mapembe wala kugeuka chura. Baada ya hapo kawa ananibusu kama kawaida mpaka mwisho zikawa kali. Ndo kazi ya msanii.

Mchezo, Can I Buy You A Drink, umeandikwa na Con Chapman. Katika mchezo huyo mimi na mume tumestarehe kwenye baa, anatokea jamaa kutusumbua (Emil Kreymer). Basi tunaamua kumkomoa kwa kujifanya sisi ni wapenda ule mchezo wa Bondage na kumwalika kujiuna na sisi, halafu jamaa anakimbia.

Ilikuwa mara yangu ya kwanza kushriki na Roxbury Repertory Theatre. Niliambiwa ni vigumu kuingia huko na watu wengi wanatokea kwenye auditions zao. Basi nilienda kwenye audition na hofu kubwa lakini siku hiyo ya kwanza nilipoenda nilipata nafasi! Mungu yu mwema!

L-R - Cliff Blake, Chemi, & Jeffrey Chrispin

(l-r Mtunzi wa Mchezo wa Kuigiza 'Can I Get You a Drink'  Con Chapman, Chemi, Jeffrey Chrispin na Emil Kreymer

5 comments:

Anonymous said...

Sioni kubusu mzungu ni jambo la ajabu!!!Usituletea mambo ya 1820.Hii ni 2012 binadamu wote ni sawa.mambo ya kuogopa mzungu hiyo ni nafsi yako na ushamba wako!!!!

Anonymous said...

Hongera Dada Chemi. Umenichekesha na mambo ya busu.

Anonymous said...

Da Chemi nakuheshimu kwa vile huogopi kusema unachofikiria. Waafrika wengine wanataka kwa nguvu mzungi. At leasti umepata kaonjo.

Anonymous said...

Da Chemi umependeza...huzeeki...hongera

John Mwaipopo said...

Da da mkubwa Chemi, kama ailvyosema mchangiaji mmoka hapo juu, huna-ga unafiki katika lile unaloamini kimtazamo wako.kama kutopenda kushirikiana na race nyingine ni jambo la kizamani, basi hata racisim haifai kuendelea kwani nayo ni jambo la kizamani